Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?

Kweli hapo kwa mashabiki wa Chadema hasa hawa wa huku JF, wengi akili zao zimeishia kuipinga CCM kwa kila jambo.

Wanajiona wao na chama chao ni malaika wasiokosea, kwao wenye makosa siku zote ni CCM, hivyo hata akitokea yeyote miongoni mwao akakosea, wanaona afadhali kukaa kimya kuliko kumkosoa, wana siasa fulani za kiuoga, kuviziana, zisizo na maana yoyote.

Hawa kama hawawezi kukosoana wenyewe ndani kwa ndani, wataweza vipi kuwakosoa wale walio nje ya nyumba yao? jaribio lolote la kufanya hivyo kwangu ni sawa na unafiki.
 
Lisu anapata kibri Kutoka Kwa wananchi tuliotoa maoni mbele ya Tume ya judge WARIOBA.

Haiwezekani viongozi wakae na kugawana madaraka kama KASHATA za kijiwe Cha kahawa.
Hivi hata swali lenyewe unalifahamu kweli?!
 

Tundu lissu sio mropokaji tu ila mlengo wake kisiasa hauna tija kwa maendeleo ya tanzania. Mtu muomini wa falsafa ya demokrasia ya kiliberali huku afrika atakua kibaraka tu wa maslahi ya nchi za magharibi. Kila kitu eti haki za binadamu haki zenyewe mtu kua shoga au msagaji. Ukileta kuhusu haki za uchumi wanakutolea nje. Halafu uhuru uhuru. Uhuru mtu kuhonga, uhuru majaji na wanasheria kuhongwa. Hakuna haki ni sheria inageuzwageuzwa mradi mwenye hela apewe haki. Hiyo hapana.
 
Mifano aliyoitoa Tundu Lisu ya ACT wazalendo 2015 na NCCR Mageuzi 2020 inadhoofisha kabisa dhamira yako ovu ya kufanya ghilba ili maneno yake yasieleweke, unajaribu kuwazongazonga wana jf Ujumbe wake usifike, neno "ya kijinga" ni neno la kistaarabu kabisa ikiwa wewe ni mwanasheria na unajua maana ya Taaluma yako, ungeweza kuandika vyema zaidi ya hili andiko lako hata kama Lisu ni mpinzani kwako bali na Mzalendo mwenzio na mdogo wako pia Ni Mwana taaluma Mwenzio. Kwa "MASLAHA YA TAIFA"
 

Lissu hawezi kuwa liability kokote maana anaweza kusimama mwenyewe na bado akawa asset, kuna namna fulani ukisimama na ukweli support inakufuata siku zote.

Mariziano was liability
 
Lissu ni Nyerere wa kizazi hiki
 
Pasco;
Huwezi kujua pengine labda Megawatts hizi anazoachia muda huu, zina uhusiano na lile tukio lake kule Dodoma Septemba 2017. Maana sasa hii siyo kawaida
 
Yupo sahihi na ndiyo hivyo watu wenye big brain hufikiri. Hivi kweli chama cha siasa kilichokomaa mnakubali kupewa wabunge, ???. Yaani kupewa,!kupewa! Ni mjinga aliyewekwa mfukoni ndiye anaweza kukubali
 
Pascal kuna mahala hujafanya proof reading, umeandika "Rais mama samia Alivyo mtu wa hiyana" ni makosa hasa
 
Sijaona kama swali ni baya unless wewe unataka kutengeneza hoja yako tofauti. Ameeleza ukweli na kuhoji hadhara kama ni sawa kukubali nusu mkate au la, jambo ambalo limekataliwa. Na huu ndiyo ushirikishaji watu waelimishwe baadaye waje waamue.
 
Sijaona kama swali ni baya unless wewe unataka kutengeneza hoja yako tofauti. Ameeleza ukweli na kuhoji hadhara kama ni sawa kukubali nusu mkate au la, jambo ambalo limekataliwa. Na huu ndiyo ushirikishaji watu waelimishwe baadaye waje waamue.
well said👍
 
Siasa zetu sometimes ni pasua kichwa.
 

Attachments

  • Screenshot_20230511-094724.jpg
    56.8 KB · Views: 7
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…