Msimamo wa nchi za Afrika juu ya suala la Urusi na Ukraine ni jambo dogo sana linalopaswa kuongozwa na kanuni, sio maslahi ya nchi zetu

Msimamo wa nchi za Afrika juu ya suala la Urusi na Ukraine ni jambo dogo sana linalopaswa kuongozwa na kanuni, sio maslahi ya nchi zetu

Lakini sisi ndio tunawapa sababu. Kama Nyerere alivyosema, ni watu wenye akili chafu wanageuka kumwangalia mwanamke alievaa nusu uchi. Sasa kwa nini katika tawala zetu tunakuwa tumevaa nusu uchi? Tunaponyanyasa watu, tunapokuwa mafisadi wa kupokea rushwa kwenye mikataba, ni wazi tutawavutia hawa wakubwa kwa kuwa wanaona fursa katika namna ya ovyo ovyo tunavyoendesha nchi zetu. Unavaa nusu uchi halafu wanaume wenye akili chafu wakikufuata unalalamika, eboo!
Kwa sababu pia hilo ndilo lengo kuu la kuweka hizo kanuni, wao wanaita "world order".

Ni kama kucheza mchezo wa kubet ambao mshindi tayari anajulikana. Underlying algorithms zimepangwa zikapangika kumtengeneza mshindi fulani, yule aliyeziweka hizo kanuni. Well, watu wanaojihisi "kunyanyaswa" mara nyingi ndio wale ambao hawkuridhika na matokeo ya uchaguzi. Tulianza kusikia haya mambo ya rushwa kwenye mikataba mara tu baada ya Tanzania kuridhia matakwa ya free market economy maana wajanja walioweka hizo kanuni wanajua kucheza hiyo michezo ya freemarket.

Putin is not a fool.
 
Si ndio wanachokuambia kila siku na kufundisha watoto darasani, mzee mimi ndio nina mtindio au wao...
Kaka soma Minsk Agreement uje hapa bhana achana na longolongo za BBC, Washington Post.
Kwa hiyo Misnky Agreement sijui inasema Zelensky akikiuka makubaliano Urusi ina haki ya kuvamia Ukraine na kuchukua sehemu za Ukraine, sivyo?
 
Kwa sababu pia hilo ndilo lengo kuu la kuweka hizo kanuni, wao wanaita "world order".

Ni kama kucheza mchezo wa kubet ambao mshindi tayari anajulikana. Underlying algorithms zimepangwa zikapangika kumtengeneza mshindi fulani, yule aliyeziweka hizo kanuni. Well, watu wanaojihisi "kunyanyaswa" mara nyingi ndio wale ambao hawkuridhika na matokeo ya uchaguzi. Tulianza kusikia haya mambo ya rushwa kwenye mikataba mara tu baada ya Tanzania kuridhia matakwa ya free market economy maana wajanja walioweka hizo kanuni wanajua kucheza hiyo michezo ya freemarket.

Putin is not a fool.
I say, wewe sikuwezi. Kama hiyo ndio reasoning yako, mbona imbombo ilipo na pijo na lori na mafikifiki!
 
Hapa hatupo kuangalia uzuri wa Putin au Zelenshhy. It does not matter maka raisi wa Urusi ni Lenin au Putin au Gorbachev, na yule wa Ukraine ni Zelenckky au sijui nani. Ndio maana nikasema ni suala la kanuni. Sasa kama huelewi maana ya kanuni, au principles kwa kiingereza, basi kaa kimya. Kaongeze elimu.
Kasome Minsk Agreement, signatory akiwa Angel Merkel.
Sign out.
 
Kwa sababu pia hilo ndilo lengo kuu la kuweka hizo kanuni, wao wanaita "world order".

Ni kama kucheza mchezo wa kubet ambao mshindi tayari anajulikana. Underlying algorithms zimepangwa zikapangika kumtengeneza mshindi fulani, yule aliyeziweka hizo kanuni. Well, watu wanaojihisi "kunyanyaswa" mara nyingi ndio wale ambao hawkuridhika na matokeo ya uchaguzi. Tulianza kusikia haya mambo ya rushwa kwenye mikataba mara tu baada ya Tanzania kuridhia matakwa ya free market economy maana wajanja walioweka hizo kanuni wanajua kucheza hiyo michezo ya freemarket.

Putin is not a fool.
Putin sio mjinga mwambie huyo, Putin ni Smart President ila huyu dogo hawezi elewa
 
Si ndio wanachokuambia kila siku na kufundisha watoto darasani, mzee mimi ndio nina mtindio au wao...
Kaka soma Minsk Agreement uje hapa bhana achana na longolongo za BBC, Washington Post.
Sioni dalili za kuwa nabishana na mtu mwenye uwezo wa kusoma Washington Post au kusikiliza BBC hapa.
 
