Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?

Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?

Kuna mahali niliandika Lissu anaropoka mmoja wa wafuasi wake humu ndani akasema kudai Katiba Mpya, Tume Huru, na mengineyo sio kuropoka..

Sasa nimuulize ndugu mfuasi, Lissu anapouliza viongozi wenzake chamani kama wana akili huyu ana maana gani?

Simply huyu ni mjuaji anayetakiwa kuambiwa ukweli apunguze mihemko, awaheshimu viongozi wenzake, na kufuata taratibu za chama chake.
Inaonekana anapiga kwenye mshono
 
Ukiwauliza waliofanya naye kazi za siasa na taaluma watakuambia haya:-

-Mh.Tundu Lissu ni "mgobo"....
-Mh.Tundu Lissu ni "pwagazapwagaza"....
-Mh.Tundu Lissu ni "mjuaji mno"....
-Mh.Tundu Lissu ,HOJA ZAKE ,MAWAZO YAKE ,MISIMAMO YAKE ndiyo iliyo JUU na BORA kushinda ya wengine.......

Nachelea kusema kuwa "grandeur delusion" ni tatizo.......

Eeeee Mwenyezi Mungu tupe HEKIMA kwani ELIMU umeshatupatia ,aaaamin aaaamin[emoji120]

"Never give wisdom to unworthy because it's unfair to the knowledgeable".

#SiempreJMT[emoji120]

#TanzaniaIdumuDahari[emoji120]
Hoja inashindwa na Hoja iliyo bora shida yenu wadanganyika mnaamini katika Porojo
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa, zikijadili jambo lolote la kisiasa, kiuchumi na kijamii lenye maslahi kwa taifa letu. Makala hizi huwa na swali, kisha hoja, halafu jibu utalitoa wewe mwenyewe msomaji.

Makala ya leo ni kuhusu maendeleo ya siasa zetu kuelekea uchaguzi wa 2025.

Siku zote Tanzania tumekuwa na siasa za kuhasimiana kati ya Chama tawala CCM na vyama vya upinzani, Kiingereza tukiita ni politics of confrontations, siasa zikiendeshwa kwa uadui na kila aina ya figisu, na kwenye baadhi ya maeneo korofi, ushindi kupatikana kwa bao la mkono!.

Baada ya kutokea kilichotokea, ile Machi 17, Samia Suluhu Hassan, kaingia na kitu cha kwanza alichokifanya kwenye siasa zetu, ni kuliishi tuu jina lake la Suluhu kwa kuleta suluhu ya kisiasa kuachana na siasa za kuhasimiana na kuitroduce, politics of reconciliation and politics of tolerance kwa Samia kukubali kufanya mazungumzo ya maridhiano kati ya CCM chama tawala na Chadema, chama kikuu cha upinzani Tanzania, huku akiunda tume Prof Mukandala na kuwaweka vyama vyote kujadili mustakabali mwema wa nchi yetu.

Kwanza Mama alikaa na vyama vyote kupitia TCD pale Dodoma, katika mkutano huo, kuna chama kilisusa kisa kiongozi wake yuko korokoroni!. Sisi wa ushauri wa bure, tukashauri ... Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.

Kwenye mkutano huo wa TCD, waungwana wakamuombea mtu msamaha, Rais Mama Samia alivyo mtu wa hiyana, akajibu pale pale "kusameheana kupo", sisi wa kuandika, tukaandika ... Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye?

Na kweli haikupita punde mtu akaachiwa, na sisi wa kuandika tukapongeza... Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!

Mara ghafla nchi ikatulia, Chadema iliyokuwa hoi bin taaban kifedha mara ikapata pumzi, ikaanza kupumua, mara sasa ikawa na uwezo hata wa kuendesha vikao, viongozi wake mara ghafla wakawa na uwezo za kufanya ziara hadi za nje ya nchi, yote haya ni matunda ya maridhiano.

Wakati Rais Mama Samia akiyafanya haya, haimaanishi CCM wote walikuwa wanayafurahia, no, kuna wahafidhina wenye nguvu na ushawishi mkubwa ndani ya CCM, walimpinga Samia, hivyo Samia alishughulika nao wengine wale wenye kelele sana, ilimbidi kuwaondosha kuwaweka mbali kwa kuwapa majukumu mengine ya kiutendaji ili kuwafunga midomo!

Wahafidhina hawa pia walikuwepo Chadema, na mhafidhina Mkuu ni Tundu Lissu! Mama akafuata hadi Ubelgiji akamtuliza, ila hakuacha kuropoka!


