Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Kelele za lissu ni za mfa maji tu...tuzipuuze
Ndugu zanguni imefika wakat naona kuna wanasiasa wanaleta kila aina ya uchochezi dhid ya nchi yetu lengo lao nikuwachonganisha wa tz na serikali yao kwa uzushi wa maneno na mipasho isiyo na tija....ni upuuz mtupu unaoongelewa na lissu...mwenzetu kahongwa nawazungu aivuruge aman ya nchi....tumpinge kwa moyo mmoja kuonyesha uzalendo wetu kwa taifa.....
 
Zilikua mitumba zile, nani akamate mitumba? Baada ya kuzodolewa kuwa wanatununulia mitumba kwa bei ya Mpya ndo wakaamua kununua kapya, hapo ndipo mwenye Mali akaona hapo ndipo pakupata ule utajiri wa mzembe moja hivi.
Hapo ndipo mwenye Mali, kwa msaada wa nyumbu kiongozi wenu wakaamua kuzingua.
Huwezi mtoa Lisu kwenye hii equation, if you're intelligent enough.
 
Kelele za lissu ni za mfa maji tu...tuzipuuze
Ndugu zanguni imefika wakat naona kuna wanasiasa wanaleta kila aina ya uchochezi dhid ya nchi yetu lengo lao nikuwachonganisha wa tz na serikali yao kwa uzushi wa maneno na mipasho isiyo na tija....ni upuuz mtupu unaoongelewa na lissu...mwenzetu kahongwa nawazungu aivuruge aman ya nchi....tumpinge kwa moyo mmoja kuonyesha uzalendo wetu kwa taifa.....
Mbona ww umehongwa na lumumba kuleta post ya kutupotosha,wakati ukweli umeshajulikana?for,now watanzania wanajielewa,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nchi tuikodishe tu, maana tuliowapa dhamana ni watu wa hovyo kbs
 
Ninaleta tafakari hii nikifahamu watu tuko kwenye "kilio".Watu tunalia kusikia tunaenda kulipa around bilioni 90 kwa "magenge" ya waporaji wa rasilimali za waafrika,mintarafu Tanzania.Binafsi nimeumia sana moyoni.Ninaugua moyoni kusikoelezeka! Bilioni 90 za watanzania wapewe "mbwa" hivi hivi tu?

Ugumu Wa kukubaliana na jambo ambalo sio sehemu ya mipango yako na hasa pale ambapo hali au jambo hilo sio sehemu ya rajua au mission yako ndio mazingira anayokutana nayo Yesu Kristu kwa mjibu wa Injili ya Matayo 15:21-28.

Katika Dominika ya leo,Mwinjili Matayo anaelezea kisa kilichomkuta Yesu alipotembelea miji ya pembezoni ya Tiro na Sidoni.Tunahabarishwa kuwa Yesu alipofika huko aliendewa na mama Mkananayo akimuomba amtoe mapepo mwanaye aliyekuwa anasumbuliwa nayo kwa muda mrefu sana.

Kadri ya Matayo,mama yule alikuwa akilipuka kwa kilio cha makelele yaliyopindukia kumuomba Yesu amponye Huyo mwanae.Cha ajabu kabisa,Yesu hakumjibu chochote yule mama dhidi ya ombi lake lile.Yesu hakuguswa na hayo makelele na nwe ya huyo mama.

Matayo anasema baada ya mama yule kuona Yesu haja-mind kilio cha yule mama,mama alizidisha "mwano" (alizidi kuhanikiza kelele) hadi Mitume wakakereka na kumuomba Yesu aingilie kati ili mama huyo aweze kuachana nao maana zile kelele zilikuwa hazivumiliki kwa kweli.

Basi kwa kadri ya Injili ya Matayo,ndiposa Yesu anawajibu Mitume kuwa yeye hakutumwa kwa wengine isipokuwa kwa kondoo (watu) waliopotea wa nyumba ya Israeli Na ndipo katika mazungumzo hayo,yule mama alimuomba tena Yesu amsaidie.Lakini katika Hali tena ya kushangaza Yesu akamueleza yule mama kuwa si vizuri(busara) kuchukua chakula kilichoandaliwa kwa ajili ya watoto na kuwagawia mbwa!

