Mshabiki mwezangu wa soka, unamzungumziaje Clotous Chota Chama?

Hahaha.. Mkuu nachoweza kusema, huyu Chama kashindikana. Na jambo la msingi tuendeleze tu dua, ili Allah azidi kuwatia 'upofu' maskauti wa Barcelona waendelee kutomuona.
Sahii mkuu hii namba inatoka ulimwengu mwingin kabisa
 
Bado namtafakari fundi Chama..... kuna kitu kinakuja juu yake mtaelewa .

Kwa ufupi tu , ukitaka kumjua kiungo mchezeshaji mwenye majukumu ya kutunza mfumo wa kushambulia wa timu , kupanga mashambulizi , kiungo mwenye uwezo wa ku ‘ unlock defensive plan’ ya adui , kiungo mwenye uwezo wa kuwafanya wenzake wakazitendea haki nafasi zao kwa zaidi ya asilimia 50 , kiungo mwenye jicho la kujua wakati gani timu ishambulie kwa mipira mirefu na wakati gani icheze direct play kwa maana ya kujenga shambulizi kutoka box moja kwenda jingine basi huna budi kumtazama raia huyu wa Zambia Cleutus Chama anayeichezea Simba SC .

Kwanza kabisa ana nguvu , kasi , uwezo wa kukaa na mpira na kuupeleka anapoona ni sawa kufika lakini agility yake inamfanya ku ‘impact ‘ offensive spirit kwa forwad line ambayo inaifanya forwad line ya Simba muda mwingi kuwa deep kwenye final third ya opponent.

Aussems alimsoma Chama akaona anahitaji kiungo mwenye uwezo kama wake kwenye kukaa na mpira , kupiga pasi na kuwavuruga wapinzani katika kwa jinsi anavyocheza na mpira ndipo akatengeneza pacha ya Ndemla na Chama juu ikinakshiwa na Emanuel Okwi
 
"Cla Cho Cha" wenyewe humuita Triple C. Ni miongoni mwa wachezaji ambao unaweza kuwatizama huku ukitupatupa popcorn mdomoni au kijikombe cha Kahawa.

Anakupa maana kamili ya kiungo chakushambulia. Anakupa anautaka, anakupa tena anaufuata, akiwa nao anaamua kukaa nao au kutafuta mwenye nafasi, na kunawakati anaingia nao chumbani na kutokea nao sebleni. Chama ni ukwaju sana.

Nawaza tu siku wanacheza Haruna na Cla Cho Cha pale kiungoni....... Sijui patakuwaje pale kiungoni na kwa wale wa juu kule shambulioni.
 
ki ukweli bila kupepesa Chama ni bonge la kiungo na utatamani kila saa mpira uwe miguuni mwake. Huyu Chama angekuwa na nguvu kidogo kama Salamba nina hakika timu zingekuwa zina kula kumi na kendelea. Ukitaka kujua kuwa Simba sasa inahitaji mshambuliaji mmaliziaji tu kwa sasa angalia pasi za mwisho za Chama na Dilunga. Yaani pasi zao za mwisho mtu unasukumiza tu ndani lakini akina Okwi, Kagere na Boko wanafunga goli tatu kati ya pasi kumi. Chama ananikumbusha mtaalamu mmoja alewahi kutokea miaka ya nyuma akiitwa Hamis Gaga "Gagarino".
 
Utakuwa mwl. Kashasha
 
Chama, saws unadhani hao wa south hawamuoni? Usikute hana wanachokitaka.
 

Sasa hivi tunamuuza Liverpool FC au FC Barcelona au PSG japo hata Klabu iliyopo Mbinguni kwa Mwenyezi Mungu nayo inamtaka leo kesho imsajili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…