Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa, zikijadili jambo lolote la kisiasa, kiuchumi na kijamii lenye maslahi kwa taifa letu. Makala hizi huwa na swali, kisha hoja, halafu jibu utalitoa wewe mwenyewe msomaji.
Makala ya leo ni kuhusu maendeleo ya siasa zetu kuelekea uchaguzi wa 2025.
Siku zote Tanzania tumekuwa na siasa za kuhasimiana kati ya Chama tawala CCM na vyama vya upinzani, Kiingereza tukiita ni politics of confrontations, siasa zikiendeshwa kwa uadui na kila aina ya figisu, na kwenye baadhi ya maeneo korofi, ushindi kupatikana kwa bao la mkono!.
Baada ya kutokea kilichotokea, ile Machi 17, Samia Suluhu Hassan, kaingia na kitu cha kwanza alichokifanya kwenye siasa zetu, ni kuliishi tuu jina lake la Suluhu kwa kuleta suluhu ya kisiasa kuachana na siasa za kuhasimiana na kuitroduce, politics of reconciliation and politics of tolerance kwa Samia kukubali kufanya mazungumzo ya maridhiano kati ya CCM chama tawala na Chadema, chama kikuu cha upinzani Tanzania, huku akiunda tume Prof Mukandala na kuwaweka vyama vyote kujadili mustakabali mwema wa nchi yetu.
Kwanza Mama alikaa na vyama vyote kupitia TCD pale Dodoma, katika mkutano huo, kuna chama kilisusa kisa kiongozi wake yuko korokoroni!. Sisi wa ushauri wa bure, tukashauri ...
Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.
Kwenye mkutano huo wa TCD, waungwana wakamuombea mtu msamaha, Rais Mama Samia alivyo mtu mwenye wema wa asili,
Psychoanalysis Trends za Viongozi Wetu, Humbleness ya Rais Samia ni Bonafide Genuine, ni asili yake, ni nature yake, ndivyo alivyo, Ila...
, akajibu pale pale "kusameheana kupo", sisi wa kuandika, tukaandika ...
Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye?
Na kweli haikupita punde mtu akaachiwa, na sisi wa kuandika tukapongeza...
Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!
Mara ghafla nchi ikatulia, Chadema iliyokuwa hoi bin taaban kifedha mara ikapata pumzi, ikaanza kupumua, mara sasa ikawa na uwezo hata wa kuendesha vikao, viongozi wake mara ghafla wakawa na uwezo za kufanya ziara hadi za nje ya nchi, yote haya ni matunda ya maridhiano.
Wakati Rais Mama Samia akiyafanya haya, haimaanishi CCM wote walikuwa wanayafurahia, no, kuna wahafidhina wenye nguvu na ushawishi mkubwa ndani ya CCM, walimpinga Samia, hivyo Samia alishughulika nao wengine wale wenye kelele sana, ilimbidi kuwaondosha kuwaweka mbali kwa kuwapa majukumu mengine ya kiutendaji ili kuwafunga midomo!
Wahafidhina hawa pia walikuwepo Chadema, na miongoni mwa wahafidhina hawa wa Chadema ni M/Mwenyekiti, Mhe. Tundu Lissu!.
Mama Samia alipopita Ubelgiji, Tundu Lissu akachangamkia fursa ya kuonana na kufanya mazungumzo na Tundu Lissu, ila baada tuu ya mazungumzo baina ya Tundu Lissu na Samia, Tundu Lissu akaibuka na haya,
Mimi Tundu Lissu nimesoma nae sekondari Ilboru, hivyo namfahamu sana, kwanza ni kichwa sana, Tundu Lissu ni kichwa cha ukweli, very bright and brilliant, tatizo lake ni moja tuu, ambalo nimeisha lisema kwenye bandiko langu hili
Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!
Hivyo nimeisha andika mengi humu kumhusu Tundu Lissu miongoni mwake ni haya
Mtu kuwa vocal kwa wanaharakati ni sifa muhimu sana haswa katika utetezi wa haki za binadamu. Hivyo katika harakati za mwanzo za vyama vingi, Chadema kilikuwa ni chama cha kiharakati hivyo wanaharakati kama kina Tundu Lissu, Dr. Wilbrod Slaa, Zitto Kabwe na wengine wengi walikuwa very vocal hivyo kuwa ni asset muhimu sana kwa mapambano ya kudai haki.
