Msiba wa Lowassa ni gunia la misumari kwa Kikwete

Msiba wa Lowassa ni gunia la misumari kwa Kikwete

Tuachane na ubishi turudi kwenye uhalisia na turudi 2005 ,ushawishi ule wa JK ulitengenezwa na Lowassa ? Najua hii ni stori ya kijiweni ambayo mpaka kesho inasemwa hivyo
Hahahauahaaaa!
Yaani ikifika hapo mi ndo nawapuuuza kabisa hawa haters wa jk, kiukweli kuna ratizo mahali katika bongo za watz......?.'elimu, elimu, elimu' kama alivyowahi kusema mwendazake!
 
Ukimfanyia dhulma aliyewahi kuwafanya dhulma wengine tena inawezekana mlikuwa wote Kuna shida gani?

Tunawaita Boyz 2 Men walikuwa pamoja kwenye harakati zao, dhulma ngapi wamewafanyia watanzania kwenye harakati zao? au hapa yupo JK peke yake, EL na RA hawapo.
Dah, mwamba una maswali magumu sana!
 
Unatumika vibaya wewe, kama jk alimfanya Lowassa waziri mkuu halafu familia ishukru watu wengine ambao hawakumpa hicho cheo, kwako wewe unaona kawaida.?

Jifunzeni kuishi na watu vizuri, madaraka yana mwisho. Ni fedhea na ni aibu kubwa. Kwa Magufuli ilikuwa hivyohivyo akaishia kujitetea, leo hivyohivyo. Aibuu
Zirudie akili zako na hapa nitakuelekeza kwa mifano maana Biblia inatufundisha kutumia mifano.

Kwa mfano, umegombana na mtu aliyekuwa rafiki yako sana na ukawaambia watoto wako kwamba Fulani nimegombana naye msimuamini sana. Miaka ikasonga, mkaombana msamaha na uliyogombana naye mkayamaliza. Je, watoto watamsamehe huyo mtu kama ulivyomsamehe wewe?
 
Mtu aliyeshika nafasi ya Uwaziri Mkuu kwa muda mfupi lakini angalia muitikio na namna msiba wake ulivyokuwa ndipo utakapojua JK aliona mbali kwamba marehemu alikuwa na nafasi kubwa ya kumfunika kwa kila kitu ndipo akafanya ya kufanya.

Pumzika kwa amani Lowassa, Mungu amekuinua katikati ya watesi wako hata katika msiba wako.
Ukaskazini nao umempaisha Lowasa
 
Hahahauahaaaa!
Yaani ikifika hapo mi ndo nawapuuuza kabisa hawa haters wa jk, kiukweli kuna ratizo mahali katika bongo za watz......?.'elimu, elimu, elimu' kama alivyowahi kusema mwendazake!
Watoto wengi wa 2000 wanakua wanakutana na stori ya Lowassa kumuweka Kikwete madarakani halafu Sasa walivyo wepesi wa kubeba Kila stori wanaamini ni kweli.
 
Mkuu, hivi umewahi kumsaliti rafiki yako, rafiki aliyejitoa maisha yake kukusaidia kwa kila namna kutimiza ndoto yako? Ni mambo ya kawaida sana kibinaadamu kusalitiana ila maumivu yake ni pale rafiki yako anapotangulia kufa na hamkuwa vizuri sana au hamkuwahi kuombana msamaha.

Kibinadamu, hata kwa kujikaza vipi, Jk hawezi kuwa na amani tena. Na inaonekana kama wale marafiki zake wote wamemtema, ulimsikia Rostam akimzungumzia Lowassa na sababu ya kuondoka kwake CCM?
Una ushahidi au ni stori za vijiwe vya kahawa
 
Kwa hiyo mlotaka ampe urais kisa ni rafiki yake? Thank u kikwete uliangalia maslahi mapana ya nchi kuliko kujali uswahiba nchi itumbukie shimoni japo jpm ndo alikuwa rais mbovu sana kuwahi kutokea Dunia hii
Hakumpa nafasi ya kujieleza mbele ya wajimbe ambao ni wapiga kura kimsingi hakutendewa haki angewaacha wajumbe waamue
 
Kwa logic yako - Kama walikuwa marafiki na huu ni Msiba wa rafiki yake Ulitegemea awe na hali gani ?!!!
Furaha ?!!!!

