Bado namtafakari fundi Chama..... kuna kitu kinakuja juu yake mtaelewa .
Kwa ufupi tu , ukitaka kumjua kiungo mchezeshaji mwenye majukumu ya kutunza mfumo wa kushambulia wa timu , kupanga mashambulizi , kiungo mwenye uwezo wa ku ‘ unlock defensive plan’ ya adui , kiungo mwenye uwezo wa kuwafanya wenzake wakazitendea haki nafasi zao kwa zaidi ya asilimia 50 , kiungo mwenye jicho la kujua wakati gani timu ishambulie kwa mipira mirefu na wakati gani icheze direct play kwa maana ya kujenga shambulizi kutoka box moja kwenda jingine basi huna budi kumtazama raia huyu wa Zambia Cleutus Chama anayeichezea Simba SC .
Kwanza kabisa ana nguvu , kasi , uwezo wa kukaa na mpira na kuupeleka anapoona ni sawa kufika lakini agility yake inamfanya ku ‘impact ‘ offensive spirit kwa forwad line ambayo inaifanya forwad line ya Simba muda mwingi kuwa deep kwenye final third ya opponent.
Aussems alimsoma Chama akaona anahitaji kiungo mwenye uwezo kama wake kwenye kukaa na mpira , kupiga pasi na kuwavuruga wapinzani katika kwa jinsi anavyocheza na mpira ndipo akatengeneza pacha ya Ndemla na Chama juu ikinakshiwa na Emanuel Okwi