Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Kama haya madeni yatalipwa naona kwa hakika ile miradi yote iliyozinduliwa kwa mbwembwe kuyeyuka kama barafu
 
Yaani TL asingesema jana tusingejua bombadier yetu imekamatwa.....
Pili kudaiwa siyo dhambi mbona hapa bongo vihela vidogo km HESLB wanatufuata hadi ofisin why serikali yetu tukufu isilipe wakati ni kweli tunadaiwaa?
Hongera sana TL naona wameanza kufuata maneno yako na soon Yohana mbatizaji nae atatoka hadharani kwamba wanasiasa wamesababisha ndege kukamatwa ili hali tunadaiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchakato umeingiliwa na wanasiasa? What nonsense is this!? Yaani walitaka haya mambo yawe siri na hizo jitihada za kidiplomasia ziishie Nchi kuchomolewa bilions za kutosha kimyakimya? Nchi inaongozwa na "wapumbavu" kwelikweli.

Mwanzo wa yote haya ni mwanasiasa uchwara mmoja kujifanya yeye ndo kidume na kuingilia mikataba ya watu bila kutumia hekima, busara, sheria na taratibu. Anapaswa akumbushwe haya mambo na sio kuhamisha goal posts.
 
Ni kweli mwana siasa namba moja nchi hii ndiye aliyetengeneza huu mgogoro, na anapaswa kukemewa kwa kuliingizia Taifa hasara kwa kukurupuka na kuvunja mkataba bila kufata sheria.
 
Hivi deni la samaki wa Magufuli limeisha tusijeagiza mv bagamoyo mpya hela ikabebwa tena
Samaki Hawajalipwa na Bila kusahau ATC ilibidi hizi ndege ziandikishwe kama Mali ya serikali ili kukwepa deni la ATC .kumbe nitumeruka jivu tukakanyaga moto
 
Nyie watanzania yani baba yako akinyanganywa shamba ama nyumba kisa anadaiwa watoto mtafurahia. Kizazi cha nyoka hiki-wicked society.

Je hamjui ya kwamba hizo pesa mtazilipa ninyi wana nchi kwa kupitia kodi zaidi? Je hamjui ninyi ndo mtaathirika zaidi na mfumko wa bei kwasababu dola zaenda nje? Mnafikiri serikali ama waziri ama rais ataathirika kwa lolote? Watu hawa wanaangamia kwa kukosa maarifa, iliwapasa kuhuzunika na kusikitika.
Hii yote inatokana kuwa na viongozi wakurupukaji, wasiopenda kufuata taratibu.
 
Kama ndege imekamatwa kisheria na wadeni wetu ni sharti tuwalipe.

Kama kuna uingiliaji wa wanasiasa hayo c hatujui, serikali ihakikishe mali ya Tz inafika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchakato umeingiliwa na wanasiasa? What nonsense is this!? Yaani walitaka haya mambo yawe siri na hizo jitihada za kidiplomasia ziishie Nchi kuchomolewa bilions za kutosha kimyakimya? Nchi inaongozwa na "wapumbavu" kwelikweli.

Mwanzo wa yote haya ni mwanasiasa uchwara mmoja kujifanya yeye ndo kidume na kuingilia mikataba ya watu bila kutumia hekima, busara, sheria na taratibu. Anapaswa akumbushwe haya mambo na sio kuhamisha goal posts.
Umesahau kumalizia :Siyo la Kifamilia 'Any decision you make in life you are responsible for it'
 
Back
Top Bottom