Mama yule baada ya kujibiwa vile,kuwa inawezekanaje,chakula cha watoto wapewe mbwa yeye akamjibu Yesu: "..hata mbwa hushiba kwa makombo yatokayo mezani kwa bwana zao"! Basi baada ya Yesu kujibiwa vile akasema..." Mama imani yako ni kubwa sana na iwe kama utakavyo..."

Ndugu wana-JF,kuna fundisho moja kubwa sana ambalo Yesu alikusudia Mitume,yule mama na hadhira yote ile iliyokuwa ikishuhudia mkasa ule walipate.Kila tendo,neno au sala( fikra,tafakari) alilolifanya Yesu alikusudia liache alama katika akili na mioyo yetu.

Kwanza kabisa Yesu alikuja kuokoa ulimwengu kwa kuanza na Taifa la Israel (kondoo waliopotea wa Nyumba ya Israel) na ndio kisa anawakumbusha Mitume jambo hilo.Isingewezekana Yesu aende kila mahali wakati ule.Ilikuwa lazima Yesu atumie "sample" ya Waisrael kukamilisha ukombozi wa mwanadamu na mataifa mengine yangefikiwa na Mitume na watu wengine ambao wangetwaa wajibu huo kama ilivyo Leo.Hiyo ndo ilikuwa mission.Vision ilikuwa kuwakomboa wanadamu:kutupatanisha tena na Muumba wetu.

Kwa hiyo,Yesu anapowajibu Mitume kuwa yeye ana-deal na wanakondoo waliopotea wa nyumba ya Israel,anataka kusisitiza kuwa katika maisha (jukumu lolote lile) ni lazima na muhimu kwanza kulinda lengo kuu.Kwamba ni muhimu kutekeleza mission kwa usahihi na kikamilifu.

Na katika kuthibitisha hilo,pamoja na baadaye kukubali kutekeleza ombi la yule mama kwa kumuwingia mwanaye mapepo,Yesu bado anasisitiza juu ya umuhimu wa kutunza lengo kuu na mission kwanza.Kumwambia mama mkananayo kuwa chakula cha watoto si kwa ajili ya mbwa ni kurudia kile ambacho alikuwa ameshawajibu Mitume..." Nimetumwa kwa ajili ya wanakondoo waliopotea..."

Katika maisha yetu,yawe ya kisiasa,kifamilia au kiuchumi,wengi tunashindwa kufikia malengo kwa sababu ya kutotazama na kuona malengo yetu makuu ni yapi.Wengi wetu tunaokota kila tukutanacho "njiani". Hivi jiulize ukitaka kusikiliza kila kelele ya mbwa wanaobweka njiani utafika saa ngapi unakokwenda? Bila shaka,safari itakufa na matokeo yake itakuwa kuanza Kugombana na kufukuzana na hao mbwa wanaobweka.

Katika ngazi ya familia,tunaalikwa kujenga na kuimarisha kwanza familia zetu kwa hali na mali kabla ya kuelekeza akili zetu kwingineko.Familia moja ndio kitovu cha mabadiliko na majengeko yawayo yoyote yale katika jamii.Ndio kule kuhakikisha kwanza watoto wameshiba na kisha ndio mbwa nao wale; ndio kule kuhangaika kwanza na kondoo waliopotea..)

Katika ngazi ya kisiasa na kiuchumi: tunao mfano mzuri hapa nyumbani.Tunaye Raisi Magufuli.Toka kuapishwa kwake,Raisi Magufuli,aliweka wazi yeye amekuja kwa ajili ya Tanzania.Tanzania ya wanyonge na maskini(Rejea: kondoo waliopotezwa na Mafisadi;na chakula cha watoto).

Kuwahudumia na kufanya kila kitu kwanza kwa ajili ya Taifa lako hicho ndio lazima kiwe kipaumbele cha kila mtanzania.Kuumia,kuugua na kufumwa fumwa moyoni kwa ajili ya watanzania wenzako huko ndio kuongoza kwa usahihi na Ukamilifu.

