Mshahara wa 2,116,000 kwa Kikokotoo kipya atalipwa shilingi ngapi akistaafu?

Naomba kwa wenye utalamu wa kujua kwa mtumishi mwenye mshahara 2,116,000. Na kafanya kazi kwa miaka 32.
Kwa kikokotoo hiki kipya
1 atalipwa keshi tshs ngapi?
2 pesa ya kila mwezi atakuwa anachukua kiasi gani
Naomba kwa anaejua anisaidie
Sawa Acp wanakuja kukujuza
 
Yule kijana ukizisoma shombo zake humu jukwaani, unaweza kufikiri walimu wote ni choka mbaya! Kumbe ukija mtaani, mambo ni tofauti kabisa. 😁
🤣🤣 na mm nilikua nawaza hvo hvo maana unakuta mwalimu analazimisha sh 200 ya masomo ya jion yaan inamtoa roho kabsa
 
Kwahiyo ww ulikuwa unasubiri ustaafu ndo ujenge!!
 
Labda kwenye Mashirika na Taasisi za serikali LAKINI kama ni kwenye Wizara za serikali HAKUNA hicho kitu. Halafu kwa taarifa yenu ngazi za mishahara za TGS ni ndogo kidogo kuliko TGST za Walimu kwenye ngazi husika.
Kwani mashirika siyo serikalini?? Kote huko ni watumishi wa umma!
 
Hii ni jumla ya mishahara ya miaka 3 ya mwisho unagawa kwa 3 unapata wastani wa mshahara bora wa mwaka, kama nimekuelewa.

Kwa hiyo ni rahisi kwa mtoa mada kukokotoa jumla ya mishahara yake ya mwisho ya miaka 3 na kugawa kwa 3 ili apate hiyo APE, na kuhusu 'N' ni idadi ya miezi aliyochangia.......kazi imebaki kwake.

Kongole kwa kusaidia na wengine, maana kila mmoja ni mstaafu mtarajiwa.​
 
Kimsingi mfuko uwa unaangalia ile mishahara mikubwa zaidi ya miezi 36 (miaka mitatu) ambayo mwanachama alipokea ndani ya miaka kumi ya mwisho wa utumishi wake kabla hajastaafu. Hiyo mishahara mikubwa zaidi ya miezi 36 ndiyo ujumlishwa kwa pamoja na kisha kugawia tatu (yaani miaka mitatu) ili kupata wastani wa kipato hicho kwa mwaka mmoja mzima. Hiyo ndiyo APE kwenye formula Iliyotolewa na mdau kwenye comments za awali. Pia mfuko uangalia idadi ya miezi mwanachama aliyochangia kwenye mfuko (ambayo kwenye formula ndiyo N). Hivi vitu viwili ndivyo ubadilika kwenye formula kutegemea mwanachama na mwanachama wakati vingine havibadiliki.
Hivyo formula ya kupata kiasi cha mkupuo kusomeka kama ifuatavyo:
Commutted Pension Gratuity= (1/580) x N x APE x 12.5 x 33%.

Au kama hautaki kuangaika na mahesabu marefu tumia formula hii kupata pesa ya mkupuo:
0.007112 x N x APE.

Na formula ya kupata pension ya kila mwezi formula ni hii hapa chini:
(1/580) x N x APE x 1/12 x 67% au kwa kifupi chukua 0.0000963 × N x APE.

Kwa kutumia mshahara wa 2,116,000 na idadi ya miaka 32 (miezi 384) aliyotoa mleta mada hesabu inakuwa hivi:
Mkupuo: (1/580) x 384 x [(2,116,000 x 12 x 3)/3] x 12.5 x 0.33= TZS 69,346,427.60.
 
Kama hutojali naomba formula za mafao.
Yaani formula ya mkupuo na ile ya pensheni ya kila Mwezi.

Mfanyie tuu jamani...
 
Asante kwa ufafanuzi mzuri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…