Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

[emoji120] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106]
 
Jana nilimsikia wakili na mbunge Tundu Lissu akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kusema ana taarifa kutoka kwenye vyanzo vyake serikali vilivyomwambia kuwa ndege ya serikali aina ya Bombadier imekamatwa na kutishia kupigwa mnada!.

Kauli ya Lissu iliibua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii,katika pita pita zangu mtandani nikakuta "Conversation" kati ya Zitto Kabwe na Waziri mwenye dhamana Prof Mbarawa,kwenye maelezo yake Prof alisema si kweli kuwa ndege imekamatwa na hakuna mgogoro bali kuna mambo madogo madogo yanakamilishwa kati ya serikali ya kampuni ndiyo maana ndege imechelewa na kuja na itakuja siku si nyingi.

Asubuhi ya leo,idara ya maelezo ambayo ndiyo mdomo wa serikali imezungumza na waandishi wa habari kupitia naibu Mkurugenzi wake mkuu Zamaradi Kawawa na kujibu kuwa ni kweli kuna kesi ya msingi iliyosababisha ndege hiyo kuzuiwa huku akiwatuhumu baadhi ya wanasiasa kuwa wapo nyuma ya kesi hiyo.

Zamaradi amedai kesi hiyo imesababishwa na baadhi ya wanasiasa ila ameshindwa kuwataja majina na kusema tayari serikali imechukua hatua za kisheria na kidiplomasia kumaliza kesi hiyo!.

My take.

Serikali ilikuwa inamsubiri Lissu aseme ndiyo nayo ijitokeze kumjibu?Rais aliahidi ndege kuwa ingewasili mwezi July mwaka huu,mwezi umekwisha ndege haijaja.

Kulikuwa na ugumu gani kwa serikali kulisemea hili mapema kuliko kumsubiri Lissu aiseme ndiyo ijitokeze kujibu,Je Lissu angekaa kimya serikali nayo ingekaa kimya?

Matokeo yake,majibu ya wizara husika kutoka kwa waziri husika na yale ya idara ya habari maelezo yanatofautiana,wananchi washike lipi?

Serikali imetoa maelezo ya kulaumu zaidi bila kuuambia umma,hiyo kesi inahusu nini? na kama kweli kuna wanasiasa wapo nyuma ya kesi hiyo,kuna ugumu gani kuwataja?

Siku zote ukweli utakuweka huru.
 
At mtu anadai wanasiasa wameizuia ndege ya mapangaboi kuja nchini!!....Huu ni uchochezi wa kuhatarisha amani na usalama wa raia na ni dhana za kizandiki wa umakanikia ya ubongo. Alistahili kuchukukiwa na kuhojiwa bila dhamana na wote wsjuao tuhuma za wachochezi bila mishiko ya kisheria tanziania.
 
Mchakato umeingiliwa Na lissu Na umeingiliwa kisiasa. Lissu Na baadhi ya watu wa mataifa wasioipendea mema Tanzania,
Na mtatiro kaa chonjo habari tunazo
Hahahahaa!! Lisu jana ameliamusha DUDE!! Leo wameibuka japo walikuwa hawataki siri ifichuke!! Yaaani waliona mbali sana kwa kupiga marufuku mikutano ya hadhara haki ya mungu sasa ingekuwa balaa!!! Kama kupitia mitandao ya jamii tu jamaa anawachemusha hivi ingekuwa ni juu ya jukwaa ingekuwaje?!! SHIKAMOO LISU
 
Haya ni maswali ambayo hata Mwenyezi Mungu mtoa haki amefurahia ulipoyauliza! Kama kweli tunapenda ukweli, Serikali ilipaswa kuwa wazi hata kwa hili!
Ubarikiwe!
 
Kwa sababu hizi tunakuwa tunaclear doubt kwamba kuna viongozi hawana vyeti na PhD ya huyu msukuma ina walakini!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Za mwizi 40
Watanzania HUKO NJE endeleeni kushabikia kila la YULE MZEE

Siku hazigandi.....

Chief Economist
 
Ifikie hatua serikali ifanye uamuzi mgumu dhidi ya hawa watu
hatuwezi kuhujumiwa na watanzania wenzetu kisha kuwachekelea
 
Wanazidi kupoteana huu mwaka wa pili, ngoja tuone mpk mwaka wa tatu itakuaje [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Psalm 133:1[emoji768] "Behold, how good and how pleasant it is for brethren to dwell together in unity."
 
Wewe umejisajili this August kuja kutisha watu hapa? Post zako nyingi unajionyesha una mamlaka ya kuwanyima watu uhuru wao wa mawazo kinyume na JF regulations. Kaa chonjo utakula ban ya maisha, hapa sio mahali pa watu wa aina yako.

Na Ni naona ana marafiki ni mods huyu maana jinai wanavyomlea kama kichanga na mama yake.Kila wakati ni kutishia watu maisha hao,sijui nani alimweleza yeye ataishi milele
 
MIMI NIMEMUELEWA HIVI ZAMARADI KAWAWA

a) Kwanza amekubali Madai ya Tundu lissu

Ununuzi wa ndege ya 3 ya Bombadier umeingiliwa na mgogoro uliotengenezwa na wanasiasa na watu wasioitakia mema Tanzania"-Zamaradi Kawawa

Nilivoelewa mimi ni kwamba ni kweli huu mgogoro ulitengenezwa na mwanasiasa (Wa CCM)ambae kipindi hicho alikuwa waziri akavunja mkataba na kufanya hivo ni kweli alikuwa haitakii mema Tanzania.

b) Watanzania tuwe wazalendo kama Tundu lissu

"Watanzania tuwe wazalendo kulinda,kutetea na kukabiliana na hujuma zozote zinazorudisha nyuma maendeleo ya Nchi"-Zamaradi Kawawa

Tusikubali kirahisi matendo haya ya wanasiasa kam hawa waliotuingiza kwenye migogoro kama hii ya kulipa pesa zetu bila sababu yeyote maana hizi pesa zingefanya kazi nyingine matokeo yake tuwawapa watu bure tu,tusisite kiwakosoa.

Kiufupi ametufanya tuyaamini aliyosema Lissu
 
SIO YEYE ALIYEZAMISHA ILE MELI NI WAHUJUMU TU. WALIIACHA IKIZAMA POLEPOLE BADALA HATA YA KUIVUTA NACKUIWEKA MAHALI SALAMA NACKUREKEBISHA TATIZO LILIOKUWEPO. kama tungefanikiwa KUITAIFISHA SI INGEKUWA MSAADA KUITUMIA HATA KWA AJILI YA MAFUNZO YA UVUVI BAHARI KUU? SASA HASARA MARA MBILI. KWANI SIO KWELI KUWA ILISHIKWA IKIVUA NDANI YA BAHARI YETUU BILA KIBALI?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…