Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?

As long as umeona kuna haja kwake kutazama upya matumizi yake ya lugha kwenye uwasilishaji wa hoja zake, hapo ni sawa pia na kusema unaona amekosea kwa lugha aliyotumia.

Hata kwenye hayo mengine, kama ameongea na viongozi wenzake chamani akapata baraka ya kuropoka nje, kwangu haina shida, lakini kama ndio ameamua kujiropokea tu tofauti na msimamo wa chama chake, hapo shida ipo..

Hata hivyo, kiuhalisia, na kwa hali ilivyo, kama chama chake bado kipo kwenye maridhiano, halafu yeye anatoka nje na kuanza kuyaponda maridhiano..

Hapa maana yake huyu mtu ameamua kuwa mtukutu, mkaidi kwa chama chake, anayewaona wenzake wote waliopo kwenye maridhiano ni wajinga isipokuwa yeye pekee.

Huyu kwangu ni arrogant asiyestahili kusifiwa chochote anachoongea, bali aambiwe ukweli apunguze ujuaji.

Bahati mbaya wengi wenu humu ndani hamna uwezo huo wa kufanya hivyo, kwenu Lissu ni malaika aliyeshuka toka mbinguni asiyekosea!.

NB.

Hii mindset yenu yakuchukulia kila jambo lililoletwa na mtu wa CCM kama mtego, nakuishia kulitafutia sababu zozote mradi mumpinge, ndio inayowafanya wengi wenu mshindwe kuyaona matatizo ya viongozi wa Chadema pale mnapoambiwa, coz akili zenu mmezi set kupinga tu!.
 
Ana hoja. Kwanini wanasiasa wagawane majimbo? Opposition watakuwa na nguvu hapo? Huko sio kuwekwa mfukoni? Uchaguzi Mkuu wa gharama zote utakuwa na maana gani?
Lengo la kuwepo kwa opposition si linakuwa limeuawa na kuzikwa?
Na je sio kutatua matatizo temporarily kwa maslahi binafsi ya baadhi ya watu?
BTW Chadema na CCM, Kinana na Mbowe wanaridhiana nini?
Kwanini problems hazijatajwa hadi leo na solutions au suggestions towards solutions to those problems?
WANARIDHIANA NINI?
 
Kwahiyo ni ukweli kuwa mwenyekiti wake kwa kuingia maridhiano ni Mjinga?
Wajinga wapo , ni yule wa mbeya anayewaza ubunge wa kupewa na wewe, hajamtaja mkt.

Maridhiano yawe serious, Si mnaridhiana wao wanaendelea kuiba pesa za wananchi afu wanawaambia msiongee, mtaharibu maridhiano.

Watimize HOJA za upinzani zilizoandikwa kimaandishi.
 
Pascal Mayalla
Tundu Lissu yuko sahihi eidha anawapendeza au anawacjukiza wenzake.
1. Anazijua hila za ccm kuwa maridhiano ni danganya toto
2. Maridhiano ni mradi wa wachache na hayana hatima nzuri
3. Ametoa mifano hai jinsi ccm siku zote ni waongo hawastahili kuaminiwa pia kwa maridhiano.

Huu ndio ukweli mchungu, tunatakiwa tuwe wakweli daima.

NImekushangaa mno kwa kauliza zako zinazoonyesha woga na kujipendekeza kiasi cha kumsema Lissu kwa kauli hii hapa chini kwenye mabano👇👇👇👇👇


(Kwa sasa Tundu Lissu yupo nchini akifanya mikutano yake ya hadhara kwa uhuru, haku akiwa na ulinzi na usalama wa kutosha bila bugudha yoyote, tatizo lake ni lile lile moja, kuropoka!)
 
Kuna fukuto huko ndani na akitoswa sijui ataenda Kugombea chama gani Sasa..

Lisu asisahau kwamba Chadema iliwahi muuza Slaa na mambo yakaenda.
Humjui Lissu vizuri wewe.
Lissu sio fisadi wala mfia vyeo.
Hilo ni jeshi la mtu mmoja.

Ninamfahamu Lissu kabla hajaingia kwenye siasa, hajui kuogopa maisha
 
Maridhiano yamefanya yeye akarudi analopoka hivi kwa uhuru bila hivyo angeendelea kuishi kwa mabeberu na kuogopa kurudi nyumbani
 
Paskali Acha kuspin... Lisu kasema. "...... Kuna watu wanachekacheka, tuna akili...!?"

Hapo anauliza na pia amejiinclude. Hakuna mahali amewasema wenzake bila yeye kujijumuisha.
 
Kwani Kuna shida gani na maoni hayo?vita hii ni kubwa.Ccm Wana tapatapa ikiwezekana wawe Wana gawa wabunge na siyo uchaguzi Hali.Angalia Wana vyo ng'ang'ani akina Mdee
 
Ndugu yangu uko kwenye mkao wa kusubiri kupewa jimbo nini? Alichozungumza Lissu kina mantiki kubwa kabisa. Kwa kifupi kama hujui CCM wanataka kuwarubuni Chadema wakubali kuachiwa baadhi ya majimbo ili wasishinikize tena katiba mpya. Lissu anakataa huu utapeli. Kwa nini kusiwe na katiba mpya kwanza halafu wananchi wawe huru kuchagua viongozi wao?
 
Chama chochote makini kinaweza kikakubaliana katika lengo kuu lakini wanachama wakatofautiana namna ya kulifikia. Kwenye hili Chadema wameonyesha ukomavu mkubwa kwa kuruhusu tofauti zao zionekane wazi wazi. Hii nayo inaweza kuwa ni strategy ya kuwaonyesha upande wa pili kuwa ni heri wapatane na Mbowe maana kuna wakina Lissu ambao hawana uvumilivu wake.

Ndivyo ilivyokuwa Marekani. Wakati Martin Luther King anahubiri upendano upande wa pili alikuwepo Malcolm X aliyesema wazi kuwa chaguo kwa Marekani lilikuwa " the ballot or the bullet". Mbowe na Lissu wanaelewana. Juhudi za kuwachonganisha hazitafanikiwa.

Amandla...
 
Bado huwa napata taabu sana kuelewa kati ya mkweli na muongo ni yupi huwa wa maana kwa jamii !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…