Msimamo wa Rais Samia kuhusu demokrasia ya kisiasa, fujo za kisiasa na fujo za kidini: Tutaelewana tu!

Wanazo hoja ni kweli.
Lakini, ni hoja gani ambayo haijajibiwa hadi sasa?
Ilete hapa tuidadavue.
Hoja tumezijibu kijumla jumla sana..

Zuio la mikutano ya kisiasa ni takwa la kisheria au la mtu binafsi?

Katiba mpya isubiri tunajenga uchumi..lini tutaacha kujenga uchumi na kuliangalia sasa jambo la Katiba?

Maandamano ya kumpongeza Mwenyekiti wetu kutimiza siku 100 madarakani ni sawa ila makongamano ya wenzetu si sawa?

Naogopa sana maana naiona hiyo siku ikifika wajukuu zetu wakihoji tulikuwa wapi kama wananchi hadi kukubali kukaa na shida ya maji,matundu ya vyoo,madarasa chini ya mti kwa miaka zaidi ya 50..?
 
Naona kuna jambo unalifahamu lakini nikukumbushe kwa vile umelisahau.

Ukichukua Katiba ya Chama cha siasa kama vile Chadema utaona vikao vya maamuzi. Kuna
  1. Mikutano mikuu kila mwaka, kila wilaya, kila kata, kila kijiji, kila kitongoji
  2. Kamati za utendaji kila baada ya miezi mitatu, katika kila wilaya, kila kata, kila kijiji, kila kitongoji
  3. Sekretarieti zinazokutana kila siku katika kila Kanda, kila mkoa, kila wilaya, kila kata, kila kijiji, kila kitongoji.
Mfano, kuna:
  1. Mkutano mkuu Taifa
  2. Baraza la Mashauriano Kanda
  3. Baraza la Mashauriano Mkoa,
  4. Mkutano Mkuu wilaya
  5. Mkutano mkuu kata
  6. mkutano mkuu kijiji
  7. mkutano mkuu kitongoji
Mikutano kama hii imetamkwa kikatiba kwa ajili ya mabaraza ya chama, yaani
  1. Bavicha
  2. Bawacha
  3. Bazecha
Mikutano hii ndiyo inaweka, kutekeleza na kusimamia utekelezaji wa mipango ya chama,
Mikutano hii, kwa mujibu wa Rais Samia haina kizuiz, isipokuwa kizuizi cha uchumi dhaifu wa kukifanya chama kushindwa kukusanya wajumbe.

Tanzania kuna mikoa 26, wilaya 160+, Kata zaidi ya 6000, vijiji zaidi ya 12,000 na vitongoji kibao. Kwa hiyo, kuna vikao vingi vya kukiruhusu chama cha siasa kusonga mbele.

Bila shaka sasa umeelewa somo la Rais Samia.
 

SWALI: Zuio la mikutano ya kisiasa ni takwa la kisheria au la mtu binafsi?

Jibu: Ni takwa la kisheria. Soma vizuri ibara ya 14 ya emergency powers act. Hii ndiyo inatumika kusimamisha baadhi ya vifungu vya Katiba katika vita dhidi ya UVIKO19

SWALI: Katiba mpya isubiri tunajenga uchumi..lini tutaacha kujenga uchumi na kuliangalia sasa jambo la Katiba?

Jibu: Swali la LINI linapaswa kujibiwa na andiko la kiserikali. Unalifahamu andiko hilo? Kama halipo, maana yake ni kwamba hicho sio kipaumbele cha kitaifa bado. Ushawishi na utetezi wa dhana uendelee kufanyika hadi hapo upande wa pili utakapoona kwamba hapa hatuwezi kuendelea kuziba masikio. Siasa za fujo hapana.

SWALI: Maandamano ya kumpongeza Mwenyekiti wetu kutimiza siku 100 madarakani ni sawa ila makongamano ya wenzetu si sawa?

Jibu: Soma vizuri ibara ya 14 ya emergency powers act. Haki zote zinagawanyika mara nne. Kuna claim rights, liberty rights, power rights, immunity rights. Lakini, Rais wa ncho anayo power right ya kutengua baadhi ya haki za baadhi ya vyama vya siasa na baadhi ya raia. Hilo ni gumu kueleweka.

SWALI: Naogopa sana maana naiona hiyo siku ikifika wajukuu zetu wakihoji tulikuwa wapi kama wananchi hadi kukubali kukaa na shida ya maji,matundu ya vyoo, madarasa chini ya mti kwa miaka zaidi ya 50?

Jibu: Endelea kujenga hoja zenye mashiko. Siasa za fujo hapana.
 
