Msemo gani unatumia kujifariji baada ya kumaliza pesa kwa matumizi ya kijinga au starehe?

bhana ee!, pesa hazijai
Ilikuwa around 2014 pale Escape One, nilitumia kizembe sana 300k na kama sio msela wangu mmoja nilikuwa niamke kapuku kesho yake.
 
Maisha ndio hayahaya..
Huko jikoni nitengenezeeni kuku sekela mzima na chips mtumio alfu na pilipili km ya siku zote..
 
Nile PESA kaburini,.
Hela yenyewe huwezi kununua Ferrari,
kujenga huwezi,hata chochote hauwezi.
Sasa ushindwe hata kunywa bia tena au kiroba,hata gongo unatwanga tu.
Mi hadi vilabuni ukinikuta utashangaa.
Napiga pombe za kienyeji ka sina akili nzuri.
Kesho bar za kueleweka
nshabadilika pedeshee tayari.
Kesho utanikuta Masaki Karambezi ndo utachoka
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Dr Remmy aliimba rafiki yangu yule tukipiga story miaka hiyo akila mchicha wake.
Kilio
" kama wote tukiwa madereva
Nani atakua abiria"
"Wote tukijenga,nani atakua mpangaji?
Wote tununue viatu vipya,fundi viatu afanye kazi gani?
 
Ilikua 2022 nilipata mchongo wa 800k afu nlikua nna jambo langu LA maana nifanye,

Shost akanipelekaa Mikocheni kuna duka LA viwalo, aseeh nlinunua nguo ambazo hata sikuwaza, kuja kutazama imebaki 260k

Hatariii tupuu.
Ikawa full kuvurugwa, alafu kanakuja kale ka msemo ka faraja, kama nilipata hizi ntapata zingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…