zimmerman
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 1,644
- 3,176
Kwa sababu pia hilo ndilo lengo kuu la kuweka hizo kanuni, wao wanaita "world order".Lakini sisi ndio tunawapa sababu. Kama Nyerere alivyosema, ni watu wenye akili chafu wanageuka kumwangalia mwanamke alievaa nusu uchi. Sasa kwa nini katika tawala zetu tunakuwa tumevaa nusu uchi? Tunaponyanyasa watu, tunapokuwa mafisadi wa kupokea rushwa kwenye mikataba, ni wazi tutawavutia hawa wakubwa kwa kuwa wanaona fursa katika namna ya ovyo ovyo tunavyoendesha nchi zetu. Unavaa nusu uchi halafu wanaume wenye akili chafu wakikufuata unalalamika, eboo!
Ni kama kucheza mchezo wa kubet ambao mshindi tayari anajulikana. Underlying algorithms zimepangwa zikapangika kumtengeneza mshindi fulani, yule aliyeziweka hizo kanuni. Well, watu wanaojihisi "kunyanyaswa" mara nyingi ndio wale ambao hawkuridhika na matokeo ya uchaguzi. Tulianza kusikia haya mambo ya rushwa kwenye mikataba mara tu baada ya Tanzania kuridhia matakwa ya free market economy maana wajanja walioweka hizo kanuni wanajua kucheza hiyo michezo ya freemarket.
Putin is not a fool.