Mimi Tundu Lissu nimesoma nae sekondari Ilboru, hivyo namfahamu sana, kwanza ni kichwa sana, very bright and brilliant, tatizo lake ni kuropoka!, Lissu ni mropokaji!.
Hivyo nimeisha andika mengi humu kumhusu Tundu Lissu miongoni mwake ni haya
Uropokaji kwa wanaharakati ni sifa muhimu sana haswa katika utetezi wa haki za binadamu. Hivyo katika harakati za mwanzo za vyama vingi, Chadema kilikuwa ni chama cha kiharakati hivyo wanaharakati kama kina Tundu Lissu, Dr. Wilbrod Slaa, Zitto Kabwe na wengine wengi kuwa ni asset muhimu sana kwa mapambano ya kudai haki.

Ni kufuatia uanaharakati wa Tundu Lissu, mimi ni miongoni mwa tulimshauri Tundu Lissu, ndie amkabili Magufuli uchaguzi wa 2020 Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli! hicho nilichokisema hapo kuwa Tundu Lissu ni zaidi ya Magufuli, ndicho kitakuja kuigharimu Chadema mbele ya safari.

Very unfortunately Lissu kikamtokea cha kumtokea, na kukimbilia nje ya nchi kutimizwa. Akiwa matibabuni, aliendelea kuropoka!, na kwa mambo aliyokuwa akiongea kuhusu Tanzania, mimi nilifika mahali, nikadhania Tundu Lissu hatarejea tena nchini Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela!

Kumbe Tundu Lissu ni very bold, akaomba kuhakikishiwa usalama wake ili arejee nyumbani, japo aliowaomba wamhakikishie usalama, walimkalia kimya, hawakumjujibu, ni akina sisi, ndio tulimmshauri arejee tuu hivyo hivyo na kweli akarejea Kamanda Lissu, Usisubiri Jibu la IGP Kuhusu Usalama Wako, Aliyekulinda na Shambulio Lile Yupo, Yeye Aweza, na Ataendelea Kukulinda, Welcome Back Home!

Moja ya sifa kubwa za pekee za Tundu Lissu, ni mkweli daima na kwenye ukweli, Lissu hana simile wala hakopeshi, hata ukweli huu kuhusu kilichotokea ndani ya Chadema, ni Lissu ndie aliyetoa Tundu Lissu kama JPM, ni mtu mkweli. Asema ukweli jinsi ukomo wa uongozi ulivyoyeyuka CHADEMA

Kwa sasa Tundu Lissu yupo nchini akifanya mikutano yake ya hadhara kwa uhuru, haku akiwa na ulinzi na usalama wa kutosha bila bugudha yoyote, tatizo lake ni lile lile moja, kuropoka!

Hebu msikilize hapa



Swali ni kwa hiki anachoongea hapa, Tundu Lissu, anauliza kama wenzake wana akili timamu kweli, unamjua huyo anayemuulizia kama ana akili kweli ni nani?. Kitendo cha kuyaita maridhiano kuwa ni ujinga, jee maridhiano ya CCM na Chadema ni ujinga?, hizi lugha Tundu Lissu anazotumia, jee ni lugha za kiungwana?, ni lugha za kistaarabu?

Kwa haya anayoyasema Lissu kutoa siri za maridhiano, je Lissu ni asset kwa Chadema, or kwa sasa, Tundu Lissu is liability?

Wasalaam

Paskali


Watu wenye tabia ya kujipendekeza na kuogopa maisha ndio huona lugha za Lisu ni uropokaji. Ikiwa unajiamini na hutegemei mbeleko huwezi kuogopa kusema ukweli.
 
Jemadari TUNDU LISSU ameendelea kuwaamsha Wananchi wa IGUGUNO SHAMBA ili wajitambue na kudai KATIBA MPYA pia amewaambia kuwa wanaibiwa Kodi na Tozo zao,
20230511_133455217.jpg
 
Maneno ya Lissu tusiyachukue kwa kumuangalia yeye na uchama wake wa CHADEMA bali katika hali halisi. Kimsingi Lissu hupo sawa kwa aslimia kubwa...CHADEMA kwasasa imekua assimilated na CCM jambo ambalo kwetu ni ushindi. Siasa zetu ni ngumu kwa kuzielewa ingawa ni rahisi kwa kuziangalia.
 
Kuna fukuto huko ndani na akitoswa sijui ataenda Kugombea chama gani Sasa..