Sioni dalili za kuwa nabishana na mtu mwenye uwezo wa kusoma Washington Post au kusikiliza BBC hapa.
Haile Sellasie UN speech ya mwaka 1963 alikuambia matatizo hayataisha, je yatatulika kwa amani, constitutionally or by force
 
Kasome Minsk Agreement, signatory akiwa Angel Merkel.
Sign out.
Hebu ona sasa. Angel Merkel akiwa signatory wa Minsk Agreement, maana yake nini?. Wanasheria wasije wakasoma hii post yako watapendekeza ukimbizwe haopitali fulani.
 
Tuna matatizo yetu,wana matatizo yao. Unaingilia vita vya urusi wakati hujamalizana na vita vya TANESCO wakati huko kwao daraja linavunjwa leo linajengwa kesho na umeme upo hata nchi ikiwa vitani.
 
Haile Sellasie UN speech ya mwaka 1963 alikuambia matatizo hayataisha, je yatatulika kwa amani, constitutionally or by force
Una quote vitu ambavyo ni very irrelevant. Sasa quote ya Haile Sellasie kuhusu kutatua mambo kwa kutumia consitution inaingiaje kwenye mgogoro wa Urusi na Ukraine? Unajua maana ya constitution? Constitution ipi utatumia kusuluhisha suala la Urusi na Ukraine.

Usifiche ujinga wako kwa kutumia maneno ya kiingereza unayookota mahali fulani fulani. I can see right through your statements kwamba huna uwezo wa kujadili hii thread. Sio ligi yako, kaa pembeni
 
Hebu ona sasa. Angel Merkel akiwa signatory wa Minsk Agreement, maana yake nini?. Wanasheria wasije wakasoma hii post yako watapendekeza ukimbizwe haopitali fulani.
Dah mkuu, nimekosea njia endelea na watu wako.
 
Putin sio mjinga mwambie huyo, Putin ni Smart President ila huyu dogo hawezi elewa
Anaelewa sema tu anafikiri WYSWI. What You See is What it Is. Mataifa makubwa hayaishi hivyo, vita inapiganwa kwenye ulimwengu wa fikra kwanza kabla ya kudhihirika kwa mabomu na missiles na machine guns. Battle of ideas haina na wala haieshimu mipaka ya kijiografia. Marekani anafanya nini Taiwan?
 
Una quote vitu ambavyo ni very irrelevant. Sasa quote ya Haile Sellasie kuhusu kutatua mambo kwa kutumia consitution inaingiaje kwenye mgogoro wa Urusi na Ukraine? Unajua maana ya constitution? Constitution ipi utatumia kusuluhisha suala la Urusi na Ukraine.

Usifiche ujinga wako kwa kutumia maneno ya kiingereza unayookota mahali fulani fulani. I can see right through your statements kwamba huna uwezo wa kujadili hii thread. Sio ligi yako, kaa pembeni
Mzee matatizo kama yakitokea kuna njia nyingi za kuyatatua na hizo ni njia mojawapo kama huzijui uliza, Mgogoro wetu na Malawi kuhusiana na Ziwa Nyasa unajua walitumia njia gani kuutatua?
 
Hii post imeandikwa vizuri na ukishawishika tu kwa namna tu ilivyo pangiliwa basi huna budi kushawishika. Ila mimi bado sijaweza kushawishika hata.

Kwa sababu mgogoro wa Urusi vs Ukraine ni tofauti sana na migogoro ya weusi na wazungu wakati wa S. Africa Apatheid, ni tofauti na mgogoro wa Biafra huko Nigeria, ni tofauti sana na mlinganisho ulioufanya wa wamasai wa Kenya vs wamasai wa Tanzania kwamba kama si sawa kwa Tanzania kuivamia kenya kukomboa wamasai wa Kajiado basi haiwezi kuwa sawa Urusi kuivamia Ukraine.

Ndiyo si sawa kwa Urusi kuivamia Ukraine iwapo tu utaisoma historia ya Urusi na Ukraines kuanzia mwaka 2022 vita ilipoanza. Ila huu mgogoro ni zaidi ya Urusi kuivamia Ukraine kwa lengo la "land grab" kama wamagharibi wanavyoubrand kwenye media. Lakini je makubaliano ya Urusi na NATO kuhusu usalama wa Urusi ilikuwa miaka ya 1990? Ilikuwa kwamba, yeah Urusi ipo radhi kuachia zile nchi zilizokuwa chini ya USSR "baltic states" kuwa huru lakini asingependa kuona zinakuwa militarized states armed with western weapons zinazotishia usalama wa Urusi yenyewe. Hapo ni baada ya figisu za Marekani kuhakikisha USSR inavunjika. Lakini nini kilichotokea baadaye? NATO kwa ulevi wao wa pesa wakazidi kuzimega nchi zilizokuwa sehemu ya USSR, na Putin akawa akiwacheki na kujesemea moyoni hiiii! Miaka ya 2000 minongono ilipoanza kwamba hata Ukraine ikikaa sawa kwenye mambo yake ya ndani ya kisiasa inaweza kujiunga na NATO Urusi ikasema sasa baasi.

