Mifumo ipo clear kwa makampuni yote:
1.Unaongea na shipping agent mfano Mapembelo, GNM cargo, silent ocean, Unique, shamwaa, Faith Royal cargo nk utachagua wewe moyo wako unapoangukia then watakupa ADDRESS YAO YA CHINA, hyo address utaicopy kama ilivyo.
2. Utaenda Alibaba, madeinchina, 1688 hao wote ni wauzaji wa jumla, utachagua bidhaa unayotaka utarequest alaf muuzaji atakujibu na utamuuliza maswali yote unayoona kwako ni sahihi kama sizes, color, quality, pia unaweza kumuomba akutumie real picture/video.
3.Utakubalina na supplier bei kama ukiridhia bei aliokutajia na mmenegotiate mpaka mkaafikiana atakuomba ADDRESS YA CHINA ili iwe rahisi na kuokoa gharama ya shipping then hile address ulioCOPY kwa shipping agent ndio utampa alaf yeye atakupa gharama ya shipping kutoka kiwandani/warehouse yao mpaka kwa shipping agent wako, hyo bei itajumuishwa kwenye gharama ya bidhaa yako.
4. Kama ni bei ndogo mfano chini ya $500 unaweza kutumia VISACARD ya voda kama huna card ya Bank inayoruhusu transaction online then utalipia kazi itabak yeye kuship kwenda kwa agent wako, ila kam ni mzigo mkubwa sana huwa wanataka 50-60% ya malipo alaf wao wanaanza kuprocess mfano kama ni order ya kiwandani ukilipa hyo wataanza kukutengenezea kutokana na makubaliano yenu wakimaliza utamalizia alaf wanakusafirishia kama taratibu za bidhaa zingne ndogo ndogo.
Jitahidi sana kuongea na supplier ili ujue muda atakaotumia mpaka mzigo wako unafika kwa shipping agent ili nawewe uendane na timetable za meli.
5. Baada ya taratibu hzo kukamilika na mzigo kufika kwa shipping agent wako kazi itakuwa imebaki kwa agent wako kukusafirishia kuja Tanzania kama ni kwa meli huwa inachukua siku 30-45 mpaka kupokea mzigo wako japo wapo wengne wanachelewesha sana mizigo.
Agent wako atakupa gharama ya mzigo wako ili ujiandae mapema pale mzigo unapofika uweze kulipia na kwenda kwenye ofisi zao kuchukua.
Meli wanapina kwa CBM (Cubic meter) ila ndege mizigo yote inapimwa kwa KG.
Pia inakuwa vizur kuomba Supplier wako wa kichina kukupa makadirio ya CBM u Uzito wa bidhaa yako ili upige hesabi zako kama utapata faida au Maana unaweza ukajikuta umeingia hasara so lazma uwe makini hapo.
Mambo mengine namna ya kumchagua supplier wadau wengne wataongezea maana mambo ni mengi hatuwez kumaliza kwa article moja labda ningekuwa kwenye computer ningeiandaa vizur zaid.
Karibuni kwenye ulimwengu wa digitali ambao unaagiza mzigo china na unapambana bei na wauzaji wa jumla kariakoo.