Nangu Nyau
JF-Expert Member
- Jul 1, 2022
- 5,015
- 14,139
Wewe lazima una tatizo kubwa la uelewa. Ni kwa asili yako una akili kidogo cha kushindwa kuelewa au unajifanya huna akili?
Hakuna anayemsema Kikwete ni msaliti kwa vile hakumpa Urais. Usaliti na unafiki wa Kikwete ni pale ambapo Kikwete aliweza kumhadaa Lowasa kuwa ni rafiki yake kumbe ni adui yake mkubwa.
Lowasa alichohitaji toka kwa Kikwete, hata bila ya urafiki wao, ni kutendewa haki. Kikwete alimnyima Lowasa haki yake ya kuomba kupitishwa kuwa mgombea wa CCM. Kikwete alihakikisha jina la Lowasa halimo miongoni mwa majina ya kupigiwa kura na wajumbe wa CCM.
Lowasa, bila hiyana, akaondoka CCM, akagombea Urais kupitoa CHADEMA. Lowasa akachaguliwa na mamilioni ya Watanzania, na kwa hakika ya 100% alishinda. Kutangazwa kuwa ni mshindi ilikuwa ni haki yake, hata asingekuwa rafiki wa Kikwete, lakini Kikwete kwa ushetani wake, akaamua kuzuia kutangazwa kwake, na kisha kuwakamata na kuwaseka magerezani watu wote waliokuwa wanajumlisha kura za Lowasa.
Ushetani huo wa Kikwete haukuishia kwa Lowasa, alifanya hivyo hivyo kwa Hayati Maalim Seif. Kimwete inaonekana kudhulumu haki za watu ni asili yake. Na mtu mwenye moyo wa dhuluma lazima ni zao la shetani.
Mwenye mamlaka ya kukata majina ya watu kamati kuu ni JK (mwenyekiti ) peke yake?
Una ushahidi gani usio na shaka unaoonyesha EL alishinda uchaguzi na sio JPM? Tume ya uchaguzi Tanzania ilimtangaza JPM na sio EL.
Kukamatwa wajumlisha matokeo ya uchaguzi ni suala la dola na mamlaka zake, una uhakika gani kama hao watu hawakuwa wajumlisha uchaguzi bali walikuwa wanamanipulate kura.
Tujiepushe sana na "hearsay" za mitaani, maana Kila mtu anaweza kuongea la kwake ilimradi linamfavor na kumfurahisha yeye.
Toka 1995 mpaka uchaguzi wa mwisho 2020 wapinzani hulalamika wameibiwa kura na matokeo ni kwamba wameshinda, kuanzia Lyatonga Mrema mpaka TL, lakini ukijaribu kuutafuta ukweli unakutana na "hearsay" na story za vijiweni tu.
2025 tunakwenda kwenye uchaguzi mwingine huku tukilalama tume sio huru na blah blah nyingi halafu tukishindwa tunasema tumeibiwa kura, kwanini tusihakikishe tume inakuwa huru na Kila kitu tunajiridhisha nacho ndio twende kwenye uchaguzi ili tuepuke maneno ya tumeibiwa kura.