Mshabiki mwezangu wa soka, unamzungumziaje Clotous Chota Chama?

Nafkiri Hawa vyura wameamua kuunga hoja kwamba jamaa anajua mpira ,anakitu cha ziada ambacho kina mfanya afanye majukumu zaidi ya moja uwanjani

Ndomana siku hizi kichuya anaanza kupotea mdogomdogo kwenye mfumo hachezi DK 90
 
Yule beki munchester sijui anaitwa jonas , anacheza ulaya kwa sababu ni nyumbani
 
Chama anawalazimisha hata washambiliaji wawe na njaa ya magoli.
Kwanza kwa kuwapa pasi maridadi kabisa za mwisho, na pili yeye anafunga magoli wakati sio mshambuliaji.
Sina hakika kama msimu ujao huyu jamaa tutakuwa nae, nafikiri uongozi wa Simba umuite ukae nae uongeze nae mkataba lakini uweke kipengele cha kumuuza endapo itapatikana klabu itakayomuhitaji,hii itaisaidia simba kutengeneza hela kupitia yeye.
 
Wale mbwa wa polisi pale taifa huwa wanatulia kabisa huku wakimwangalia chama anacheza mpira
Huyu jamaa ni burudani kwa wote, walioko uwanjani na wanaotizama runingani, na shauri wagonjwa wenye maumivu makali siku simba inacheza wapelekwe uwanjani, jamaa anauwezo mkubwa wa kuwapunguzia maumivu yao kila wamtizamapo awapo na mpira.
 
Chama ameongezeka uwezo wake baada ya kukutana na kocha bora wa mazoezi na mafunzo ya uwanjani na kuridhishwa na kipato anachokipenda.
Natumaini kiwango chake kitazidi kuongezeka kadri anavyofurahia maisha bora katika timu yake ya Simba sc.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…