Mshahara wa Dkt. Ndugulile akishaanza kazi WHO ni noma. Rais wa India akasome

Hii pesa anavuta azizi pale jangwani na ni ndogo
 
Kumbuka huyo wa India ni mkuu wa serikali...ni mwanasiasa mwenye maamuzi..... hao watu hata wasipokua na mshahara huona sawa tu maaana at their capacity wanaweza tengeneza dola 1M in a minute.
 
Hmm….wapo Watanzania wengi wanaolipwa zaidi ya $130,000K kwa mwaka?

Wako wapi hao Watanzania?
1. Viongozi wa juu wa kampuni ya ORICA.
2. Viongozi wa juu wa Barrick.
3. Viongozi wa juu Geita Gold.
4. CEO's na COO's wa NGO's
Hapo ni kwauchache sana...
 
Shangaa India ambaye ni Giant kiuchumi mkuu wake wa nchi ameachwa mbali sana mara mbili na ushee ila niamini mimi Hiyo pesa bado ndogo sana kwa mzigo anauchukua mama ushungi.
Bi usungi akila kona moja tu ana mabilioni yakununua piki piki za chawa wake kila kata kwa nchi nziam!!
 
1. Viongozi wa juu wa kampuni ya ORICA.
2. Viongozi wa juu wa Barrick.
3. Viongozi wa juu Geita Gold.
4. CEO's na COO's wa NGO's
Hapo ni kwauchache sana...
Kati ya Watanzania zaidi ya milioni 60, hao “wengi” wanaolipwa hiyo mishahara mikubwa ni wangapi?
 
Hata kwa nje, si hela ndogo hiyo.

Wastani wa kipato cha Wamarekani hakifiki hata $100,000.00 kwa mwaka.

Mshahara wa $11,000.00 kwa mwezi si mdogo, ingawa si mkubwa kivile.
Waungwana wamesema ni ndogo mkuu.
 
Mshahara mdogo sana huo angalia mfano mkurugenzi mkuu wa kampuni ya mafuta ya Total duniani kwa mwaka analipwa dola milioni 8.02 sawa na shilingi bilioni 16 za kitanzania kwa mwaka ukipiga hesabu kwa mwezi mshahara wake kwa mwezi ni kama shilingi bilioni moja na nusu za kitanzania hiyo ilikuwa 2022

Hiyo hela milioni 30 kwa mwezi ya Ndugulile ndogo sana kwa kazi ya kimataifa

Chairman and CEO of TotalEnergies, Patrick Pouyanné, saw his compensation increase from $6.50 million in 2021 to $8.02 million in 2022, according to a financial document. The board of TotalEnergies has indicated that it will propose a 10% increase in the remuneration of its CEO this year.
 
Kitu ikishaitwa mshahara, haikutoi maishani. Hiyo pesa ya siku moja huku migodini.
 
Feisal Salum pale Azam analipwa Zaid ya hiyo.
Unaongelea top 1 percent mkuu. Majority of Tanzanians wanakufa hawajawahi kugusa Milioni 15 kwa mkupuo, hela ambayo Ndugulile anaingiza in two weeks
 
Mbona hizo ndogo sana, kuna wengine wanalipwa 1.7 Million GBP kwa cheo kama chake kwa mwaka na wako kimya tu humu...Hongera kwake lakini kwa kuwakilisha nchi na wananchi vyema.

View attachment 3086642
Hiyo ni top one percent. Majority of Tannzanians they would kill to be paid robo ya ambacho Ndugulile anaingiza kwa mwezi
 
Anazidiwa hadi na WafanyaBiashara wa kkoo ambao hawajasoma hata. Watu kwa mwezi Faida wanaingiza hadi 50m
But still hiyo haiondoi ukweli kuwa Milioni 360 bado ni nyingi KIBONGO BONGO

Plus we unazungumzia top one percent, majority of Tanzanians they dont earn that much
 
Tanzania hii hii? Hyo si kama kiinua mgongo cha mwalimu 🤣
 
Milioni 360 kwa mwaka ni hela ndogo mkuu? Watanzania wangapi unaowajua wanaingiza hiyo hela?
Kwa cheo chake na majukumu yote hiyo hela ni ndogo mno sawa na mwalimu wa sekondar anayelipwa laki 5
 
Watanganyika mnapenda ubishi wa Simba na yanga kila jambo. Hiyo pesa siyo ndogo, sh millions 39 hivi kwa,nwezi unaita ndogo? Katika wizara kuanzia waziri hadi chini hakuna anayelipwa huo mshahara hata yeye alipokuwa waziri hakuwahi kulipwa hivyo
 
Watanganyika mnapenda ubishi wa Simba na yanga kila jambo. Hiyo pesa siyo ndogo, sh millions 39 hivi kwa,nwezi unaita ndogo? Katika wizara kuanzia waziri hadi chini hakuna anayelipwa huo mshahara hata yeye alipokuwa waziri hakuwahi kulipwa hivyo
Wanamasiala hawa.

Huo mshahara unatatua matatizo yangu yote nilioamka nayo leo 🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…