Mshabiki mwezangu wa soka, unamzungumziaje Clotous Chota Chama?

Mshabiki mwezangu wa soka, unamzungumziaje Clotous Chota Chama?

Habari za wakati huu, hivi ni nani aliyemuona huyu mchezaji maana anatuaminisha sana sisi ambao hatujawahi kucheza soka kuuona huu mchezo ni mrahisi sana, kuna haja sasa ya TFF kumtambua Chama kama mchezaji bora wa karne hii ya 21 na kama itawapendeza serikali ya awamu ya tano impatie uraia wa Tanzania huyu kijana.
 

Attachments

  • 7666eea479f74c56b14b99e5c624e8ea.jpg
    7666eea479f74c56b14b99e5c624e8ea.jpg
    53.3 KB · Views: 2
Habari za wakati huu, hivi ni nani aliyemuona huyu mchezaji maana anatuaminisha sana sisi ambao atujawahi kucheza soka kuuona huu mchezo ni mrahisi sana, kuna haja sasa ya TFF kumtambua Chama kama mchezaji bora wa karne hii ya 21 na kama itawapendeza serikali ya awamu ya tano impatie uraia wa Tanzania huyu kijana.
Apewe uraia tu kwa utashi wako , haya ndiyo matatizo kujitekenya umeanza na kutoa ushuzi .
 
Hawa jamaaa hawana maneno, lakini wanajua sana, kama uraia basi wapewe tu.
Tanzania nchi kubwa sana.
 
Tanzania sio Marekani. Uraia wake hautamanishi. Huyu jamaa zile pasi zake mpenyezo sio poa. Pass laini,sio cross dongo
 
Bado namtafakari fundi Chama..... kuna kitu kinakuja juu yake mtaelewa .

Kwa ufupi tu , ukitaka kumjua kiungo mchezeshaji mwenye majukumu ya kutunza mfumo wa kushambulia wa timu , kupanga mashambulizi , kiungo mwenye uwezo wa ku ‘ unlock defensive plan’ ya adui , kiungo mwenye uwezo wa kuwafanya wenzake wakazitendea haki nafasi zao kwa zaidi ya asilimia 50 , kiungo mwenye jicho la kujua wakati gani timu ishambulie kwa mipira mirefu na wakati gani icheze direct play kwa maana ya kujenga shambulizi kutoka box moja kwenda jingine basi huna budi kumtazama raia huyu wa Zambia Cleutus Chama anayeichezea Simba SC .

Kwanza kabisa ana nguvu , kasi , uwezo wa kukaa na mpira na kuupeleka anapoona ni sawa kufika lakini agility yake inamfanya ku ‘impact ‘ offensive spirit kwa forwad line ambayo inaifanya forwad line ya Simba muda mwingi kuwa deep kwenye final third ya opponent.

Aussems alimsoma Chama akaona anahitaji kiungo mwenye uwezo kama wake kwenye kukaa na mpira , kupiga pasi na kuwavuruga wapinzani katika kwa jinsi anavyocheza na mpira ndipo akatengeneza pacha ya Ndemla na Chama juu ikinakshiwa na Emanuel Okwi
Asante Mwalimu Kashasha.
Chama akiwa na mpira, anacheza kama hataki lakini kila anachofanya ni sahihi.
Angalia Mchango wake kwenye goli la Kwanza na la pili.
Ngoja niangalie marudio kwenye U tube
 
Chama anajua halafu ana nidham itamsaidia kua na miasha pale msimbazi.
 
Alitupiamo ngapi jana maana mi nilivosikia shangwe kitaaa nikaenda kulala
 
Namtazama hapa luningani, huyu jamaa alipaswa awe anacheza walau ligi kuu ya Afrika Kusini (PSL). Ana uwezo mkubwa sana hasa anapocheza kama Kiungo Mshambuliaji (Inside 10). Hapa kwenye ligi ya bongo anapoteza muda na kipaji chake.
Mshabiki mwezangu wa soka, unamzungumziaje Chama?
Shida yake ni uchoyo
 
Back
Top Bottom