Msigwa amhoji Tundu Lissu kupinga Wamasai kuhamishwa Ngorongoro, Lissu akosa majibu

Ngorongoro itamalizwa na makazi ys watu mle ndani ,ingawa wengine wanasema ni tofauti na mbuga zingine ile conservation area lakini maana ya conservation si imetengenezwa tu na watu ,maana kama leo hii mikumi pataachwa watu watasogea hivo hivo taratibu hadi ndani ya mbuga . Ukiangalia mikumi pale Doma mashamba ya mahindi yanaliwa kila mwaka na tembo wanatokea hifadhini,watu wakilalamika wanaambiwa watoke karibu na mbuga ,na mnyama ukimgusa inakula kwako.

Leo wamasai wanakaa ndani ya mbuga kwani wana hadhi tofauti na watanzania wengine? Wengine wanasema wamasai wao wenyewe mle ndani ni kivutio kwa watalii lakini hata nje ya mbuga wanaweza wakafuatwa ,maana ukiangalia kwa mtalii karibia vile vjijiji vyote kuanzia karatu ni mvuto tosha ,pia ukiangalia watalii wanatoka nje wanaenda ziwa manyara kuangalia kabila la Hadzabe wanavyoishi na hapo ndani ya mbuga ,sasa wamasai wana uspecial gani sijui

Sent using Jamii Forums mobile app

Kweli kabisa hao watoke na iwekwe sheria kali ya uvamizi wa hifadhi hawa sio wa kuchekewa

Mimi shambani kuna wanyama wanakuja na sio hifadhi kuna nyoka wa aina nyingi na ndege wengi kwa sababu nimepiga marufuku kuchungia humu nikikamata faini
Na watoto kuwinda ndege marufuku
Tulikamata ndoo tatu za manati na makofi juu ila sasa hawasogei na kuna aina ya ndege 12

Sasa ningekuwa waziri mbona mngeona zizi na kantyentye na jolowe wamerudi mpaka mjini [emoji23][emoji23]
 
Hata Selous ilikuwa conservation area mpaka sasa kama sikosei,mbona hamna wamasai au watu wanafuga huko na wameweka makazi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Selous ni game reserve kuna tofauti kati ya National Parks, Game Reserves, na Conservation Areas.

Note: Mimi nipo neutral sijui kundi gani wapo sahihi khs hili sakata.
 
... nakubaliana na wewe kwa 100%.

Tatizo kubwa tulilo nalo nchi zetu hizi utakuta move yote hiyo kuna hila ndani yake;

Utashangaa wanawaondoa hao wamasai ili kupisha wenye fedha waweze kuwinda vizuri!

mbona mawindo yapo kila mwaka kila raia anaruhusiwa kuwinda mwezi wa 7 na unapangiwa wanyama wa kuwinda na wasizidi kiasi fulani kutokana na ongezeko la wanyama mtindo wa kuwinda upo miaka yote na mataifa yote huja kuwinda sasa kukazania waarabu tuu ni chuki za kidini au nini?
 
Botswana yenye almost eneo kama la kwetu wana only 6M people's na wanyama wengi kuliko idadi ya watu ila wana coexistence bila shaka
Sasa mkuu jangwani utalinganisha na nchi yetu kweli? Raia watakaaje jangwani mwamba? Halafu Botswana ina karibia kuingia mara 2 kwenye nchi yetu!
 
mbona mawindo yapo kila mwaka kila raia anaruhusiwa kuwinda mwezi wa 7 na unapangiwa wanyama wa kuwinda na wasizidi kiasi fulani kutokana na ongezeko la wanyama mtindo wa kuwinda upo miaka yote na mataifa yote huja kuwinda sasa kukazania waarabu tuu ni chuki za kidini au nini?
Sasa mwarabu ni race au ni dini? Mbona na wewe ni mjinga kiasi hiki?
 