Ni kufuatia uanaharakati wa Tundu Lissu, mimi ni miongoni mwa tulimshauri Tundu Lissu, ndie amkabili Magufuli uchaguzi wa 2020
Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli! hicho nilichokisema hapo kuwa Tundu Lissu ni zaidi ya Magufuli, kwenye nini, ndicho kitu kitakuja kuigharimu Chadema mbele ya safari!.
Mara tuu baada ya kumshauri Tundu Lissu amkabili Magufuli, ndipo like tukio la very unfortunately likamtokea Tundu Lissu kwa kushambuliwa na wasiojulikana, na kukimbizwa nje ya nchi kutibiwa. Akiwa matibabuni, aliendelea kuwa vocal, na kwa mambo aliyokuwa akiongea kuhusu Tanzania, mimi nilifika mahali, nikadhania Tundu Lissu hatarejea tena nchini
Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela!
Kumbe Tundu Lissu ni very bold, akaomba kuhakikishiwa usalama wake ili arejee nyumbani, japo aliowaomba wamhakikishie usalama, walimkalia kimya, hawakumjujibu, ni akina sisi, ndio tulimmshauri arejee tuu hivyo hivyo na kweli akarejea
Kamanda Lissu, Usisubiri Jibu la IGP Kuhusu Usalama Wako, Aliyekulinda na Shambulio Lile Yupo, Yeye Aweza, na Ataendelea Kukulinda, Welcome Back Home!
Moja ya sifa kubwa za pekee za Tundu Lissu, ni mkweli daima na kwenye ukweli, Lissu hana simile wala hakopeshi, hata ukweli huu kuhusu kilichotokea ndani ya Chadema, ni Lissu ndie aliyetoa
Tundu Lissu kama JPM, ni mtu mkweli. Asema ukweli jinsi ukomo wa uongozi ulivyoyeyuka CHADEMA
Kwa sasa Tundu Lissu yupo nchini akifanya mikutano yake ya hadhara kwa uhuru, huku akiwa na ulinzi na usalama wa kutosha bila bugudha yoyote, tatizo lake ni lile lile moja, he is very vocal!.
Hebu msikilize hapa
Swali ni kwa hiki anachoongea hapa, Tundu Lissu, sio kuwa ameanza kutoa siri za mazungumzo ya maridhiano kabla the public hatujatangaziwa rasmi na wana maridhiano wenyewe?!.
Kumbe kwenye mazungumzo ya maridhiano watu wameridhiana kugawana nusu mkate!. Nani alilijua hili?. Kumbe wameahidiana kuachiana majimbo!, nani alilijia hili?, kama sio Tundu Lissu kuyasema haya, akina sisi tungejuaje na mazungumzo ya maridhiano ni siri!. Asante Lissu kwa taarifa hii.
Kwa kawaida mazungumzo yoyote ya majadiliano au reconciliation hufanywa behind the camera with honest, truthfulness, trust na the spirit of a win win situation, hakuna mshindi, hakuna mshindwa. No any details za mazungumzo hayo hutolewa nje kwenye public domain kabla ya kufikia muafaka, wanaridhiana nini, but now through Tundu Lissu, the cat is out of basket, you can't hide anymore!, this is breach of trust!.
Lissu anazungumza kwa kutumia lugha kali!, anauliza kama wenzake wana akili timamu kweli, unamjua huyo anayemuulizia kama ana akili kweli ni nani?. Kitendo cha kuyaita maridhiano kuwa ni ujinga, jee maridhiano ya CCM na Chadema kweli ni ujinga?.
Hizi lugha za Tundu Lissu anazotumia, ambazo ni very vocal, jee ni lugha za kistaarabu na kiungwana?, mimi naziona kama zina ukakasi fulani, lakini sijui nyinyi wenzangu.
Hii sio mara yangu ya kwanza kuialert Chadema about the impending doom!, walipompokea Edward Lowassa, niliwaeleza kitu
Ujio wa Lowassa CHADEMA: Kuna kundi wamesusa, wanapanga kurejea CCM! japo nilibezwa, lakini la kutokea lilikuja kutokea, hivyo sitashangaa hata hapa nikibezwa, ila litakapotokea la kutokea, nitawakumbusha.
Kwa haya anayoyasema Lissu kutoa siri za maridhiano, je Lissu badi ni asset kwa Chadema, au kwa sasa, Tundu Lissu is liability?. Sisi waona mbali, kuna kitu hapa tunakiona kwa mbali, kisipokuwa handled with care, it's going to cost Chadema very dearly.
Wasalaam
Paskali