Lisu asisahau kwamba Chadema iliwahi muuza Slaa na mambo yakaenda.
Lissu nguvu yake ni kubwa kuliko chadema kwa sasa,na aijua chadema nje ndani kwa sasa,cha maana chadema watakachofanya wakiona atawaharibia ni kum Chacha Wangwe tu kisha zigo kurushiwa CCM
 


Swali ni kwa hiki anachoongea hapa, Tundu Lissu, anauliza kama wenzake wana akili timamu kweli, unamjua huyo anayemuulizia kama ana akili kweli ni nani?. Kitendo cha kuyaita maridhiano kuwa ni ujinga, jee maridhiano ya CCM na Chadema ni ujinga?, hizi lugha Tundu Lissu anazotumia, jee ni lugha za kiungwana?, ni lugha za kistaarabu?

Kwa haya anayoyasema Lissu kutoa siri za maridhiano, je Lissu ni asset kwa Chadema, or kwa sasa, Tundu Lissu is liability?

Wasalaam

Paskali

Yupo very straight na sahihi kabisa.

Nikionacho hapa umeweka pembeni na rehani taaluma yako na kuamua kuvaa sare za Chama chako kuingia front kukipambania, sababu wewe unaona athari za mikutano ya Tundu Lissu kwa Chama chako, hivyo unataka kuvuruga kwa kuibua mijadala chonganishi.

Labda unisaidie, ni kiongozi gani wa CHADEMA uliyemsikia akitoa kauli za kuwa wamekubali kugawiwa majimbo? Maana anachofanya Lissu ni kushambulia kauli za namna hiyo, maana ni kweli kauli hizo zipo lakini hazitoki ndani ya CHADEMA ila waanzilishi wake ni nyie wenyewe ndani ya CCM.

Kuhusu maridhiano, binafsi sijawahi kuwasikia CHADEMA kama Chama wakitoa tamko la kuwa wameshafanya maridhiano, bali kuna mambo wameridhiana lakini hawajafika mwisho kwani vikao vya maridhiano vinaendelea, hata rais alikiri kuwa hata yeye anakumbana na vikwazo kutoka kwa wahafidhina ndani ya Chama lakini akatoa wito wayapokee maridhiano na waendelee kumpa muda wakati vikao vinaendelea.

katika hili, Pascal Mayalla unataka kutubeba ufala.
 
Mifano aliyoitoa Tundu Lisu ya ACT wazalendo 2015 na NCCR Mageuzi 2020 inadhoofisha kabisa dhamira yako ovu ya kufanya ghilba ili maneno yake yasieleweke, unajaribu kuwazongazonga wana jf Ujumbe wake usifike, neno "ya kijinga" ni neno la kistaarabu kabisa ikiwa wewe ni mwanasheria na unajua maana ya Taaluma yako, ungeweza kuandika vyema zaidi ya hili andiko lako hata kama Lisu ni mpinzani kwako bali na Mzalendo mwenzio na mdogo wako pia Ni Mwana taaluma Mwenzio. Kwa "MASLAHA YA TAIFA"
Nyerere alisema, "ujinga sio tusi", bali upumbavu.
 
Nitazungumzia moja tuu kwenye hoja zako paschal Mayalla
Kuombewa msamaha kwa Mbowe na Zitto hadharani kwenye ule mkutano una harufu zote za stage managed .
Ili kupata kukubaliwa na jumuia ya kimataifa ilibidi Mbowe atolewe kwenye kesi ya kubambikiziwa ikawa si Mbowe wala CDM walikuwa tayari kuomba msamaha ikabidi itumike plan B, enter Zuberi Kabwe Zito.
Ikawa convenient face saving formula na matunda yake tumeona ya mikopo,misaada,na mialiko nchi mbalimbali kitu hakikuwepo kwa hayati Mwendakuzimu.
Samia anajua kujishusha kwa faida ya wengi. Yupo diplomatic na mijadala inasaidia nchi kuliko yeye mwenyewe.
 
Swali ni kwa hiki anachoongea hapa, Tundu Lissu, anauliza kama wenzake wana akili timamu kweli, unamjua huyo anayemuulizia kama ana akili kweli ni nani?. Kitendo cha kuyaita maridhiano kuwa ni ujinga, jee maridhiano ya CCM na Chadema ni ujinga?, hizi lugha Tundu Lissu anazotumia, jee ni lugha za kiungwana?, ni lugha za kistaarabu?
Paskali, acha tafsiri ambayo hailingani na alichosema Lisu. Kwenye clip uliyoweka Lisu anatoa mifano ya waliopigwa changa la macho ktk chaguzi zilizopita na anasema itakuwa ni ujinga kuingia mtego ule ule. Hakuna mahali popote kwenye clip anasema maridhiano ni ujinga. Pili hatujaambiwa kwenye maridhiano wamekubaliana nini ili uweze ku-conclude kuwa Lisu anayaita ujinga.
 
