Mshkaji wangu anataka kumroga mama watoto wangu

Mshkaji wangu anataka kumroga mama watoto wangu

Asilimia kubwa sana ya wanawake wanaoolewa wakiwa wadogo (miaka 20 kushuka chini) hua wanakuja kusumbua sana sana sana wakifika miaka 30+ hivi.. Yaani hua wanacharuka vibaya mno, hawashikiki hawaambiliki ni kama wanawehuka. Binafsi nina mifano zaidi ya mingi ya aina hiyo.
Bora wewe umeona. Ni balaa si ya nchi hii. Ndoa inatakiwa kuingiwa na walioisha tulia, awe mwanaume au mwanamke
 
Tatizo ataanza kuchapwa akiwa katika ndoa mpaka achoke ndipo atatulia. Lipi bora, upate aliyetulia au atakayekuhangaisha katika ndoa
Kwanza ndugu yangu kumbuka ya kwamba hamna mbususu yako peke yako....ni wakati wako tuu.
Hivyo basi tuachane na haya mambo ya wivu juu ya mbususu
 
Sijawah muomba msamaha baada ya yeye kuondoka home.
Sijawah mpigia simu wala kutuma ujume mfupi hata sasa ninavyoandika hapa.
nilisitisha mawasiliano nae, hato niliyafanya kabla hajaondoka home
- nikapelekwa gender desk police kuwa nimetelekeza na situnzi familia na mimi ni mnyanyasaji, nikapangua mashtaka kwa hoja na vielelezo, kesi kule ikamgeukia yeye, hata hivyo nikamuomba radhi na kumsihi tuyamalize, akagoma kabisaa. Hakuridhika

Mara nyingine ukioa usiseme nisamehe mke wangu sema yameisha na usiseme kwa unyenyekevu.Kujishusha kwa mwanamke yeye hukushusha zaidi mwanamke kama anania ya kukuacha hata uombe msamaha unalia na kugalagala bado atakuona boya tu.Mwanamke mwenye nia ya kuwa nawe hata usipoomba msamaha yataisha tu.

Nadhani hdi sasa jibu unalo pamoja na kuomba kwako msamaha bado hajakusamehe.Sema mkuu huna aibu kusimulia hiki kisa maana inaonekan hapa duniani hakuna mwanamke mwingine kama mke wako.Swala la kukutukania mzee wako alipaswa asiwe na meno hata 4 halafu unachimba unatokomea si watoto anao shida yako iko wapi? Umemuabisha sana mzee.
 
Mleta mada amekuwa dhaifu sana kwa mkewe. Huyo mama anajua udhaifu wako ndio ameona akuchapie hapo hapo.

Kingine, nasikia wanawake wa kinyakyusa sio poa. Pole sana!
 
tafuta mwanasheria akusaidie acha kuwa mjinga utafungwa kweli ukifanya mchezo

Kama ndoa haiwezekani si kuachana kwa amani ya nini kusumbuana tena
 
- nikapelekwa gender desk police kuwa nimetelekeza na situnzi familia na mimi ni mnyanyasaji, nikapangua mashtaka kwa hoja na vielelezo, kesi kule ikamgeukia yeye, hata hivyo nikamuomba radhi na kumsihi tuyamalize, akagoma kabisaa. Hakuridhika

Mara nyingine ukioa usiseme nisamehe mke wangu sema yameisha na usiseme kwa unyenyekevu.Kujishusha kwa mwanamke yeye hukushusha zaidi mwanamke kama anania ya kukuacha hata uombe msamaha unalia na kugalagala bado atakuona boya tu.Mwanamke mwenye nia ya kuwa nawe hata usipoomba msamaha yataisha tu.