Nchi hii ilikuwa imegeuzwa shamba la bibi.Baadhi ya watendaji,wanasiasa na wafanyabiashara ("mbwa") walikuwa wanakula chakula watoto. Kuna watu kwa miongo mitatu wao walifanya kazi si kwa ajili ya "wana-israel" (watanzania mafukara na maskini).

Hivi inakuwaje,"mbwa" wanatoka huko nje wanakuja hapa wanaomba tenda kumbe lengo lao ni kuliibia Taifa na sio kujipatia faida halali kwa misingi ya makubaliano? Kujiamini huko walikutoa wapi? Si kwamba walizoea na walikuwa wakifahamu kuwa watanzania sio watu focused? Si kwamba walijua mtanzania ukimkuta anaenda Kariakoo ukimpiga "sound" tu anaweza kubadili uelekeo kwenda Mbagala licha ya kwamba haikuwa sehemu ya ratiba yake?

Makandarasi-mbwa kwa nini walikuwa na walizoea kuja hapa Tanzania na kujichotea chakula cha watoto kiasi kile? Kandarasi anaomba kazi halafu analipwa na kisha hafanyi kazi kwa mjibu wa makubaliano na bado anataka aachwe hivyo hivyo tu!

Angalia: anatokea Mtu mmoja anasema kama "mbwai iwe mbwai",lakini wanatokea watu "wanakuwa- compromised" na mkandarasi-mbwa ili Serikali ishindwe katika Mabaraza ya usuluhishi ili yeye anufaike.Mbwa wanashiba at the expense ya watoto kulala njaa!

Kandarasi-mbwa sasa kwa kushirikiana na watu ambao wao wameshiba wameendeleza dhuluma ya kutafuna chakula cha watoto.Watu wanafurahia na kuchekelea.Watu wanapiga kengele za madebe na majembe kufurahia Mali ya walala-hoi kushikiliwa huko Canada.Watu wanashadidia kwa matusi na kejeli kuwa Raisi Magufuli ndiye tatizo!

Tuko katika shida kubwa sana kama nchi.Watu wanaharibu mambo waziwazi na mchana kweupe.Hatua zinachukuliwa na wale waliotakiwa kwenda huko mahakamani wakaeleze kinagaubaga jinsi makubaliano yalivyovunjwa hawafanyi hivyo na kama ilivyostahili ila matokeo yake mtu mwenye nia njema ndiye anawambwa msalabani!

Pole sana Raisi Magufuli! Watoto unaowapigania na unaowatafutia chakula hawajali.Watoto wako hawaoni shida chakula chao kuliwa na mbwa.Nikutie moyo iko siku utashinda.Fidia hizo hazitoenda hivi hivi tu lazima na "mapepo" ya walioshiriki kutoa chakula cha watoto yatatibika tu.Kaza kamba.Kuna watoto wanaona uchungu chakula kuvamiwa na mbwa.
 
Kelele za lissu ni za mfa maji tu...tuzipuuze
Ndugu zanguni imefika wakat naona kuna wanasiasa wanaleta kila aina ya uchochezi dhid ya nchi yetu lengo lao nikuwachonganisha wa tz na serikali yao kwa uzushi wa maneno na mipasho isiyo na tija....ni upuuz mtupu unaoongelewa na lissu...mwenzetu kahongwa nawazungu aivuruge aman ya nchi....tumpinge kwa moyo mmoja kuonyesha uzalendo wetu kwa taifa.....
Uchochezi gani tuambie? Kwani wewe ni nani? Mbona hayo ni maneno yako tuu? Wakati serikali tena ikulu inakiri wewe muoga na mahaba umekomaa tu acha ujinga pevuka wewe!!!!!
 
Kwenye uzi naona wametajwa WANASIASA, sijaona mahali walipotajwa WAPINZANI, but naona hoja zote zinaelekezwa huko? Yu mkini hao wanasiasa wanatokea Makinikia humo humo, so tusiwe wepesi wa kupindisha mada na kuhukumu. Napita tu
Mwanasiasa aliyetajwa kwenye vyombo vya habari ni Tundu Lissu anawatoa makasi.... Huyu ni nani kama si mpinzani. Lawama zinaelekezwa kwa Lissu. Sasa wapi ambapo hatujaelewa au hujaelewa?
 
