Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Tundu Lisu akiendelea hivi ipo siku atapata madhara kisiasa tena makubwa! Ni rahisi sana wanasiasa wenzake kumchafua kisiasa kuhusu ushirikiano wake na hawa mabepari

View attachment 570244

Sent using Jamii Forums mobile app

Tundu Lissu hahitaji kura za wanafiki. Kama atakosa kura kwa kusema kweli acha tu akose lakini taifa lijue viongozi wanaowachekea ndio wanaowaangimiza.
 
sjaewa wanasiasa wanaingia vipi hapo alitakiwa afafanue kama ndo wao walio sababisha ndege kuzuiwa au
Kuna jamaa mmoja nilimkuta kazini wakati naanza kazi.

Muhuni muhuni hivi. Aliniambia "siku zote kazi ikikushinda lazima uwe na story ya kutoa ili kuwa na exit strategy".

Bahati nzuri ushauri wake sikuuhitaji. Maana kazi haikunishinda.Ila nilijifunza watu wanavyofanya kazi.

Sasa hapa kilichotokea mpaka hiyo habari ya wanasiasa kuchomekwa ni kama vile serikali kazi imewashinda, wanatafuta kuchomeka story ya ku distract watu. Ku save face kama si exactly exit strategy.

Hapo kwa watu tunaojua kuangalia vitu vinavyo matter na kutoa ujinga wa distraction tunaona hivi.

Serikali inadaiwa deni. Haijalipa. Ndege inekamatwa mpaka serikali ilipe deni.

Hiyo ndiyo habari ya msingi.

Hizo longolongo za wanasiasa ni distraction.

Serikali ingekuwa haidaiwi deni huyo mwanasiasa angeanzia wapi kujipenyeza katika sakata hili? Angetunga deni la uongo na kuliweka kwenye akaunti za serikali?

Sent from my Kimulimuli
 
Samwel mathayo takataka wewe...hata hujui unachokiandika!
Punguza kuandika pumba humu ukitegemea uteuzi...watu tupo kwenye shida we unaandika mashudu hapa!
Pathetic!
 
Aliyesababisha ilo deni kwa hulka ya maamuzi ya kukurupuka afikishwe mahakamani haraka sana kwa kosa la kuhujumu uchumi na kuliingizia taifa hasara.

Maamuzi bila busara na hekima ili kufurahisha raia wasiojielewa yatagharimu nchi fidia nyingi.
Tatizo la nchi hii ni washangiliaji wa...mfalme
Daima ujinga umekua mtaji mkuuu
Elimu Elimu Elimu

Anagawa taifa kuaminisha raia maskini kuwa wako hivyo kwakua wenye magari na nyumba za "bati " wamekua wakiwaibia hivyo yeye amekuja kufanya wote tuishi nyumba za nyasi
Bahati mbaya sana mtu asiye na elimu hufurahia sana mtu akishuka ....methali kama "aliye juu mngojee chini ...inafanya watu wabaki kuamini watu wadondoke

Tunahitaji fikra ya "aliye juu...mfuate huko...huko"
Zaidi tujue hata Marekani maskini wapo
 
Hata yeye anakwamisha maendeleo ya nchi kwa kuwaandama wawekezaji wa ndani na nje wanaonekana wanaurafiki na wana siasa wanao taka kiti chake bila kujali ajira za wananchi masikini wanaopata ridhiki zao kwao.
 
Msemaji wa serikali amesema hatua za kisheria na kidiplomasia zimeanza kuchukuliwa kulimaliza jambo hili.

Transfer of ownership ya ndege hiyo haijafanyika. Mtu mwingine anaenda kuichukuwa kiwandani kwa kisingizio kuwa ana madai na yule anayetaka kuinunua (ambaye alishatoa deposit money kiwandani) halikubaliki kisheria. Kitu cha namna hiyo ni sawa na utekaji nyara. Ndiyo maana serikali imeanza kuchukua hatua za kisheria kwa watekaji nyara hao ambao wameshirikiana na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wakiongozwa na Tundu Lissu.

Njia za kidiplomasia zimewezesha serikali ya Canada kuwanyang'anya ndege hiyo hao watekaji tayari kuwa handed over to Tz, wakati hatua za kisheria zikiendelea dhidi ya hao watekaji.

Hivyo hao wanasiasa wetu walioshirikiana na hao watekaji wasubiri mziki unaowastaili. Wanasiasa hawa walianza na terrible twins na sasa wameteka bombardier. Mahakama ya wahujumu uchumi inawangoja kwa hamu upelelezi utakapokamilika. Walianza na uchochezi/ uchokonozi, sasa waneamua kufanyap uhujumu uchumi!!! Inawezekana hata hayo maelfu ya sare za kijeshi yaliyokutwa kwenye hizo godowns za Manji wanahusika pia.
 