Nadhani hdi sasa jibu unalo pamoja na kuomba kwako msamaha bado hajakusamehe.Sema mkuu huna aibu kusimulia hiki kisa maana inaonekan hapa duniani hakuna mwanamke mwingine kama mke wako.Swala la kukutukania mzee wako alipaswa asiwe na meno hata 4 halafu unachimba unatokomea si watoto anao shida yako iko wapi? Umemuabisha sana mzee.
Ahahah.
Sawa ,suala lankuwa na aibu inategemeana na vitu vingi. Mimi ni muwazi, utakavyonielewa wewe sasa hilo haliko ndani ya uwezo wangu
 
Nimeusoma mkasa wa jamaa kwa kweli bado hajawa mwanaume kamili halafu kwanini mwanamke anakudharau kiasi hicho?
Nguvu za kumkaza vizuri inaonekana ni tatizo na ndio maana analeta dharau kama hizo kwa sababu yupo tayari kukujibu na kukufanya kila aina ya vitimbwi.

Huyu Mshikaji inaonesha anampenda sana huyu mwanamke na manzi ashalijua hilo ndio maana anamuendesha kama gari bovu.
Hakika mwanamke kama anania ya kuishi nawewe hata kama usipo omba msamaha bado atakuwa nawewe maana wanawake wote wanajua kuwa mwanaume kamili haombi msamaha hata kama umfumanie live.Hata ukiomba msamaha kama hana nia ya kuishi nawewe haitasaidia kitu.

Jamaa atasumbuliwa sana hata akioa yule manzi atakuwa anakuja kufanya vurugu pale maana anajua fika maamzi ya jamaa sio ya kiume.Kuna tofauti kubwa sana kati ya kulipiza na kufanya maamzi.

Kuna muda mwanaume ufanye maamzi magumu hata kama yatakuacha na maumivu makali ni sawa maana hayatadumu yataisha na kusonga mbele sio unakubali kulala ovyo kama popo tena kwa gharama kisa uzembe tu wa kutokufanya maamzi mapema.
 
Mleta mada amekuwa dhaifu sana kwa mkewe. Huyo mama anajua udhaifu wako ndio ameona akuchapie hapo hapo.

Kingine, nasikia wanawake wa kinyakyusa sio poa. Pole sana!
NI kwel kamanda, japo mi sio dhaifu, ila napendelea zaidi peaceful means katika kutatua changamoto.
 
NI kwel kamanda, japo mi sio dhaifu, ila napendelea zaidi peaceful means katika kutatua changamoto.
Mchukulie mtu vile anavyokuja, dunia ya sasa haina huruma. Kitendo cha mama watoto kuondoka na documents za muhimu ni ishara tosha kuwa ana jambo baya anataka kufanya, undugu na urafiki unafia hapo.

Angalia welfare yako na hao madogo, yeye ameshakuwa adui yako, huna namna unaweza kumrudisha kwenye line tena.
 
Tafta kwanza ule wimbo wa Banana Zorro unaitwa Zoba, sikiliza huo kisha uje hapa tuzungumze kiume sasa
 
Mchukulie mtu vile anavyokuja, dunia ya sasa haina huruma. Kitendo cha mama watoto kuondoka na documents za muhimu ni ishara tosha kuwa ana jambo baya anataka kufanya, undugu na urafiki unafia hapo.

Angalia welfare yako na hao madogo, yeye ameshakuwa adui yako, huna namna unaweza kumrudisha kwenye line tena.
Nakubaliana na wewe mkuu
 
Wakuu heshima kwenu.
Sipendelei sana kuingia deep kwenye mkasa mzima unaoihusu familia yangu , especially mimi na wife.
Ila kwa kifupi tu, wife alizingua big big big time (usiulize nini maana ni ishu serious sana inayoweza husishwa na suala la uaminifu moja kwa moja)

Na nilipotaka maelezo toka kwake, akanijibu shit kwel kweli, nikaona this is too much, nikamchapa vizuuri tu.
Ila akili ziliponirudia nikaona nimefanya sio kitu kizuri, nikamuomba radhi.

