Pre GE2025 Msigwa: Mbowe aliacha tuliyomtuma Ikulu akaenda kushughulikia Billicanas. CHADEMA hakuna Sera ni kudandia mambo ya CCM tu!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nimeipenda hii
 
Wewe mbilikimo bila Chadema hao CCM wangekuonea wapi? Jaribu kuwa na shukrani,Chadema hii iliyokuokota jalalani hadi leo unajua kuvaa suti na kuendesha magari ndiyo unaitukana namna hii? Hivi ungeshinda uenyekiti Kanda ya Nyasa ungekuwa huko CCM? Jaribu kuweka akiba ya maneno ukijua kabisa kuwa huko CCM wewe ni wa kuja tu na hawajayasahau matusi yako kwao,wanakutumia tu for a while then wanakumwaga.
 

Attachments

  • FB_IMG_1719903155204.jpg
    51.5 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1719903252490.jpg
    26.2 KB · Views: 1
Msigwa alipokuwa mbunge aliwahi kumsifia Marehemu JPM lakini chama chake hakikumchulia hatua. Ajaribu kumsifia Lissu katika chama chake cha sasa aone itakavyopokelewa.

Msigwa alitofautiana na wenzake wa chama chake kwenye suala la kuhamishwa wamasai kutoka eneo la Ngorongoro lakini hakuchukuliwa hatua yeyote. Ajaribu kupinga hadharani suala la DPW aone kama atachukuliwa poa na chama chake kipya.

Msigwa anasema walimuagiza Mbowe akazungumzie mambo 10 Ikulu lakini alizungumzia mambo yake binafsi. Inabidi atuambie katika hayo mambo 10 yapi hayakuzungumziwa kwa sababu ya mambo ya Bilcana.
Msigwa ana haki ya kumsifu Mwenyekiti wake wa sasa kwa kuleta uhuru zaidi katika mambo ya siasa. Lakini anapaswa kutuambia nani alinyang'anya huo uhuru ili tusinyang'anywe tena huo uhuru.

Inaelekea kuwa kilichomtoa CDM ni kuhisi kuonewa na Mbowe na si kingine. Kama ni hivyo, hayuko katika siasa kutumikia wananchi bali kujitumikia yeye mwenyewe.

Amandla...
 
Msigwa kaamuabkutia akili MFUKONI
 
Angehama kama Mwenyekiti wa Kanda ingekuwa na impact kubwa sana kuliko ilivyo sasa. Inawezekana hilo ndilo lilikuwa lengo.

Amandla...
 
Msigwa akiendelea kuitungua CDM, basi 'Karma' itamuhukumu......kwa mujibu wa wakili msomi Pascal Mayalla
 
Hao mahiri uliwahi kuwataja walipokuwa CHADEMA?Au unasubiri kila atakayetoka ndiyo umuite mahiri?Tazama hii kiumbe!
 
Bado natafakari,kama kaweka mfukoni akili zake anazozitegemea kufikri,sijui anatumia nini kwa wakati huu.Amejidunisha kuliko uhalisia wa kujidunisha.The highest degree of self-degradation. Shame.
Naam, ni lugha ya picha, namaanisha reasoning capacity yake ilikuwa kubwa sana, but kwa sasa, ameacha ku reason na kujenga argument za kijinga dhidi bya chama chake Cha awali.
 
Jamani mtafutieni wilaya huyu Msigwa maana keshajimaliza kisiasa.
Ni sawa na mwanamke aliyekaa kwenye ndoa miaka ishirini na kuzalishwa watoto lkn siku akiondoka kwa mume anasema yule mume Hana nguvu za kiume.
Msigwa anajidhalilisha.
 
Mzee mwenzangu, huyu jamaa si alishatoka chadema? Nadhani awaache na utapeli wao. Ukiona umeachana na mke au mume ukaendelea kumuongelea au kumfuatilia, jua kuna jambo. Jitafakari.
 
Naam, ni lugha ya picha, namaanisha reasoning capacity yake ilikuwa kubwa sana, but kwa sasa, ameacha ku reason na kujenga argument za kijinga dhidi bya chama chake Cha awali.
Tupo pamoja.Huyu mtu kajidunisha mnooo mnooo!Bado namshangaa kuendelea kutumia kauli ya "akili ndogo haiwezi kuongoza akili kubwa"!Misemo yake na kauli zake kwa sasa akiitumia anaonesha alivyo kasuku,roboti la Nape na kiumbe wa kukaririkariri tu maneno.The emptiness within him!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…