Malofa wakubwa hawa (kwa sauti ya Mkapa) yaani wanajitetea kwa hoja nyepesi hizi inawezekana vipi tunadaiwa alafu wanataka kufanya kimya kimya wakati hilo deni tunalipa kwa sisi walipa kodi na hao wanasiasa anaowalalamikia akumbuke pia chanzo cha deni lenyewe na kesho watakuja na maneno ya ki-lofa kama haya wakati hawa wengine wakianza kutudai mapesa mengine kwa kua hamtaki kushauriwa.
 
Tulipeni madeni tuache longolongo aiseeee
Mpwa sio kulipa tuu bali kwa madeni ya kipuuzi kama haya yanayoletwa na mtu mmoja kwa ajili ya kujionyesha hapangiwi inabidi turudi kwenye katiba na kuiweka sawa ili anyolewe bila maji.
Hasara kama hiyo moja ya Bilioni 87 imesababisha maisha ya wenzetu wangapi kufa kwa kukosa dawa? Vifaa tiba? Au watoto na wadogo zetu wangapi wamekuwa wajinga au mateja kwa vile walistahili kusoma na wamekosa mikopo na kushindwa kusoma?
Hivi hatuwezi kuazima katiba au sheria za China kwa mwezi mmoja tuu tukashikishana adabu hasa kwa hawa viburi koko?nakumbuka China walimnyonga mjane wa Mao kama sikosei miaka ile kwa tabia chafu bila kujali jina la marehemu mumewe.
 
Cha ajabu nini ? si wanadai basi watalipwa tu sasa kelele za nini kudaiwa ni jambo la kawaida watalipwa na ndege itakuja na maisha yaendelee
 
Serikali wamekosea kukatisha mkataba wa hiyo kampuni!, lakini tukubali walitonywa na watanzania wenzetu kuhusu mali za Taifa nje ya nchi....
 
Haya ndiyo madhara ya Kuamini ubabe kuliko Akili katika Kuongoza watu.

Leadership ni Wisdom na knowledge! na wala si vitisho na Ubabe wa kijinga...

By the way: Sipendi Ubabe karika Kuongoza! Lakini Ninaipenda CCM katika Kuongoza
 
!
!
Kweli kabisa Zamaradi Kawawa, wanasiasa wanaodaiwa walipo hela za watu haraka ili ndege iweze kuachiwa. Na wana siasa hawa pia wasisahau na wale Samaki kuna fidia tunadaiwa
 
Lisu mtamuonea tu,alichofanya yeye ni kushare habari tu,
alieanza kujua kuna vitu haviko sawa kuhusu ndege ni Zito kabwe na akamwuliza mbarawa.
Itakuwa zito alimtonya lisu,


zito nae atakuwa pengine katonywa na Jack zoka,si marafiki tang zito yuko cdm?.
 
Ununuzi wa ndege ya 3 ya Bombadier umeingiliwa na mgogoro uliotengenezwa na wanasiasa na watu wasioitakia mema Tanzania.

"Wanasiasa waliotengeneza mgogoro huo wanahujumu maendeleo ya nchi na usalama wa raia"-Kaimu Mkurugenzi Mkuu-Idara ya Habari Zamaradi Kawawa

Ndege ya 3 ya Bombadier ipo na inakuja kwahiyo wananchi waiamini Serikali yao. Serikali imesikitishwa na ushiriki wa wanasiasa na baadhi ya watu kuhujumu maendeleo ya nchi.

Watanzania tuwe wazalendo kulinda,kutetea na kukabiliana na hujuma zozote zinazorudisha nyuma maendeleo ya Nchi.

Watanzania, Tuunge mkono jitihada za Rais Magufuli katika kuleta maendeleo bila kujali itikadi ya chama, kabila au dini. Kuhusiana na mgogoro wa ununuzi wa ndege hatua za Kidiplomasia na sheria zimeanza kuchukuliwa ili kumaliza jambo hili.

Unaweza kusoma mwenyewe tweets za kaimu msemaji wa serikali.



View attachment 570220
View attachment 570219

Hii nchi vyama vya upinzani vimegeuka kuwa Vikaragosi vya wasioitakia mema Tanzania. Chochote kinachokuwa kibaya dhidi serikali wao ndio wa kwanza kushangilia. Hivi kweli unaweza kuita press conference na kuanza kushangilia kuwa ndege imekamatwa kwa deni. Leo serikali inapochukua hatua ya kuwabana wawekezaji kwa upinzani ni kero, serikali inapopambana na mafisadi na madawa kulevya haohao wapinzani ndio mstari wa mbele kwenda mahakamani kuwatetea. Serikali ya awamu ya tano ina mapungufu yake lakini inapokuja National Interest tunatakiwa kuiunga mkono.
 
Na mkiagiza dream liner Barrick watakuwa wameshinda kesi.Tutaikamata na kuipiga mnada kupata malipo ya awali ya madai yetu.Baada ya hapo tutakamata mali zote za Tanzania zilizopo Canada Uingereza na Marekani. Hatutaki mzaha na ushenzi sisi
Kwani Tanzania Ina Mali nje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom