Msimamo wa Rais Samia kuhusu demokrasia ya kisiasa, fujo za kisiasa na fujo za kidini: Tutaelewana tu!

2.Uharaka wa Katiba..
Tupo kwenye kipindi ambacho ili tuijenge nchi basi tunahitaji mawazo kinzani na ya kwetu chama tawala,sasa mianya iliyopo kwenye katiba ya sasa inatupa uwezo mkubwa sana hata tusitake wapinzani waseme mawazo yao kinzani..rejea zuio la mikutano ya kisiasa,rejea uwiano wa wabunge wa upinzani bungeni na wa chama tawala,tazama bungeni upitishwaji wa miswada,vifungu vya kisheria spika anasema " wanaopinga waseme hapana,wanaokubali waseme ndiyo" imetupelekea leo tunahaha kuelezea kuhusu hizi TOZO..

Tupo kwenye kipindi mtu anaweza kukausha tu mifuko ya hifadhi na kuamua kuzifanyia pesa jambo jingine bila kushauriana na mtu..

Mimi kama mwana CCM natamani kuiona hali hii na nyingine kama hizi ziondoshwe na wala tusitegemee mbeleko za mapungufu ya Katiba ili tuendelee kuwepo madarakani..
 
Bila ya shaka una utindio wa ubongo. Wahi Mirembe kabla hujaanza kuokota makopo barabarani.
Wewe kama huna mtindio wa ubongo mbona ulirudia darasa la saba, kina Dionise wa CBE wakakuacha nyuma unajivuta kama konokono?
 
Mwenye mamlaka ya kumtangaza na kumwakikishia mgombea Urais kuwa ameshinda kwa mujibu wa sheria ni tume ya Taifa ya uchaguzi.CCM ni tume ya uchaguzi ya Taifa hadi itangaze matokeo?


Hizo kura "halali" za ushindi unazozizungumzia ni zipi hizo wakati CCM walipora uchaguzi nchi nzima?Siku hizi wizi wa kura unaitwa ni kura halali?Kuiba kura siyo fujo za kisiasa?

 

Swali: Mwenye mamlaka ya kumtangaza na kumwakikishia mgombea Urais kuwa ameshinda kwa mujibu wa sheria ni tume ya Taifa ya uchaguzi.CCM ni tume ya uchaguzi ya Taifa hadi itangaze matokeo?

Jibu: Naona huna uzoefu na siasa za uchaguzi. Kanuni ya kwanza ya kujiongezea kura ni kuwaaminisha wapiga kura kwamba utashinda, hata kama tayari unaona maji yako shingoni. Kama hili hulifahamu achana na mjadala huu.

Swali: Hizo kura "halali" za ushindi unazozizungumzia ni zipi hizo, wakati CCM walipora uchaguzi nchi nzima? Siku hizi wizi wa kura unaitwa ni kura halali?Kuiba kura siyo fujo za kisiasa?

Jibu: Maneno kwamba "wakati CCM walipora uchaguzi nchi nzima" yanahitaji ushahidi wenye hadhi ya kisheria kuyathibitisha. Mpaka leo jambo hilo limeshindikana. Hata hao kina Mdee pichani pale Bungeni juzi wameadhibiwa kwa kutolewa Bungeni kwa wiki kadhaa kwa sababu ya kushindwa kuyathibitisha ndani ya Bunge. Ukituhumu ni juu yako kuthibitisha. Ukishindwa kuthibitisha unafuta kauli na kulamba adhabu yako.

Mwisho, kumbuka haya mawili:

1. Sheria ya Usalama wa Taifa (1996) ilitungwa na wabunge wote wakiwemo wa upinzani. Wakatoa mamlaka kwa TISS kufanya "covert operations" pale ambapo kuna sababu za kiusalama kufanya hivyo. Sheria hiyo haisemi kuwa "covert operations" hazitafanyika kwenye uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

2. Chadema waliandika Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 wakasema kuwa wataiweka nchi rehani kwa kutumia madini kama dhamana ya mikopo ya kimataifa.

Ukishindwa kulipa mkopo nchi inachukuliwa na mkopeshaji. Kwa maoni yangu, hii ingekuwa sababu nzuri ya kiusalama kuifanya TISS kuchukua hatua zinazofaa kuichinjia baharini Chadema.

Mtu yeyote anayejua kazi za secret service atakwambia hivyo. Hata hivyo, sijui kwa uhakika kilichotokewa katika uchaguzi wa 2020. Utafiti unaoratibiwa na Ngurumo uendelee, labda utatupa majibu sahihi katika siku za usoni.
 
Samia hakuhakikishia wapiga kura kuwa atashinda ila aliwaambia kuwa anaenda kuunda serikali hata kama watu watachagua upinzani.
Mihimili yote mitatu ilishiriki katika kuisaidia CCM katika kupora uchaguzi.Huwezi kwenda kulalamika kwa mtu ambae ndiye amekuibia kura.Huwezi kwenda kuomba haki yako ya kisheria kwa yuleyule ambae ameshiriki kukuibia haki hiyo.
Sasa kwa nini hiyo unayoiita TISS haikuchinjia chadema baharini?Haijui wajibu wake?Tuna taasisi ambazo hazijui wajibu wake?Tuna taasisi ambazo zinaendeshwa kutokana na mtu alivyoamka siku hiyo na mke wake badala ya taasisi kuendeshwa kwa mujibu wa sheria?

