Ni kweli, Dkt Magufuli alifikia kipindi alipungukiwa hekima sana ya utu, kiasi kwamba matendo yalitendeka na watu kuumia akawa siyo mfariji tena wa taifa. Unajua ukitaka kujua uchungu hebu mtu wako wa karibu apate matatizo nakuambia roho itauma, sasa sijui kwanini hata kupotea kwa Ben au Azory hakuweza hata kuzisaidia hizo familia kujua wapendwa wao wapo wapi, hata tukio la Lisu yeye alipaswa awe mfariji wa kwanza ila ndiyo hivyo wabaya wake wakautumia ukimya wake kumshushia mazigo ya lawama yote. Nadhani kwenye issue za mahusiano Dkt Kikwete will always remain the best president!