Kelele za lissu ni za mfa maji tu...tuzipuuze
Ndugu zanguni imefika wakat naona kuna wanasiasa wanaleta kila aina ya uchochezi dhid ya nchi yetu lengo lao nikuwachonganisha wa tz na serikali yao kwa uzushi wa maneno na mipasho isiyo na tija....ni upuuz mtupu unaoongelewa na lissu...mwenzetu kahongwa nawazungu aivuruge aman ya nchi....tumpinge kwa moyo mmoja kuonyesha uzalendo wetu kwa taifa.....
Hatutaki na Usicheze na Iman,Watanzania Tulio wengi Tunamwamini TUNDU LISSU.Kazi kwako kututoa Iman.
 
Kelele za lissu ni za mfa maji tu...tuzipuuze
Ndugu zanguni imefika wakat naona kuna wanasiasa wanaleta kila aina ya uchochezi dhid ya nchi yetu lengo lao nikuwachonganisha wa tz na serikali yao kwa uzushi wa maneno na mipasho isiyo na tija....ni upuuz mtupu unaoongelewa na lissu...mwenzetu kahongwa nawazungu aivuruge aman ya nchi....tumpinge kwa moyo mmoja kuonyesha uzalendo wetu kwa taifa.....
Sijui kwanini idadi ya wajinga imeongezeka awamu hii.

Sent from my SM-G610F using Tapatalk
 
Kelele za lissu ni za mfa maji tu...tuzipuuze
Ndugu zanguni imefika wakat naona kuna wanasiasa wanaleta kila aina ya uchochezi dhid ya nchi yetu lengo lao nikuwachonganisha wa tz na serikali yao kwa uzushi wa maneno na mipasho isiyo na tija....ni upuuz mtupu unaoongelewa na lissu...mwenzetu kahongwa nawazungu aivuruge aman ya nchi....tumpinge kwa moyo mmoja kuonyesha uzalendo wetu kwa taifa.....



Halafu kuna watu wanajiita viongozi kumbe wamechaguliwa wapiga kura misukule kama wewe!Hivi Lissu ndiye aliyelifikisha taifa letu hapa lilipo hadi kuwa kama shamba la bibi?
 
Maendeleo ya nchi kwa historian yake yanahujumiwa na watanzania wenyewe toka upate Uhuru mwaka 1961.

Tumepitia vipindi vingi sana vya kupambana wenyewe kwa wenyewe Katika kuwaletea maendeleo wanainchi kutokana na baadhi ya watanzania kutopenda kuona Serikali yetu inafanya vizuri.

Wengine mpaka walishakuwa wakimbizi wa kisiasa nchi za ulaya toka utawala wa Mwl Nyerere kwasababu ya kutofautiana kwa mitazamo ya Siasa za nchi.

Baada ya hapo tumeona viongozi wanajilimbikizia Mali na kuwaacha watz na umasikini wa kutupwa.

Misaada mingi imetafunwa na kuandika report za uwongo kwa wafadhili ili mradi tu Serikali ionekane haifai.

Kumekuwa na tabia ya kuiba nyaraka za Serikali na kuwapa watz wasiokuwa na mamlaka kisheria kuwa nyaraka hizo ili tu kuonyesha Serikali haifai kuongoza.

Haya mambo yasipodhibitiwa kama Taifa basi Kuna siku hatutaelewa nani ni mkweli ktk taarifa kwa wanainchi Kitu ambacho ni hatari sana kwa AMANI ya nchi na Taifa kwa ujumla wake.

Watanzania wanahitaji Huduma nzuri za jamii..Elimu,Afya,Maji,Barabara na Huduma nzuri na bora kutoka ofisi za umma mfano Mahakama,Halmashauri zetu,Taasisi zake na bila kusahau Huduma za Majeshi kama Polisi Uhamiaji na Jeshi la zimamoto n.k
 
Back
Top Bottom