Hata Selous ilikuwa conservation area mpaka sasa kama sikosei,mbona hamna wamasai au watu wanafuga huko na wameweka makazi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe unachanganya madawa. Hiyo mifano unayotoa huko kwingine kote ni tofauti na Ngorongoro. Ngorongoro wanyama na binadamu wameishi pamoja kwa muda mrefu sana. Hilo eneo wamasai wamekuwepo kwa muda mrefu sawa na wanyama. Ni kweli kwamba wamasai wameongezeka idadi na hawawezi kuendelea kukaa pale wote milele. Utaratibu ufanywe wapewe elimu na wahamishwe kwa staha. Wakubaliane na serikali kuwa idadi ya watakaobaki iwe ndogo. Tatizo kubwa lipo kwa serikali na wanaopiga debe wamasai wahamishwe. Serikali imetumia mbinu za janja janja kukabiliana na hili jambo. Kwa nini itafute wamasai bandia waseme kuwa wamekubali kuhama? Kwa nini ''waandishi'' wa habari uchwara kama kina Kitenge walivalia njuga hili jambo kiasi cha kuhonga waandishi wengine eti wasapoti uhamaji? Hapo inatupeleka kwenye hofu kuu ya watu wengi: awamu hii ina elements za ufisadi na upigaji nyingi, je, kuna namna nyuma? Je, ni kweli kwamba kuna watu wanataka kupewa hayo maeneo na ndiyo wanashinikiza? All in all, hili jambo siyo kubwa kama inavyodhaniwa kama serikali ingetumia uwazi na ukweli kulishughulikuia.
 
Uko sahihi kabisa mleta uzi. Kwa tulioishi kaskazini tunakumbuka hadi miaka ya mwanzoni mwa 90 ilikuwa ukishatoka tu nje ya Arusha kuanzia Kisongo utaona Mbuni, pundamilia na wanyama wengine kirahisi. Yaani hadi ufike kreta Ngorongoro huku njiani ushaona wanyama kibao. Watu wa wilaya za Karatu na Monduli walikuwa wakiwawinda kirahisi digidigi na wanyama wengine kirahisi ndani ya vijiji vyao. Lakini haya maendeleo yetu binadamu kama ulivyosema yamewaharibia sana wanyama. Siku hizi kutoka Arusha hadi Ngorongoro huwezi ona Twiga wala Pundamilia.

Halafu kitu kingine ambacho hakisemwi wala hutasikia masai akilalamika ni hili suala la wamasai kujeruhiwa au kuuwawa na wanyamapori. Pale zahanati ya Makao niliona masai kibao waliojeruhiwa vibaya na nyati. Na kuna cases za watu kuliwa na wanyama. Masai wao watajidai tu hawana noma na wanyamapori huku wakiteketea.

Mimi nashauri masai wapunguzwe tu sio wa kuwaondoa wote maana nao ni sehemu ya vivutio mbugani. Hata mimi kukuta mtu anachunga mifugo yake pale kreta pembeni ya Simba, Chui, Fisi na wakali wengine ni maajabu. Pia kuweza kushuka ule mlima na mifugo hadi chini na kurudi jioni salama ni maajabu mengine. Masai haogopi pori kabisa. Wabakizwe wachache kimkakati.
 
Wewe unachanganya madawa. Hiyo mifano unayotoa huko kwingine kote ni tofauti na Ngorongoro. Ngorongoro wanyama na binadamu wameishi pamoja kwa muda mrefu sana. Hilo eneo wamasai wamekuwepo kwa muda mrefu sawa na wanyama. Ni kweli kwamba wamasai wameongezeka idadi na hawawezi kuendelea kukaa pale wote milele. Utaratibu ufanywe wapewe elimu na wahamishwe kwa staha. Wakubaliane na serikali kuwa idadi ya watakaobaki iwe ndogo. Tatizo kubwa lipo kwa serikali na wanaopiga debe wamasai wahamishwe. Serikali imetumia mbinu za janja janja kukabiliana na hili jambo. Kwa nini itafute wamasai bandia waseme kuwa wamekubali kuhama? Kwa nini ''waandishi'' wa habari uchwara kama kina Kitenge walivalia njuga hili jambo kiasi cha kuhonga waandishi wengine eti wasapoti uhamaji? Hapo inatupeleka kwenye hofu kuu ya watu wengi: awamu hii ina elements za ufisadi na upigaji nyingi, je, kuna namna nyuma? Je, ni kweli kwamba kuna watu wanataka kupewa hayo maeneo na ndiyo wanashinikiza? All in all, hili jambo siyo kubwa kama inavyodhaniwa kama serikali ingetumia uwazi na ukweli kulishughulikuia.
Ila wanaopinga hawatoi hoja hizo, wanasema Wamasai hawatakiwi kuhamishwa sababu ni makazi yao walipewa

