Mshahara umetoka, nyongeza ipo lakini lazima ucheke tu

Mshahara umetoka, nyongeza ipo lakini lazima ucheke tu

Kuna jamaa yangu kaongezewa elfu ishirini kwenye mshahara wake (20,000/=), halafu jumla ongezeko kwenye makato yake ni shilingi 7,900/=, kwa hiyo ongezeko la pesa kwenye take home ni sh 12,100/=. Hiyo ndiyo wanasema unapewa kitu kwenye mkono wa kulia halafu unanyang'anywa kwenye mkono wa kushoto!!

Sasa huyu hawezi kusema nimeongezewa sh 20,000/=, bali atasema nimeongezewa sh 12,100/= ambayo haitoshi kulipia hata kodi ya nyumba ya nusu mwezi!! USHAURI: Ongezeko la mishahara liwe linalenga kumwongezea mtu kwenye TAKE HOME CASH!!
Kuna Siku nilisema Watumishi walio wengi Uelewa Wao mdogo ktk Masuala ya KODI wengi waliamini hiyo nyongeza ni kubwa na haitakatwa Kodi Matokeo yake ni Vilio kila idara
 
Mimi naona ikiongezwa elf20 kila mwaka siombaya...ila kwa utalatibu wa kuongeza kwa miaka 6 elf20,hii sio nzuri..
 
Sasa hujui matatizo ndiyo MTAJI wa wanasiasa? Wakiyatatua leo yakaisha, kesho watakula mawe?

In short, lazima wayapalilie matatizo mengine ile kesho maisha yao yaendelee.

^Acheni viongozi waishi vizuri!^~ in someone's personal voice.
 
Mkuu kwanini usiache kazi waajiriwe watakaorizika na Mshahara wako ?
Wewe unabwaja tu.kil aliyekua ana ndot za kuajiriwa akipata hio ajira anakuja kujua kunbe mshahar hautosh kukidh mahitaj mengine.unaongea ongea tu hapo kwa shemej yako na remote umeshika.
Kuongeza ongezeko lipo na litaendelea tu.na umekaa kubeza wenzio kuona wasiseme
 
Back
Top Bottom