Huu ukawa mwanzo wa mambo mengi sana, wife na ndugu zake waka kaa kikao, wakamshauri kuwa aachane na mimi. Akaanza harakati za kutekeleza maazimio ya kikao chao
Baada ya 10 days, aka force akatafuta pf3, akatafuta cheti cha daktari (alihonga).
Baada ya hapo, akaenda polisi, akakata RB (koote huko alishatafuta watu yeye akisaidiana na ndugu zake). Haya yoote yalikua yanafanyika bila mimi kujua chochote, nimekuja kuyafaham too late.

Akatega siku niko ofisini, nimeondoka tumeagana vizurii kabisa kwa vicheko (Nisijue moyoni anaendelea na mipango ya kuniingiza kwenye 18 zake).
Ile narudi home, nakuta ,kabeba watoto wangu, kabeba hati ya nyumba na eneo, kabeba card ya gari na vyeti vyake vyooooote vya taaluma na ajira (mtumishi wa serikali yeye) akasepa.
Nikaja gundua kuwa ni kaka yake alimfuata.
Basi siku bother kumtafuta. Nikatoa tu taarifa nyumbani kwetu kwa wazee.

E bwana ee, baada ya hapo, nikaanza kupelekewa moto,

- nikapelekwa gender desk police kuwa nimetelekeza na situnzi familia na mimi ni mnyanyasaji, nikapangua mashtaka kwa hoja na vielelezo, kesi kule ikamgeukia yeye, hata hivyo nikamuomba radhi na kumsihi tuyamalize, akagoma kabisaa. Hakuridhika

- wazee wangu wakaja, wakakaa kama familia na familia yake, mbele ya kikao, akamtusi baba angu, akatamka kuwa hanipendi wala hanitaki tena, na hata watoto sitakaa nije kuwaona tena. Nikamsihi, kwann unafanya haya hali wewe ndio sababu ya yote haya mpaka nikakupiga , akagoma katakata, kikao hakikuisha na suluhu ila ndugu zake wakasema hii ndoa lazima ivunjike. Hakuishia hapo

- akanipeleka baraza la usuluhishi la kata, hapa lengo lake ni kupewa form no.3 ili akafungue shauri la kudai talaka mahakamani. Wale wazee wa baraza walipotusikilizaa, wakamuona hana hoja, wakamuuliza wewe ni nani aliyeingilia kati na anakuendesha na kukudanganya? Mmezaa watoto wa 4, unataka talaka ya nini?? Wakamwambia, nenda kajifikirie upya ndio urudi tena, tutakupa. Huku nako akaonekana hana hoja ya msingi, na bado nikawa namsihi aghairi maamuzi yake ila waaap. HAKURIDHIKA

- juzi kati, niko mkoa mmoja kanda ya ziwa, napigiwa simu na mkuu wa upelelezi , kuwa nahitajika kituoni.
NIkasafikiri mpaka dar, kufika na kureport, namkuta wife pale, nikakamatwa na kutiwa ndani ( lockup). Hapo polisi wakachukua funguo za nyumbani kwangu wakampa wife, akaenda akasomba vitu vya ndani, akaondoka kwenda kupanga na kuanza maisha mengine akiwa na watoto, ambao toka alipokimbilia kwao nao mwezi November 2024.

- nikatoka nje kwa dhamana, hata muda huu niko chini ya dhamana na ninatakiwa ku report kituon after every short period of time.

SASA KISA KINAANZIA HAPA JAPO NI KIFUPI
Currently ,nikagundua wife kadhamiria kunikomesha, kazi zangu ni za kusafir, ila kwasasa siwez enda safari zaidi ya week kwasababu natakiwa kituoni kila mara.
Baada ya kuondoka home, imani yangu kwake ikatoweka nikahisi huyu asije nifanyia kitu mbaya, kwa muda nikawa nalala lodge, hiz zote ni gharama natumia.
Kazi zangu ni kama zimekwama.
Kesi yangu kimsingi ni kama imeshatoka polisi, ila chaajabu ni kwamba hawataki kuipeleka mahakamani, wananisumbua sana na masuala ya ku report kila mara kituoni.
Yale matumaini yoote ambayo nilikua nahis huenda hiz za wife ni hasira tu, nikaja gundua she is seriously intending to destroy me.

