Msiba wa Lowassa ni gunia la misumari kwa Kikwete

Msiba wa Lowassa ni gunia la misumari kwa Kikwete

off course kikwete alikuwa anasimamia mwiko wa baba wa taifa, tatizo aliyeingia nae alikuwa ndani ya mwiko!
N. B, katika kutimiza miiko huwa hatuangalii sura,tuna kata na kufunua.
-Tutazunguka mbuyu lakini hii ndiyo sababu kuu,
Mwl, Jkn, alishamnongoneza,tuongozwe na vikabila vidogovidogo, yameshapita tugange yajayo!
 
Leo nimemuona Kikwete pale kwenye msiba Monduli. Hali yake haikuwa ya kawaida kabisa na mwishowe aliondoka na sijui hata alipoenda.

Sasa sijui alikuwa na tatizo la kiafya au ni kitu gani? Alikuwa hawezi kukaa kwa utulivu kwenye kiti chake. Na sura yake ikionyesha kama vile alikuwa na maumivu flani.

Mwili wake ulikuwa una swing back and forth akiwa amekaa kwenye kiti. Na ni jambo ambalo naona kama alikuwa akishindwa kuji control. Baada ya muda kile kiti chake kilikuwa wazi kabla hata Rais hajaondoka. Kwasababu kiitifaki, hakuna anayeruhusiwa kuondoka kabla ya rais.
Wahka wa nafsi.

Anaonyesha ujasiri wa macho tu lakini moyo una msuta. Mauti ya Lowassa yamemkumbusha kuwa kila kitu ni cha muda tu hapa duniani.

Hawezi kukiri makosa kwa vile kaaminisha akili yake kuwa hana kosa ila nafsi yake inamsuta na nina yakini anatamani wakati ungeweza rudi nyuma arekebishe makosa yake.

Kikwete wa msiba wa Lowassa na Kikwete wa msiba wa Membe ni watu wawili tofauti. Kwa Membe Kikwete alikuwa na huzuni ya kuondokewa kwa Lowassa Kikwete ana huzuni ya matendo yake kwa Lowassa.

Inasadikika Lowassa hakuwahi kumkabili Kikwete kwa neno lolote baya na hii ni mbaya zaidi kuliko hata angemshambulia.

Binadamu wote tutakufa ila hakika jitimai ya Lowassa itamuua Kikwete very very very soon.
 
Na
Mkuu, hivi umewahi kumsaliti rafiki yako, rafiki aliyejitoa maisha yake kukusaidia kwa kila namna kutimiza ndoto yako? Ni mambo ya kawaida sana kibinaadamu kusalitiana ila maumivu yake ni pale rafiki yako anapotangulia kufa na hamkuwa vizuri sana au hamkuwahi kuombana msamaha.

Kibinadamu, hata kwa kujikaza vipi, Jk hawezi kuwa na amani tena. Na inaonekana kama wale marafiki zake wote wamemtema, ulimsikia Rostam akimzungumzia Lowassa na sababu ya kuondoka kwake CCM?
Na Hali hii itamtesa JK hadi atakapoitwa mbele za haki kupewa majibu ya alichokiyendaHak
Mwanasiasa gani katika nchi hii ambaye hajawahi kufanya dhulma?
Ya huyu ni kwa alichomtenda swaiba wake ni zaidi ya wote.
 
Kwa hiyo mlotaka ampe urais kisa ni rafiki yake? Thank u kikwete uliangalia maslahi mapana ya nchi kuliko kujali uswahiba nchi itumbukie shimoni japo jpm ndo alikuwa rais mbovu sana kuwahi kutokea Dunia hii

Wewe lazima una tatizo kubwa la uelewa. Ni kwa asili yako una akili kidogo cha kushindwa kuelewa au unajifanya huna akili?

Hakuna anayemsema Kikwete ni msaliti kwa vile hakumpa Urais. Usaliti na unafiki wa Kikwete ni pale ambapo Kikwete aliweza kumhadaa Lowasa kuwa ni rafiki yake kumbe ni adui yake mkubwa.

Lowasa alichohitaji toka kwa Kikwete, hata bila ya urafiki wao, ni kutendewa haki. Kikwete alimnyima Lowasa haki yake ya kuomba kupitishwa kuwa mgombea wa CCM. Kikwete alihakikisha jina la Lowasa halimo miongoni mwa majina ya kupigiwa kura na wajumbe wa CCM.

Lowasa, bila hiyana, akaondoka CCM, akagombea Urais kupitoa CHADEMA. Lowasa akachaguliwa na mamilioni ya Watanzania, na kwa hakika ya 100% alishinda. Kutangazwa kuwa ni mshindi ilikuwa ni haki yake, hata asingekuwa rafiki wa Kikwete, lakini Kikwete kwa ushetani wake, akaamua kuzuia kutangazwa kwake, na kisha kuwakamata na kuwaseka magerezani watu wote waliokuwa wanajumlisha kura za Lowasa.

Ushetani huo wa Kikwete haukuishia kwa Lowasa, alifanya hivyo hivyo kwa Hayati Maalim Seif. Kimwete inaonekana kudhulumu haki za watu ni asili yake. Na mtu mwenye moyo wa dhuluma lazima ni zao la shetani.
 