Kwenye hiyohiyo mikutano tumeshuhudia baadhi ya wanachama wa CHADEMA wamewekwa rumande wengine wametoka leo
 
Kwenye hiyohiyo mikutano tumeshuhudia baadhi ya wanachama wa CHADEMA wamewekwa rumande wengine wametoka leo
Hizo ama ni isolated cases au transitional cases kwa sababu maalum.
Mfano, ukitangaza kuwa unakusudia kunyoa mav*zi mkuu wa nchi maana yake ni kwamba umejipanga kufanya siasa za fujo.
Na kiusalama, mikutano ya ndani ni hatari kuliko mikutano ya hadhara.
Kwa hiyo, utapekuliwa pekuliwa tu.
Hili nalo gumu kueleweka?
 
Tukiachana na hayo mengine lakini Tanzania bado tunahitaji mazingira sawa ya kufanya siasa kushindwana kwa hoja sio wenye madaraka kutumia vyombo vya dola ili waendelee kubaki kwenye nafasi zao na kiukweli kuwa na upinzani ni afya kwa Demokrasia pia hata maendeleo
 
Nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa, halafu nakuuliza swali. Wakati Dr Slaa na Katibu Mkuu wa CDM uliona mapambana kati ya CDM na dola kama sasa? Tafakari juu sababu zake.
 
Hizi ni nadharia za kishuleshule, kwenye uhalisia utakwama sana. Mambo haya ndio yanapelekea wasomi wengi kuishia kuajiriwa, au kuwa matajiri uchwara.
Theory-Action-Review cycle haikwepeki kama unataka kufanya siasa za kitaifa.
Na theory maana yake ni yale yote uliyoyapata shuleni.
No short cut
 

Mkuu naweza kukubaliana na wewe.

Lakini what about CCM ?

iT IS THE WORST OF ALL
 
Mkuu naweza kukubaliana na wewe.

Lakini what about CCM ?

iT IS THE WORST OF ALL
Usihitimishe haraka hivyo.
Weka vigezo huru mezani kuhusu utayari wa vyama vya siasa kuendesha nchi, tufanye objective scoring.
Utashangaa kwamba bado CCM inaibuka kidedea.
 
Nashukuru kwa maelezo haya..kwa mwendo huu bado huoni dai la Katiba ni hoja ya msingi sana?

Ikiwa Mkuu wa Nchi amepewa mamlaka makubwa hivi na huyo Mkuu pia ni Mwanasiasa na Mwenyekiti wa Chama huoni hatatenda usawa kwa Wanasiasa wengine wataokuwa mlengo tofauti na yeye(wao)?

Hapa ndipo wenzetu wanapojenga hoja kwa mifano ya wazi na sisi tukashindwa kuijibu badala yake tukaminya mrija wa hewa ili wapinzani wakose hewa wademke demke..
 
Sawa. Kuna mawili hapo:
1. Umuhimu wa Katiba Mpya
2. Uharaka wa Katiba Mpya

Ushahidi gani unahitajika kwa kila kipengele?

1. Kazi za Wariona na Kisanga ni ushahidi wa kipengele cha kwanza
2. Kipengele cha pili hakina ushahidi hadi sasa, japo Chadema wanakiuma uma midomo tu na kulazimisha kipaumbele cha Chadema kiwe ndio kipamumbele cha Serikali ya CCM.

Mambo hayaendi hivyo.

Tuweke nguvu ya hoja katika kipengele cha pili, cha kwanza kinaeleweka na kukubalika.
 
Nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa, halafu nakuuliza swali. Wakati Dr Slaa na Katibu Mkuu wa CDM uliona mapambana kati ya CDM na dola kama sasa? Tafakari juu sababu zake.
Ukweli ulio wazi siasa za kipindi kile mtu kama Dkt.Slaa angekuwa anazifanya sasa sijui kama angekuwa bado anahema..

Wapinzani ni wale wale wanasubiria tuteleze wapate pa kujengea hoja lakini sisi tumekumbwa na ugonjwa wa kukosa uvumilivu hili ndiyo ninaloliona likitusumbua sasa hivi..

Tusilazimishe wanaotupinga waje soft soft,watakuja wakali na sisi tunapaswa kuwavumilia..

WANASIASA WANAPENDA MADARAKA LAKINI HAWAPENDI SIASA..
 
Unawasilisha nini? Huu UPUUZI WAKO? Upuuzi wako beba peleka lumumba.
 
Mpuuzi kweli wewe!!! Mfumo wa vyama vingi nchini upo kwa miaka 30 sasa ndiyo miongo mitatu sasa ya chaguzi ambazo hazikuwa huru na za haki lakini bado huoni uharaka wa kuwa na Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi. Kwa ufinyu wako wa akili labda tusubiri miaka mingine 30 huku genge la wahuni wa maccm wakiendeleza udhalimu na dhuluma zao kwenye kila chaguzi ikiwemo wizi na mauaji ili kuendelea kung’ang’ania madarakani.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…