Shida yangu kubwa, mimi siiwezi michezo ya ubaya ubwela. Mimi ni wale ambao Yesu alisema "mtu akikupokonya koti lako, mwachie na kanzu, pia, akikuambia twende maili moja, wewe nenda maili 2". Kwakifupi, mimi mambo ya kulipiza ubaya siyawezi.

Sasa siku moja nikiwa very frustrated, nikakutana na mwamba mmoja ni mshkaji wangu, class mate tukiwa chuo. Katika hapa na pale nikamsimulia madhira kwa uchache aliyonitendea shemeji yake. Huyu jamaa anamjua wife maana mimi nilizaa mtoto wa kwanza na huyu mama tukiwa chuo mwaka wa kwanza, na ile hustle ya malezi na matunzo walikua wanaiona maana tulikua tuna kaa hostel moja kigamboni nikiwa mwanafunzui ninaye survive kwa pesa ya boom.

Bas nilipomsimulia (hapo kabla sijawekwa ndani) , jamaa akasikitika sana. Akanitia moyo akasema yatakwisha.
Ila mshkaji niliona kalichukulia lile suala kwa uzito sana. Alitamka neno moja tu "ni yule shemeji uliyekua unamhangaikia enzi zile tukiwa chuoni??? (Over 10 years ago)"

Nikamwambia ndio huyo huyo nilioa.Basi jamaa akafikiria akasepa.

Sasa jana jioni nikiwa facebuk, akaniona online, akaniuliza "braza kimya sana, lile jambo vipi linaendeleaje?"

Nikamwambia "jambo limekaa vibaya sana, hapa penyewe nimetoka lockup nina siku 2 tu, niko nje kwa dhamana, shemeji yako kaamua kuninyoosha"

Jamaa hakua na maneno mengi, akaniuliza "hivi shemeji majina yake ni nani?"
Nikamtajia.
Akaniuliza anafanya kazi maeneo gani? Nikamtajia.

Akasema "braza, nitahangaikia hili suala kwaajili yako,wewe ni ndugu yangu tumetoka mbali, siwezi ona unateseka namna hii kisa mwanamke yeye kakaa tu ana enjoy na mmezaa watoto"

Nikauliza , "una plan kufanya nini"
Akasema "huyu, ningepata mchanga wa mahala alipokanyaga nyayo zake ingekua vizuri, ila sio kesi kwakua ushaniambia anafanya kazi maeneo gani, hii pia itasaidia"

Hapa nikashtuka, nikamwambia "braza , naomba kwanza utulie, next week natakiwa ku report kituoni pamoja na yeye, baada ya kusikia nini kinazungumziwa huko nitakupa feedback kwanza"

Akasema "sawa, na kabla hujakwenda huko, nitakuambia nini cha kufanya"

Wakuu, hapa kwa akili yangu ndogo kabisa, nikajua tu kuna "juju" linataka kuandaliwa, wife apigwe "kimbola/kombora" ila nikasema kwanza "hold on".

Wazee mimi si mtu wa mambo hizo.
Na hata kama huyu mama kashaamua kunipiga pini, ila bado tuna watoto nae na anao yeye, hata kama yeye kanikusudia mabaya, honestly mimi bado namuwazia mema.

Japo kwasasa nishaona kuwa hakuna dalili wala matumaini yoyote ya sisi kuwa pamoja tena, na nimeshaanza ku move on, na yeye alishaga move on kitambo i think ndio maana ananitenda ubaya huu.
Mke wa miaka 15, tulioana na kuzaa mapema sana, maana mimi ndio kwanza sasa nina 35 yrs na yeye 36 yrs.
Ila kiukwel kanikusudia mabalaa mabaya sana, na mshkaji wangu anataka kupambana nae kupitia teknolojia ya "anga za juu", ila mimi kiukwel, I DO NOT WISH HER ANYTHING BAD".

Ungechukua uamuzi ganu juu ya msaada kama huu ninaopewa na mdau wangu?

