Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Maadui zetu wanashangilia wakiona nyuzi kama hizi.

Hakuna kitu kizuri kama kuona adui zako wakifikiria KUPOTEZANA WENYEWE KWA WENYEWE..!

Pathetic..!
 
Ndege ya 3 ya serikali ipo na inakuja kwahiyo wananchi waiamini serikali yao- Kaimu Mkurugenzi Mkuu-Idara ya Habari, Zamaradi Kawa
hatukatai, hata Lissu kasema... lakini kuna bei ya ziada tumeilipa.
tatizo ni....hizi ni pesa za kodi zetu kwa nini wazichezee?
 
Wewe umejisajili this August kuja kutisha watu hapa? Post zako nyingi unajionyesha una mamlaka ya kuwanyima watu uhuru wao wa mawazo kinyume na JF regulations. Kaa chonjo utakula ban ya maisha, hapa sio mahali pa watu wa aina yako.
Mkuu achana naye mpuuzi huyu kwanza ni mtu wa fitna huko rungwe kaanzisha figisu la kumng'oa DC kwa njaa zake
 
Mchakato umeingiliwa Na lissu Na umeingiliwa kisiasa. Lissu Na baadhi ya watu wa mataifa wasioipendea mema Tanzania,
Na mtatiro kaa chonjo habari tunazo
Hebu nijuzeni lissu kaingiliaje,
Hivi yy kusema imezuiliwa ndo kuingilia?,
Kwani lissu ndo aliwawakilisha na kuwasaidia kwenda mahakamani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na mkiagiza dream liner Barrick watakuwa wameshinda kesi.Tutaikamata na kuipiga mnada kupata malipo ya awali ya madai yetu.Baada ya hapo tutakamata mali zote za Tanzania zilizopo Canada Uingereza na Marekani. Hatutaki mzaha na ushenzi sisi
Nimefurahi sana,hata ndege ya rais ikienda huko waikamate
ujinga ni tatizo..barrick watakugawieni!!?..au kwenu ndiyo pataporudi nyuma kimaendeleo
 
Aache upuuzi huyu! Atuwekee huo ushahidi ea hao wahujumu na kama uko ushahidi wakamatwe siyo kutaka kutengeneza zengwe la kuwabambikia kesi uchwara.

Ununuzi wa ndege ya 3 ya Bombadier umeingiliwa na mgogoro uliotengenezwa na wanasiasa na watu wasioitakia mema Tanzania.

"Wanasiasa waliotengeneza mgogoro huo wanahujumu maendeleo ya nchi na usalama wa raia"-Kaimu Mkurugenzi Mkuu-Idara ya Habari Zamaradi Kawawa

Ndege ya 3 ya Bombadier ipo na inakuja kwahiyo wananchi waiamini Serikali yao. Serikali imesikitishwa na ushiriki wa wanasiasa na baadhi ya watu kuhujumu maendeleo ya nchi.

Watanzania tuwe wazalendo kulinda,kutetea na kukabiliana na hujuma zozote zinazorudisha nyuma maendeleo ya Nchi.

Watanzania, Tuunge mkono jitihada za Rais Magufuli katika kuleta maendeleo bila kujali itikadi ya chama, kabila au dini. Kuhusiana na mgogoro wa ununuzi wa ndege hatua za Kidiplomasia na sheria zimeanza kuchukuliwa ili kumaliza jambo hili.

Unaweza kusoma mwenyewe tweets za kaimu msemaji wa serikali.



View attachment 570220
View attachment 570219
 
Wakuu How do you feel unapoiona Bendera yenye Rangi Nzuri ikishindwa kwa Kuhujumiwa.unafaidika nini Tanzania Ikishindwa?

View attachment 570234



Huwa sishangai Vitendo kama Hivi Ndo Husababisha Mi6, Israel Mosads, CIA, kupoteza Watu.
Hii bendera nzuri sana Ila shida nchi imechafuliwa na TAKATAKA za Lumumba ndo maana watu wengi tunakua na mashaka na Uzalendo.
 
Mbona awakusema mpk Camanda LISU kasema. Ndio mapovu sasa??
 
Hivi ninyi watu wenye mtazamo wa kuhimiza uzalendo na umoja wa kitaifa kwa nini mko biased

1. Mnaona sawa pale utawala unaposhindwa kufanya vizuri kutuhadaa watanzania kwa wito wa uzalendo.

2. Pale upande wa pili unaposhindwa kufanya vizuri mnauchukulia hatua kali haya yote tunayashuhudia. Huo uzalendo haushuhudiwi ukifuatwa

Mimi nadhani roho hii ya visasi mnayoitengeneza (utawala) kwa kuwanyanyasa wengine kisa upinzani mmeipanda na kuimwagilia maji kama hamtoing'oa kwa kutenda haki mtakivuna hicho roho zenu zinachokipanda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali iliambiwa mapema kwanini ilipe cash?? Mkajidai mna pesa. Maana kama mlijua mna madai na kampuni ya Canada hamnge lipa cash. Upeo wenu mdogo na kuogopa kumshauri bwana mtukufu ndiko kunatugharimu. Kweli wana siasa walioko ndani ya chama tawala ndio wametufikisha hapa. Maana mnge mshauri mtukufu haya hayange tokea.
Mbona mlikaa kimya hadi libume ndio muite press. Hizi ni aibu za serikali ya awamu hii.
Kwani ni wanasiasa gani walio inyanganya kandarasi hiyo kampuni ya Canada kama sio Ccm. Bado mambo yataharibika kwa sababu ya ubabe wenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom