Msiba wa Lowassa ni gunia la misumari kwa Kikwete


Mwenye mamlaka ya kukata majina ya watu kamati kuu ni JK (mwenyekiti ) peke yake?

Una ushahidi gani usio na shaka unaoonyesha EL alishinda uchaguzi na sio JPM? Tume ya uchaguzi Tanzania ilimtangaza JPM na sio EL.

Kukamatwa wajumlisha matokeo ya uchaguzi ni suala la dola na mamlaka zake, una uhakika gani kama hao watu hawakuwa wajumlisha uchaguzi bali walikuwa wanamanipulate kura.

Tujiepushe sana na "hearsay" za mitaani, maana Kila mtu anaweza kuongea la kwake ilimradi linamfavor na kumfurahisha yeye.

Toka 1995 mpaka uchaguzi wa mwisho 2020 wapinzani hulalamika wameibiwa kura na matokeo ni kwamba wameshinda, kuanzia Lyatonga Mrema mpaka TL, lakini ukijaribu kuutafuta ukweli unakutana na "hearsay" na story za vijiweni tu.

2025 tunakwenda kwenye uchaguzi mwingine huku tukilalama tume sio huru na blah blah nyingi halafu tukishindwa tunasema tumeibiwa kura, kwanini tusihakikishe tume inakuwa huru na Kila kitu tunajiridhisha nacho ndio twende kwenye uchaguzi ili tuepuke maneno ya tumeibiwa kura.
 
Kikwete ni mtu mnafiki Sana.Ila sishangai Sana watu wengi wa pwani Wana Tania hizo,ni watu wa kuogopa sana.

Unafiki ni tabia ya Watanzania wote tusitake kusingizia watu wa Pwani.

Watu wengi wa Pwani ni waislamu, kwenye uislamu moja ya kipengele kinachokemewa sana ni unafiki sasa sijui tunawezaje kuwahusisha watu wa Pwani na unafiki.

Watu wa Pwani wangekuwa wanafiki sidhani kama wangeweza kumkaribisha JKN aka Nyerere na kuishi naye Dar es salaam na kuwa naye kwenye harakati za uhuru mpaka kutoa hela zao mifukoni.

Watanzania tungekuwa sio wanafiki basi sidhani kama CCM Leo hii ingekuwa madarakani, Watanzania tungekuwa sio wanafiki sidhani kama Taifa hili lingekuwa masikini na watanzania wenzetu kutoka baadhi ya community wasingekuwa masikini.
Taifa lingekuwa sio la wanafiki basi ukabila na udini usingekuwepo maofisini na mitaani.
 

Wewe inaonekana ni mtu wa blabla sana. Watu wanaongea kwa evidence, wewe unaleta hadithi.

Timu ya ujumlishaji matojeo ya Lowasa ilikuwa inapokea nakala za nakala za fomu za matojeo zenye sahihi za wahusika wote. Kikwete baada ya kupata habari hizo, akaamuru kituo hicho cha ujumlishaji kura za Lowasa kivamiwe na kumbukumbu zote zipotezwe.

Katika hali ya kawaida, kama Kikwete asingekuwa na ushetani ndani mwake, si angewaachana hizo kumbukumbu zao, na kama kumbukumbu zilichezewa, sizingeletwa fomu original ambazo kila chama na wasimamizi wa uchaguzi walikuwa wanapewa?

Hivi unajua kwa kuogopa kuonekana wazi uhuni uliofanyika, walitangaza tu tarakimu za jumla bila hata ya kusema kila mgombea alipata kura ngapi toka kila mkoa, kama sheria inavyotaka?
 

Sasa Mimi nawewe nani ni blah blah, weka ushahidi unaoonyesha EL aliibiwa kura na alikuwa ameshinda uchaguzi.

Hao vijana hawakukamatwa na JK walikamatwa na dola kwa kutiliwa shaka kufanya vitendo vya kutiliwa shaka, wapi walikuwa registered na mamlaka na kutambulika kufanya hiyo kazi? Tume ya uchaguzi iliwapa kibali na kuwa aware na hao watu?

Tume pekee kisheria ndio yenye mamlaka yakujumlisha na kutangaza matokeo na si vinginevyo.

Brother unaniita Mimi blah blah wakati chote ulichoandika na kujibu ni hearsay na hakuna clear evidence yeyote toka hiyo 2015.
 
Unafiki wa some measure kila mtu anao,Ila watu wa pwani wamezidi.
 
JK ni mnafiki sana.Nani unafikiri kasahau alipo

Unafiki wa some measure kila mtu anao,Ila watu wa pwani wamezidi.
Narudia tena, WATANZANI WOTE NI WANAFIKI TU.

CDM: EL fisadi na wakamuweka kwenye list of shame, hao hao wanampa nafasi ya kugombea Urais na kutuliza ushahidi uko wapi El fisadi?
Musukuma Mbunge: alikuwa rafiki mkubwa wa EL na kutumia sana hela ya EL lakini alimkana na hata kumdhaliliisha kisa JPM.
CCM: Ilimuita EL fisadi, mwizi na mgonjwa, hao CCM wakampokea Kwa kishindo eti nimerudi nyumbani.
Watanzania JK akiwa Rais walisema wanataka Rais mkali na dictator, akaja Rais mkali na kaelement kaudikteta wakasema wanataka Rais kama JK mwenye ubinadamu.

Watanzania hawa hawa wanalalamikia wanaibiwa kwenye madini na makelele mengi, anakuja mtu anafumua mikataba ya madini wanarudi kusema tutashitakiwa.

Watanzania hawa hawa wakristo Kwa waislamu Leo hii wanapeleka watoto shule za kidini na kuacha shule za umma, watanzania hawa hawa kuna taasisi zimejaa ukabila na kama wewe si mchaga au mkristo hupati kazi, watanzania hawa hawa kuna taasisi wamejaa wahaya na wakristo kama huna uhusiano nao hupati kazi, zipo taasisi watanzania hawa hawa zimejaa waislamu (japo ni chache) kama wewe sisi muislamu hupati kazi.
 
Kikwete ni mnafiki kinoma mkuu.Hebu fuata link ifuatayo uone yaliyomtokea Chuo cha Kijeshi Monduli kwa sababu ya unafiki wake.

 
Walalahoi wanajadili ujinga ambao haumdhuru Kikwete yupo na maisha yake hana habari na maisha ya mtu. Kaeni kwa kutulia
Atakufa na wahaka, wewe subiri tu. Si umeona leo kaondoka mapema msibani huku akipepesuka!!?
 
Ume ongea Historia nzito mkuu, endelea kutujuza je zile Kash Kash kipindi Cha magu.
πŸ‘‰Ali fanya kweli, au ndo mbinu za kina jk??
 
Kama kawaida JK Huwa hajibu anaendelea na michakato yake
 
Urais haugawiwi kienyeji hivyo nyie mbumbumbu msiojua Siri.
 
Nyie wajinga kwenye mlitaka fisadi apewe urais , au mnazani urais ni kupeana tu, ndomana kikwete anabaki kuwa best president, kwa kumkataa huyo mzee
 
Jamani nafasi ya uraisi nchini ni moja tu na kuna watanzania wengi wanaiwinda kuwa siku moja inaweza kuwa bahati yao kama ilivyo tokea kwa Marehemu Magufuli.
Sasa marehemu Lowasa ndio Mwenyezi Mungu hakuwa na mipango ya yeye kuwa raisi. Kwa hiyo tukubali na tushukuru kwa neema nyingi alizobarikiwa na Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…