Kweli, familia ya Mzee Lowassa haijamtaja kabisa kabisa Mzee Kikwete, watu wengi mno wamepewa shukrani za kipekee, ila Mzee JK hata kutajwa hakuna, dah

Kikubwa cha kushukuru Mzee JK nae anajua sana uvumilivu na kulinda ulimi wake..!!

Yaani mlitegemea mtu mdhulumaji wa haki za watu kwa sababu ya madaraka ashukuriwe? Huyu ndiye alidhulumu ushindi wa Maalim Seif huko Zanzibar. Alidhulumu ushindi wa Lowasa. Alidhulumu maisha ya Dr Ulimboka, hata akaponea chupuchupu.
 
Una mana Gani? Kwamba akina makamba hawana elimu ya kutisha kumpita lowasa? Kwanza lowasa kasoma fine arts.
Wapi kazungumzia elimu?kama na wewe unaamini Makamba na Amina Salum wana ushawishi kuliko Lowassa basi una matatizo makubwa.Anachozungumza hapo ni kwa nini JK hakuruhusu jina liende ili akapambane na akina Migiro,Makamba na Membe?
 
Hata kama ni wewe rafiki yangu uje unisukumie kashfa nipate ajali ya kisiasa nianguke kukulinda wewe, nijikongoje niinuke, uje tena unifyekelee mbali nisiyafikie maono yangu, huo moyo wa kukuvumilia undava wako mimi rafiki yako mkubwa nitautoa wapi?
Hatari sana mkwere yule
 
sikia rafiki yawezekana wewe hujui,jk kwenye issue ya lowassa alifanya sawasawa na wala hana baya lolote alilofanya,sasa kuhusu haiba yake,wajihi wake,jk anaumwa kansa ya tezi dume hivi unategemea awe na nguvu vipi?,umri pia umekwenda hawezi kuwa mkakamavu,hebu tumwache jk please
Mkuu Unaijua Tezi Dume?
Tezi dume ikishafanyiwa surgical.operation huwa haipo tena..
Kwahyo.usidanganye watu
 
taarifa za wakubwa tunazo sisi walalahoi. karibuni tuendelee kubeba tofari apa saiti. ayo ya wakubwa yatakupasueni kende mkashindwa kupeleka moto. mbele ya wanasiasa wanatuona sisi ni watwana na mapimbiroo
 
Kwann hutaki tumseme?
Kikwete hana kosa ukichungiza kiundani malalamiko yamegawika ktk chuki za kikanda chuki za kisiasa na udini kwa mbali lkn tujiulize kwann nyerere alimkataa kwa sababu zip na chama kilimkataa kwa sababu zip na kwanin kikwete alimchagu wazir mkuu anza na hayo maswali bila kusahau mfumo wa chama na serekali kiutendaji ukoje hapo utapata jawabu kikwete hana kosa lkn yy ametupiwa gunia la misumari lkn niswala la muda tu tutege skio tu
 
Hakuna wakati ambapo Kikwete amesemwa vibaya na kusutwa kama wakati huu wa msiba wa Lowasa. Mzee huyu amesutwa na kuzodolewa ktk namna ambayo siyo rahisi kwa nafsi yake kukosa maumivu.

Ni kwa vile tu moyo wa mtu ni kichaka huwezi kujua unaongea nn. Lkn hata kwa kumuangalia tu anaonekana usoni kwake kapoteza nuru, furaha na bashasha. Badala yake amejaa wasiwasi, wahaka na hofu.

Nimemuangalia leo alipoinuliwa ili kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Lowasa alitembea kwa uoga na almanusura apepesuke mbele ya jeneza.

Familia ya Lowasa imewashukuru watu wengi sana lkn Kikwete hakutajwa hata kwa bahati mbaya. Yaani urafiki wake na Lowasa wakati wa ujana na uwepo wake msibani vyote vimepuuzwa. Huu ni msumari wa moto uliopigiliwa utosini kwa Kikwete.

Mwito.
Tujifunze kuishi vema na watu ili tuwe na mwisho mwema.
Kikwete ni mtu mnafiki sana, sishangai. Watu wengi wa pwani wana tabia hizo,ni watu wa kuogopa sana.

Fuata link ifuatayo uone unafiki wa Kikwete.

 
Hakuna wakati ambapo Kikwete amesemwa vibaya na kusutwa kama wakati huu wa msiba wa Lowasa. Mzee huyu amesutwa na kuzodolewa ktk namna ambayo siyo rahisi kwa nafsi yake kukosa maumivu.

Ni kwa vile tu moyo wa mtu ni kichaka huwezi kujua unaongea nn. Lkn hata kwa kumuangalia tu anaonekana usoni kwake kapoteza nuru, furaha na bashasha. Badala yake amejaa wasiwasi, wahaka na hofu.

Nimemuangalia leo alipoinuliwa ili kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Lowasa alitembea kwa uoga na almanusura apepesuke mbele ya jeneza.

Familia ya Lowasa imewashukuru watu wengi sana lkn Kikwete hakutajwa hata kwa bahati mbaya. Yaani urafiki wake na Lowasa wakati wa ujana na uwepo wake msibani vyote vimepuuzwa. Huu ni msumari wa moto uliopigiliwa utosini kwa Kikwete.

Mwito.
Tujifunze kuishi vema na watu ili tuwe na mwisho mwema.
Mkapa ,magufiri, lowasa huko kote kasemwa semwa sana sijui kwa nini
 
Back
Top Bottom