Jioni njema
Kuna kitu umetuficha. Huo ubaya ubwela wa mkeo aliuanza baada ya wewe kumfanyia nini?
 
Acha hicho kisasi kwa ajili ya Roho yako na ya watoto wako. Chochote utakachomfunga nacho kitahamia kwa watoto wako uliozaa nae. Tafuta wakili lazimisha kesi iende mahakamani. Vitu amevipata kwa ulaghai so wakili anaweza kuvidicredit mahakani. Pia fungua shauri la kuibiwa document kama zipo kwa jina lako. Ameiba document za umiliki wa nyumba, gari na vitu vya ndani. Tumia sheria hiyo hiyo kumkomesha. Nahiyo hati ya talaka ruhusu itoke. Hawezi kuishi na wewe tena. Usiharibu sifa yako njema mbele za Mungu kisa mwanamke.
 
Kwanza ndugu yangu kumbuka ya kwamba hamna mbususu yako peke yako....ni wakati wako tuu.
Hivyo basi tuachane na haya mambo ya wivu juu ya mbususu
Tatizo siyo wivu wa mbususu bali madhara ya mwanamke kuitoa nje. Kuna utofauti mkubwa kati ya mwanaume na mwanamke wakichepuka. Mke akichepuka anaenda mzima mzima. Kwa vile wanawake huwa hawana tamaa bali hupenda. Na anayechepuka naye ndiye dereva wake. Ona madhara ya uchepukaji wa mke wa Fanton Mahal . Issue siyo wivu wa K bali madhara yatokanayo na uchepukaji. Miaka 15 si mchezo
 
Sio kwamba sitaki kumuacha, nilikua nafikiri ni hasira tu hapo mwanzo ndio maana nikawa natafuta suluhu. Ila sio kwamba ninamganda, ndio maana alipoondoka sikujisumbua kumtafuta, na alipoona nimekaa kimya ndioa akaanza kunipeleka kwenye vyombo vya sheria.
Chaajabu ni kwamba anataka taraka lakini hajapeleka shauri la talaka mahakaman mpaka sasa
Mwenzako yuko smart, kumbe bado mpaka sasa hujaweza kusoma process za diverce pamoja na Tanzania divorce proceeding laws. Please rejea vifungu vya sheria ya divorce vimeelezwa vizuri sana humuhumu ndani ya jamii forum tena kwa ustadi wa hali ya juu kuliko documents nyingi nilizosoma;Waandishi wamesummarize vizuri sana, tena sana, tatizo wengi tunasoma topics za mapenzi , udaku , mipira n.k.

Hoja yangu ni mara nyingi sisi wanaume tuna huruma sana, halafu tunadhania kwamba ni hasira au amechanganyikiwa, wanawake wakireact namma hiyo wamedhamilia, tena wanaweza kujifanya chizi ili kuwapumbaza kumbe mwenzako ndiyo hivyo anakusambaratisha chali, taratibuuuuuuu.

Huyu mke wako youko smart kuliko unavyofikiri, tena inawezekana kapata washauri wanaojua sheria, unasema anataka divorce lakini bado hajatender divorce mahakamani. Lazima ujue kuwa huwezi kutenda divorce mahakamani bila kuwa na maandishi ya Ward Marriage Reconciliation Board (WMRB) au mabaraza ya kanisa, Ile kamati ya usuruhisho ya kata, ile aliyokupeleka wakamzingua. Sasa atakuwa anatafuta plan B husifikiri amekata tamaa.

Naunga mkono hoja ya kukaa kimya, endelea na shughuli zako ila husilizike, ningekuwa mimi ningeenda kwenye kata nikaaomba wajumbe watoe kibali cha taraka , muende mahakamani kila mtu apewe chake muachane kwa amani ili wewe uendelee na pilikapilika zako, kwa sasa wewe umefungwa physically and physchologically.Fanya hima hujitoe kwenye kifungo , uwe huru bro.
 
Back
Top Bottom