Lissu nguvu yake ni kubwa kuliko chadema kwa sasa,na aijua chadema nje ndani kwa sasa,cha maana chadema watakachofanya wakiona atawaharibia ni kum Chacha Wangwe tu kisha zigo kurushiwa CCM

Hakuna chama cha upinzani kinaweza kufanya mauaji kwa mfuasi wake kisiingie hatiani. Chama tawala tu ndio huweza, maana ndio chenye maamuzi dhidi mamlaka za kiuchunguzi.
 
Jemadari Tundu Lissu akiendelea kuliamsha Taifa Mkoani Singida Kijiji cha Mtinko amesema tukienda kwenye Uchafuzi wa 2025 bila Katiba mpya TUMEKWISHA!.

KATIBA MPYA! KATIBA MPYA! KATIBA MPYA!

NO HATE NO FEAR.
20230511_162215187.jpg
 
Pamoja na kukubaliana nawe kuwepo kwa 'moderation' katika uwasilishaji wa habari/taarifa ili kutoonekana kubomoa zaidi kuliko kujenga kwa pamoja, nchi hii sasa imefikia mahali pa hovyo sana kutokana na kurembaremba na kupeana sifa zisizostahili mara nyingi, hasa kwa viongozi. 'Bruntness' na lugha ngumu, hata kama haipendezi kuisema, lakini ikiwa ndio ukweli ni sahihi kabisa sasa kusemwa hivyohivyo.

Kiongozi anaposhindwa kusema ukweli kwa kutumia lugha anayofikiri itawaudhi hao wanaosemwa, na badala yake analembalemba tu, kwa mfano :"kwani watazikwa na hizo mali wakifa"?; badala ya kuwa 'direct' kwamba wote watashughulikiwa kwa mjibu wa sheria; namna hii ya uwasilishaji ndiyo inayozidi kulemaza nchi.
Matumizi ya lugha inayotumika kwangu sio jambo kubwa sana, japo ni muhimu.

Kwangu ninachopigania ni kiongozi kufuata taratibu walizojiwekea, asiwepo mmoja akataka kujiweka juu ya wenzie chamani, kwamba iwe kama vile yeye ndie pekee mwenye mdomo wa kusema, basi ndio anasema popote, na chochote anachoamua.

Ukiwa kama kiongozi halafu unakwenda nje ya vikao vyenu unaanza kuwasema wenzio, tena mbaya zaidi mpaka kuuliza kama wana akili kweli, huu kwangu ni ujuaji wa kitoto uliovuka mipaka, kukosa hekima kabisa, ni kuropoka tu.
 
Kwangu ninachopigania ni kiongozi kufuata taratibu walizojiwekea, asiwepo mmoja akataka kujiweka juu ya wenzie chamani, kwamba iwe kama vile yeye ndie pekee mwenye mdomo wa kusema, basi anasema popote chochote.
Hili hatjui kama hivyo ndivyo.
Sijawasikia CHADEMA wenyewe wakilisemea hili kama unavyoliweka wewe.

Pamoja na kukubaliana na msingi wa hoja hiyo, kuna mengi ambayo bado tulioko huku nje ya chama hatuyajui.
Kwa mfano. Mbowe kama Mwenyekiti wa chama alitoa msimamo wake (sijui kama ulikuwa msimamo wa kushirikisha na wenzake kwenye chama), alipozungumzia habari za maridhiano kwa mara ya kwanza kabisa, kwenye ule mkutano wake kule na Diaspora; na kuurudia msimamo huo huo mara kadhaa sehemu nyinginezo; kama pale viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza.

Msimamo huo pia hatujasikia ukizungumziwa kwa uwazi ndani ya chama.

Kwa hivi karibuni kaamua kunyamaza, kamwachia Lissu naye aseme yake

Kwa hiyo, kwa upande wangu sijui kama unayoyasema wewe kuhusu haya yanayoendelea ndani ya chama ni kweli au siyo kweli. Hili sijui.
Lakini naunga mkono anayosema Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, labda arekebishe lugha tu kidogo ili isitumiwe na watu wasiokitakia chama hicho mema, kama inavyofanyika sasa hivi.
Tazama mada zote zilizowekwa hapa kumhusu Lissu na aliyoongea, zimeanzishwa na watu wa aina gani utajua Lissu kagusa waya hasa.
 
Back
Top Bottom