Mimi kama mlipa Kodi ningekuelewa zaidi ungesema hawa jamaa wawili hawakututendea haki katika Sakata la Richmond - Hayo mengine nadhani yatakuwa hayatuhusu unless na wewe ni mwanafamilia....
 
Hakuna wakati ambapo Kikwete amesemwa vibaya na kusutwa kama wakati huu wa msiba wa Lowasa. Mzee huyu amesutwa na kuzodolewa ktk namna ambayo siyo rahisi kwa nafsi yake kukosa maumivu.

Ni kwa vile tu moyo wa mtu ni kichaka huwezi kujua unaongea nn. Lkn hata kwa kumuangalia tu anaonekana usoni kwake kapoteza nuru, furaha na bashasha. Badala yake amejaa wasiwasi, wahaka na hofu.

Nimemuangalia leo alipoinuliwa ili kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Lowasa alitembea kwa uoga na almanusura apepesuke mbele ya jeneza.

Familia ya Lowasa imewashukuru watu wengi sana lkn Kikwete hakutajwa hata kwa bahati mbaya. Yaani urafiki wake na Lowasa wakati wa ujana na uwepo wake msibani vyote vimepuuzwa. Huu ni msumari wa moto uliopigiliwa utosini kwa Kikwete.

Mwito.
Tujifunze kuishi vema na watu ili tuwe na mwisho mwema.
Wenye akili ndogo wanadhani uadui wa lowasa na kikwete ni personal,yaani wao binafsi walikosana wakawa maadui!!

Sivyo kabisa,urafiki wao ungedumu Hadi Leo ungeleta madhara kwa dola,ilikua lazima wakosanishwe Kwa vyovyote vile Kwa mstakabali was taifa la kesho!!

Urais was kupeana kama marafiki ni hatari sana Kwa taifa,ndio maana wanamtandao walipaswa kusambaratishwa Ili 2015 wasiingize mtu wao ikulu,na hilo Dola walifanikiwa sana kuwasambaratisha!

Mengine ni makosa ya kibinaadamu pale uadui unapozidi viwango!!

Nadhani!!
 
Hakuna wakati ambapo Kikwete amesemwa vibaya na kusutwa kama wakati huu wa msiba wa Lowasa. Mzee huyu amesutwa na kuzodolewa ktk namna ambayo siyo rahisi kwa nafsi yake kukosa maumivu.

Ni kwa vile tu moyo wa mtu ni kichaka huwezi kujua unaongea nn. Lkn hata kwa kumuangalia tu anaonekana usoni kwake kapoteza nuru, furaha na bashasha. Badala yake amejaa wasiwasi, wahaka na hofu.

Nimemuangalia leo alipoinuliwa ili kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Lowasa alitembea kwa uoga na almanusura apepesuke mbele ya jeneza.

Familia ya Lowasa imewashukuru watu wengi sana lkn Kikwete hakutajwa hata kwa bahati mbaya. Yaani urafiki wake na Lowasa wakati wa ujana na uwepo wake msibani vyote vimepuuzwa. Huu ni msumari wa moto uliopigiliwa utosini kwa Kikwete.

Mwito.
Tujifunze kuishi vema na watu ili tuwe na mwisho mwema.
We ulitajwa?
 
“Mheshimiwa Lowassa ni muhanga wa mifumo yetu ya uchaguzi. Alikuwa mgombea wa urais wa kwanza katika upinzani kupata kura zaidi ya milioni sita. Halikuwa jambo dogo…… The full potential ya uongozi wa mheshimiwa Lowassa haikuwahi kutumika, tuwape watu nafasi katika misingi ya kweli na haki, watumike” - Freeman Mbowe, Monduli, 17.02.24
 
Back
Top Bottom