Kwa background hii complicated sasa sisi waafrika tulaani nini hapa kati ya Ukraine na Mrusi? Sera ya kutofungamana na upande wowote ni sera baab kubwa kwenye situation kama hii.
Wewe unaongea ya kwako. Siyo aliyoyasema Putin. Putin alitamka wazi kuwa anafanya operation maalum ya kijeshi nchini Ukraine ili kuwakomboa wananchi wa Ukraine wanaotengwa na kuonewa na itawala wa Ukraine kwa sababu ya asili yao, na hao ni wale wanaoongea Kirusi.
 
Unadhani mambo ni black.and white kama unavyotaka yawe? Katika mgogoro kati ya Israeli na Palestina principle inasemaje na Marekani yupo upande upi? Kama tukifata kanuni na basics, kanuni ni kutofungamana na upande wowote kwenye migogoro isiyotuhusu. Nyerere alijihusisha sana kwenye migogoro inayotuhusu.

Of course hakuna kiongozi wa Tanzania ya sasa mwenye calibre ya Nyerere lakini walau kwenye hili la Ukraine na Mrusi - aidha kwa woga au kwa sababu zinginezo -- wapo sahihi kutojihusisha kwenye mgogoro usiotuhusu.
Hiyo tafsiri yako, ni tafsiri potofu kuhusiana na 'Kutofungamana na Upande wowote".

Tuliposema hatufungamani na upande wowote haikumaanisha kuwa hatuna upande kati ya uovu na usahihi. Hatusimami katikati ya uovu na wema, bali tulimaanisha kuwa tunasimama katika ukweli bila ya kujaali kama ukweli huo itakuwa kinyume cha Magharibi au Mashariki. Tunapotoa msimamo wetu tunalalia katika ukweli na siyo kusimama katika maamuzi ya blocks zile mbili, yaani ya Mashariki (chini ya Urusi) au ya Magharibi (chini ya Marekani). Na kwenye hilo Nyerere aliliishi.
 
Hao NATO Us-led walivyovamia LIBYA na kumtoa Ghadafi ni haki? Siwalaumu viongozi wa Africa kuwa kimya ni vyema wakakaa kimya kwa sababu hata kipindi cha Nyerere Waziri Mkuu Kawawa, tulikuwa Non Allied, unalikumbuka hilo?
Ghadafi kumwua kila aliyehoja matendo ya Serikali yake ilikuwa haki. Kuwakamata waliokuwa wanahoji utawala wake, kuwapeleka magerezani, halafu baadaye kwenda kuwakusanya na kuwazika kwenye makaburi ya pamoja, ilikuwa ni haki?

Baada ya kifo cha Gadafi, Walibya wamepitoa magumu mengi, lakini kwa nini ukienda Libya, pamoja na hayo magumu yote, hakuna anayemlilia Gadafi?

Kutofingamana na Upande wowote kumve wengi hamwelewi hata maana yake.

Kumbukeni wakati wa kipindi cha vita baridi, ukiwa katika kwenye block mojawapo ilikuwa huwezi kutoa msimamo wako pekee yako, ni lazima ufuate msimamo wa block. Nyerere alilikataa hilo alitaka asifungwe na block. Kama uovu umefanywa na block ya Magharibi, awe huru kuusema. Halikadhalika kama umefanywa na Mashariki, auseme pia. Hakumaanisha kutofungamana na upabde wowote, kati ya ukweli na unafiki, kama tunavyofanya sasa.
 
Nimeshasema, Afrika tulipaswa kulaani kwa nguvu zote uvamizi wa USA na NATO wa Libya, Iraq nk. lakini tutakuwa wajinga na walevi ikiwa hatutalaani uvamizi wa Urusi kwa Ukraine kwa kuwa USA nao walivamia Libya na Iraq. Na kama unasema tusiwalaani Urusi kwa sababu hiyo na wewe ni mjinpa kama hao viongozi wa Afrika kama kina Malema. Hamjui mnachokisema. Jirani yako atakupa lift kwenda Kariakoo, na hilo litafanya umtetee au usilaani matendo yake ya kunajisi watoto mtaani kwako siku akikamatwa kwa hilo kosa, au ukiona amenajisi mtoto wa mtu ambae huko nyuma nae alinajisi mtoto wa mtu mwingine. Sasa huo ni mtindio wa ubongo
Huwezi kulaani azimio la UN. Kuivamia Iraq lilikuwa azimio la UN, sawa na sisi tulivyovamia visiwa vya Anjwani, lilikuwa azimio la AU. Sadam alikuwa anawaua Washia, tena mpaka kwa sumu.

Gadafi alikuwa kiongozi muuaji. Hakuna aliyeukosoa utawala wake aliyeishi. Dun8a haihitaji viongpzi wa namna hiyo. Tinahitaji Dunia iliyostaarabika.

Labda tuilaumu Marekani kwa nini haifanyi hivyo hivyo kwa mataifa ya Afrika, maana mengi yana tawala zinazokaribia kwa ubaya na hizo zilizokuwa za Iraq na Libya.
 
Back
Top Bottom