Hoja ingekuwa kuhusu mustakabali wa Ngorongoro baada ya Wamasai kuhamiswa, pengine tungekuwa na mjadala mzuri
 
Sasa mkuu jangwani utalinganisha na nchi yetu kweli? Raia watakaaje jangwani mwamba? Halafu Botswana ina karibia kuingia mara 2 kwenye nchi yetu!
Botswana 🇧🇼 ni jangwa?ila wametumia akili na mipango iliyosafi kujenga nchi yao, President Nyerere anasoma UK na President Khama naye amesoma UK, legacy gani wameziachia nchi zao?,Tanzania tunaongezeka kwa 3%to4%,Botswana wao ni 0.4%,maisha bora kwa raia wake
 
Botswana 🇧🇼 ni jangwa?
Mkuu umesoma Jografia ya shule ya msingi wewe? Unalijua jangwa la Kalahari? Ingia basi kwenye ramani ya Afrika uangalie!! Karibia mchi mzima ya Botswana imefunikwa na jangwa!
 
Wewe unachanganya madawa. Hiyo mifano unayotoa huko kwingine kote ni tofauti na Ngorongoro. Ngorongoro wanyama na binadamu wameishi pamoja kwa muda mrefu sana. Hilo eneo wamasai wamekuwepo kwa muda mrefu sawa na wanyama. Ni kweli kwamba wamasai wameongezeka idadi na hawawezi kuendelea kukaa pale wote milele. Utaratibu ufanywe wapewe elimu na wahamishwe kwa staha. Wakubaliane na serikali kuwa idadi ya watakaobaki iwe ndogo. Tatizo kubwa lipo kwa serikali na wanaopiga debe wamasai wahamishwe. Serikali imetumia mbinu za janja janja kukabiliana na hili jambo. Kwa nini itafute wamasai bandia waseme kuwa wamekubali kuhama? Kwa nini ''waandishi'' wa habari uchwara kama kina Kitenge walivalia njuga hili jambo kiasi cha kuhonga waandishi wengine eti wasapoti uhamaji? Hapo inatupeleka kwenye hofu kuu ya watu wengi: awamu hii ina elements za ufisadi na upigaji nyingi, je, kuna namna nyuma? Je, ni kweli kwamba kuna watu wanataka kupewa hayo maeneo na ndiyo wanashinikiza? All in all, hili jambo siyo kubwa kama inavyodhaniwa kama serikali ingetumia uwazi na ukweli kulishughulikuia.
Hata mi jambo la kuhamasisha wamasai sioni tatizo ila mbinu inayotumika ndo inatia mashaka ,ni kama wanaondolewa kwa nguvu ili wawekezaji wachukue maeneo ,na ikiwa ni hivo heri wamasai wabaki maana hamna tofauti unaondoa watu halafu unaingiza wengine kwa maslahi yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mi jambo la kuhamasisha wamasai sioni tatizo ila mbinu inayotumika ndo inatia mashaka ,ni kama wanaondolewa kwa nguvu ili wawekezaji wachukue maeneo ,na ikiwa ni hivo heri wamasai wabaki maana hamna tofauti unaondoa watu halafu unaingiza wengine kwa maslahi yako

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao watu wanaosema wamasai wataondolewa ili wapewe wawekezaji wana ushahidi wowote au ni hisia tu?
 
Back
Top Bottom