Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Ku share publically na kU damage reputation Ya serikali au nchi? Lisu kuna kitu hajui when freedom fighters wakiingia msitu watu wa kwanza kuuawa kabla ya mkoloni huwa ni puppets

Tunavyojua akina sisi ni kwamba Puppets ni wale walioliingiza Taifa kwenye mikataba mibovu ya raslimali zetu,walionunua vivuko vibovu kwa mabilioni ya shilingi,iojenga Barabara substandard na wale wote waliovunja mikataba hovyo hovyo bila kuzingatia sheria na wanaotuongizia hasara kila siku.Hawa ndiyo PUPPETS na haki hao ni kunyongwa hadi kufa
 
Zamaradi Zamaradi schoolmate wangu kweli 'wanasiasa ndio sababu???' Upinzani unawasaidia kuwapa mawazo ninyi mmewageuza kuwa maadui haya sasa mtanyooshea watu vidole vitatu kati ya tano vinawageukia ninyi. Mjipange upya hili la kwanza more to come
 
Haya ndio tumekuwa tukiyasema kila siku....Hawa wapinzani wa nchi hii wakae wakijua hawamkomoi MAGUFULI bali wanatukomoa sisi WATANZANIA
Kwa kuvunja mikataba na kuletea hasara watanzania au !!!???[emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
Yawezekana una ubongo wenye jinsia mbili kiasi cha kukufanya ushindwe kufikiri sawa sawa na kukuacha kwenye dilemma!Hivi Lissu unayeng'ang'ania kumuhusisha na kukamatwa kwa hilo pangaboi lenu ndiye aliyesababisha hilo deni?

Acheni unafiki,msiwatwishe lawama watu wasiohusika na ukurupukaji wenu.
Mkuu,hawa Watu si wa Dunia hii,maana hawaelew kinachozungumzwa na ni wagumu hatar

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpwa sio kulipa tuu bali kwa madeni ya kipuuzi kama haya yanayoletwa na mtu mmoja kwa ajili ya kujionyesha hapangiwi inabidi turudi kwenye katiba na kuiweka sawa ili anyolewe bila maji.
Hasara kama hiyo moja ya Bilioni 87 imesababisha maisha ya wenzetu wangapi kufa kwa kukosa dawa? Vifaa tiba? Au watoto na wadogo zetu wangapi wamekuwa wajinga au mateja kwa vile walistahili kusoma na wamekosa mikopo na kushindwa kusoma?
Hivi hatuwezi kuazima katiba au sheria za China kwa mwezi mmoja tuu tukashikishana adabu hasa kwa hawa viburi koko?nakumbuka China walimnyonga mjane wa Mao kama sikosei miaka ile kwa tabia chafu bila kujali jina la marehemu mumewe.
Dah inauma
 
Hii nchi vyama vya upinzani vimegeuka kuwa Vikaragosi vya wasioitakia mema Tanzania. Chochote kinachokuwa kibaya dhidi serikali wao ndio wa kwanza kushangilia. Hivi kweli unaweza kuita press conference na kuanza kushangilia kuwa ndege imekamatwa kwa deni. Leo serikali inapochukua hatua ya kuwabana wawekezaji kwa upinzani ni kero, serikali inapopambana na mafisadi na madawa kulevya haohao wapinzani ndio mstari wa mbele kwenda mahakamani kuwatetea. Serikali ya awamu ya tano ina mapungufu yake lakini inapokuja National Interest tunatakiwa kuiunga mkono.
Unadhani kama wasingeongea si ingebaki siri
 
Hao wanasiasa ndio walinyang'anya tender kinyemela?!

Hao wasioitakia mema nchi hii ndio mahakama iliyotoa huo uamuzi?

Mahakama iliyotoa huo uamuzi haitambuliki katika mkataba tuliosaini wenyewe na mkandarasi/mdeni wetu tukiwa na akili timamu?

Nani amesema mkilipa deni la watu hiyo ndege haiji?

Mbona mnataka kutufanya nchi nzima mabashite?

Alafu mbona mliukuwa mnafanya siri?!

Nyinyi mlioamu kufanya siri kwa walipa kodi na alieamua kuwaeleza ukweli walipa kodi,ni nani mzalendo?

Anaetuambia kila siku msema kweli ni mpezni wa Mungu ni nani kama sio boss wako?

Pathetic!!
Pathetic is a kind word!
 
Kwenye maamuzi makubwa kama kuvunjwa mikataba nakilaumu moja moja chama cha CCM maana likitokea tatizo bungeni mnadhimu uwaita na kufanya maamuzi ya pamoja kua wote wakubaliane kumbuka kafulila alisema kwenye escrow mawaziri wanne walimuunga mkono. Je mbona chama kinalinda maslahi ya chama kuliko maslahi ya taifa? Hii haikosawa haiwezekani madeni yanakuwa mengi kiasi hichi kwa makosa yanayozuilika.


Kamati ya uchunguzi imesema acacia hawalipi kodi na kuwaita mezani wakati hao wanaenda mahakamani sababu ya makinikia. Hapo nani mwenye nia thabiti ya kutetea maslahi mapana ya taifa?


Kuna wabunge walikua mawaziri wengine watumishi serikali ndio wametuingiza hapa tulipo kwenye matatizo halafu bado wanachama na bado wapo madarakani na wengine watumishi wakati kuna baadhi ya watu wamefukuzwa uwanachama sababu za kiuchaguzi.

Hapo ukipima kuiona nia thabiti ya kujikomboa kama taifa kuna ukakasi japo kua tunaamini Roma haikujengwa siku moja lakini ukijengea mnao zenye mchwa ndani matokeo yanajulikana
 
  • Thanks
Reactions: HRT
mkuu, kama serekali inahitaji cooperation kutoka vyama vya siasa kwa nini iwanyime uhuru wao wa kikatiba?
watu (wapinzani) wamebinywa pumzi puani, sasa inabidi waitolee kule chini...wafanyeje sasa?
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom