Hakuna wakati ambapo Kikwete amesemwa vibaya na kusutwa kama wakati huu wa msiba wa Lowasa. Mzee huyu amesutwa na kuzodolewa ktk namna ambayo siyo rahisi kwa nafsi yake kukosa maumivu.
Ni kwa vile tu moyo wa mtu ni kichaka huwezi kujua unaongea nn. Lkn hata kwa kumuangalia tu anaonekana usoni kwake kapoteza nuru, furaha na bashasha. Badala yake amejaa wasiwasi, wahaka na hofu.
Nimemuangalia leo alipoinuliwa ili kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Lowasa alitembea kwa uoga na almanusura apepesuke mbele ya jeneza.
Familia ya Lowasa imewashukuru watu wengi sana lkn Kikwete hakutajwa hata kwa bahati mbaya. Yaani urafiki wake na Lowasa wakati wa ujana na uwepo wake msibani vyote vimepuuzwa. Huu ni msumari wa moto uliopigiliwa utosini kwa Kikwete.
Mwito.
Tujifunze kuishi vema na watu ili tuwe na mwisho mwema.
Lakini sababu hasa ya Jakaya Mrisho Kikwete kulaumiwa kwa ajili ya Edward Ngoyai Lowassa ni zipi?
Je, zaweza kuwa ni hizi mbili?
1. Inasemekana tangu mwaka 1995 walifanya alliance ya mmojawao either by hooks or by crooks ni lazima aje kuwa Rais na mwingine PM.
Mwaka 1995 waliingia kwenye mchujo. Hawakupenya kwa sbb mwasisi wa taifa hili Hayati Mwl. Julius K. Nyerere aliwapiga "veto". Nyota ikamzukia Hayati Benjamin William Mkapa
Hawakufa moyo. Waliendelea mbele na mipango yao hadi 2005. Mchuano ulikuwa mkali sana kati yao. Mazungumzo yakafanyika nje ya kapu la mchujo. Mkataba ukaingiwa kati yao kuwa EL amwachie JK na yeye zamu yake ingekuwa 2015 na sharti lingine ktk mapatano hayo likawa, angeshinda (JK), basi mzee EL angekuwa PM wake. Ndivyo ilivyokuwa.
2. Mambo yaliharibika mara baada ya safari yao ya matumaini ilipoanza Novemba, 2005.
Katikati hapo (mwaka 2008) ikazuka kashfa ya kampuni ya ufuaji umeme ya Richmond PLC.
Zigo la kashfa hiyo likamwangukia EL pekee. Rais na rafiki yake JK akashindwa kumlinda wala kumtetea.
Wapambe wakavuruga kila kitu. Na kwa sbb hiyo PM - Edward Lowassa akajiuzuru u - PM mwaka huo 2008.
Njiani pale wakapozana kwa namna walivyojua. Lakini wapambe wa katikati wasiotaka EL aje kuwa Rais, wakajaribu kila njia kumchafua na hata kumuua kwa sumu.
Hilo lilimsumbua sana EL kiasi cha kujiuliza nini kimempata rafiki yake (Rais JK) ambaye ana resources zote za kuhakikisha anamlinda lakini akashindwa kufanya hivyo hata kuacha mifumo ndani ya serikali na chama chao CCM kumsakama na ku - tarnish image yake kiasi kile.
Mzee akasubiri hadi 2015. JK alijaribu kutunza ahadi yake kumwachia rafikiye. Vurugu zilizotokea Dodoma mwezi Juni, 2015 wakati wa mkutano mkuu? Halmashauri kuu ya CCM? kuteua mgombea kila mtu anakumbuka na kuelewa vyema. Jakaya Mrisho Kikwete akamtosa rafikiye mchana kweupe!!.
EL kwa hasira akaondoka CCM na kujiunga na CHADEMA. Huko akapata nafasi ya kutimiza ndoto yake. Akagombea Urais kwa udhamini wa CHADEMA kushindana na mgombea wa CCM John P. Magufuli.
Ushindani ktk uchaguzi huo ulikuwa mkali sana. Kura zikapigwa na kuhesabiwa. Eti John P. Magufuli wa CCM akatangazwa mshindi. Lakini wachunguzi wa mambo wanasema wazi kuwa Lowassa ndiye aliyeshinda kwenye ballot box lakini ktk kutangazwa, akatatangazwa John P. Magufuli!!
Hilo likathibitisha pasipo shaka kuwa rafikie alikuwa na dhamira ya kumtosa tangu mwanzo. Angekuwa ni mtu wa kusimama ktk mapatano yao na kama huko CCM mlango ulijifunga pasipo kutarajua, basi JK alikuwa na uwezo wa kumpa rafikie u - Rais wake hata kupitia CHADEMA. Hakufanya hivyo!!
Hiki ndicho kinachomuumiza Jakaya Mrisho Kikwete. Dhamira yake inamsuta. Anaona aibu. Na yule mtu waliyempa u - Rais kupitia CCM (John P. Magufuli) alitumia nafasi na mamlaka yake sawasawa kuwanyoosha akiwemo yeye mwenyewe Kikwete.
Yaani Jini walilolifuga na kulilisha wenyewe (John P. Magufuli), likawageuka na kuanza kunyonya damu zao. Mwisho wa siku wakaona kuwa, ipo siku linaweza kuja kuwaua. Wakaamua kutumia umafia kuliondoa!!