Mshituko: Rafiki yangu tuliyeshibana unamuoaje Dada yangu?

Ulitaka aolewe na mtu usiyemjuwa au ulitaka umuoe wewe?
 
Wivu kutoka kwa kaka/upande wa mke inaitwa FITNA BIN MANYUNYU hii haina nguvu sana.

FITNA BIN MANYATI hii inatoka upande wa mke hii ni mbaya sana inavunja mpaka ndoa.

Wewe acha wivu mkuu, muache jamaa amuoe dada na wewe upate ankari wa kukuomba ela ya pipi.
 
Nakubaliana nawe kaka.
 
Kwani una undugu wa damu na huyo bwana? Mshukuru Mungu kuwa dada yako anaolewa na mtu mwenye mwelekeo. Kuna wengine dada zao wanaolewa na wahuni tu. Wanawapa mimba wengine na kuwatelekeza.
 
Mkuu kwangu Mimi nampongeza sana huyo jamaa, amefanya kitu cha heshima lakini pia kalipa fadhili mlizomfanyia kwa kuunganisha ukoo na kufanya kuwa na udugu wa kudumu,jisikie amani,Dada yako kuolewa na huyo bwana haina tofauti hata angeolewa na Mimi,

Nitakupa mifano huu toka kwa familia ya bibi kizaa mama,ambapo alibahatika kuwa na watoto wa kike watatu akiwemo mama yangu,bibi alikuwa ni mpishi katika middle school wilaya furani enzi hizo, kutokana na khali ya bibi kuwa mpishi na kupenda kuishi na kijana,mwanafunzi wengi walikuwa wanasoma hapo middle school walipendelea kuja kuishi kwa bibi na aliwalea kama watoto wake,

huwezi amini watoto wote wa bibi waliolewa na vijana aliokuwa akiwalea na kuwatunza kama watoto wake ,miongoni mwa hao waoaji ni baba yangu mzazi na ndoa zilidumu vizuri tu hadi vifo vimekuja kuwatenganisha,

Kama kweli wazazi wamelidhia naimani ndoa hivyo itadumu daima,na kwa mwanamme sioni kama ataweza kumtenda hiana mwanamke kutokana na mazingira aliyokulia na kulelewa na wazazi wako,wewe ulitaka upate mashemeji wenye kuvaa milegezo na kunyoa viduku?

Let your sister marry the man,hence feel free,maisha yao wewe hayakuhusu ,pambana na maisha yako au wewe ilikuwa na mpango wa kumuoa Dada yako dheni jamaa kautibua?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daah, hii kuna mahali niliiona na jamaa bado ni marafiki.
 
Kuna mambo mengi sana wazazi wako wameangalia kabla ya kumkubalia kumuoa dada yako ila kiufupi wameona ndiye mtu sahihi kuishi na dada yako..muunge mkono tu huyo jamaa ili undugu uzidi kuimarika na wala huna sababu ya kumchukia jamaa maana hutaweza kumuoa dada yako
 
We boya Sana sasa utamuoa wewe wakati rafiki yako kakusaidia kumuhifadhi Dada hata usipoenda harusini ataoa tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa maada omba msamaha kwa wanajukwaa, huoni wote wako tofauti na mtizamo wako...kama bado roho inakuuma mtafute dada ake na mshikaji nae umtie mimba na umuoe hapo itakuwa ngoma droo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…