Kama walizembea katika hili ni mangapi mpaka sasa hivi watakuwa wamezembea?Hii inaonyesha kuwa tuna taasisi tasa ambazo muda wowote zinaweza kuuza nchi yetu,na huu ndiyo mfumo ambao CCM imetengeneza kwa miaka yake 60 ya kuongoza nchi hii.Ni muda muafaka sasa CCM kukaa pembeni ili ituachie nchi yetu tuweze kuindesha kwa mujibu wa sheria.
 
Hiyo ni hoja nyingine kabisa. Itakayotegemea utashi wa mtu binafsi.

Magufuli aliteua wapinzani kwenye serikali yake. Matokeo yake mkabeza kwamba hao anaowateua ni makanjanja.

Kule Zanzibar nadhani hilo takwa la kushirikishwa kwa vyama vingine kwenye serikali lipo kwenye katiba yao. Sidhani kama kuna impact yoyote positive tangu huo utaratibu uanze kule Zanzibar zaidi ya "kutuliza" wapinzani kwa style ya "tule wote".

Hapa kwetu kama hicho ndicho mnachokitaka baada ya kugundua hakuna namna nyingine yoyote halali au haramu ya kuifanya CCM iachie madaraka basi mseme tena mseme kwa uwazi.

Kwamba "...na sisi wapinzani tunataka kula keki ya taifa mtushirikishe katika kula."

Ila mkianza kuleta pretense zenu kwamba mnapambania maslahi ya watanzania kwa ujumla hivyo muachwe mfanye kila mnachokitaka kwa uhuru sidhani kama uhuru huo mtaupata.

Duniani hakuna kitu kama hicho.
 
Uongo ni jadi yako mpuuzi wewe hunijui sikujui na sijawahi kurudia darasa la lolote lile na wala sijawahi kutia mguu CBE. Ná huyo dionise sijawahi hata kumsikia masikioni mwangu. Muongo mkubwa wewe. Umeshindwa hoja sasa unaleta viroja na kutunga uzushi.
Wewe kama huna mtindio wa ubongo mbona ulirudia darasa la saba, kina Dionise wa CBE wakakuacha nyuma unajivuta kama konokono?
 
No comment. Nothing to discuss. The thread is empty and heavily biased.
 

Tunashukuru kuwa umetuonyesha kuwa kweli ulienda shule. Kwa sisi mambumbu, mfano wa sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingetusaidia zaidi kuelewa hoja yako.

Aidha, haujafafanua kwa vipi haki ya mtu baki inaathirika kwa chama kufanya mikutano ya hadhara na kuandamana. Sijawahi kusikia Chadema wakilazimisha watu kuhudhuria mikutano yao lakini kuna mifano mingi ya vyuo na shule kufungwa ili wanafunzi na walimu wakahadhurie mikutano ya hadhara ya viongozi wa serikali. Kwangu mimi hii ni kuingilia haki yao ya msingi ya kupata elimu katika muda uliowekwa. Tumeshuhudia barabara zikifungwa ili viongozi wa serikali wapate nafasi ya kutoa hotuba bila kujali kuwa kuna watu baki ambao wana safari zao muhimu. Sijawahi kusikia ikifanyika hivyo kwa ajili ya mikutano ya Chadema au chama kingine cha upinzani. Hapa guilty party ni huyo unaemtetea.

Sijawahi kusikia Chadema wamezuia serikali kutekeleza programu zao za maendeleo. On the contrary, nimesikia viongozi wa serikali na chama chao wakisema waziwazi kuwa watazito katika programu zao za maendeleo sehemu zote zitakazopigia kura vyama vya upinzani pamoja na kuwa kodi zao zinachangia katika kufanikisha hayo maendeleo. Hapa tena, you are barking up the wrong tree.

Amandla...
 
Mh!!! Mama Amon!!!!
 
madhara ya kua na watu mjengoni ambao kiuhalisia walitakiwa kua jikoni wakikatakata vitunguu ni kama haya.
 
Kazi ya siasa ni mdomo.
Kazi ya chama cha upinzani ni kuangalia mapungufu ya chama tawala na kuyaanika,Kazi ya chama tawala ni kujibu hoja za Wapinzani.
Uwezo wa ccm kujibu hoja ulishakufa,tegemeo lao ni kuwahaidi teuzi baada ya kustaafu wakuu wa police Ili wawasaidie kuzijibu hoja za Wapinzani.
 
SIASA za FUJO zimeanzishwa na CCM Kwa KUSHIRIKIANA NA Polisi CCM ingeendesha Siasa kwa HAKI hakuna Chama kingeleta FUJO
Kwanini CCM ivizuie VYAMA vingine VISIFANYE SIASA lakini CcM ifanye? Viongozi wa CCM wanazunguka Nchi nzima Wanafanya SIASA wapinzani Wakifanya hata MIKUTANO ya NDANI wanakamatwa kwanini Kusiwe na SIASA ZA FUJO?
Tufike Mahali CCM ikubali Vyama vyote Vina HAKI sawa ya KUFANYA MIKUTANO na POLISI Waache Kuwakamata na Kuwanyima Dhamana Watuhumiwa na Walio Wengi Wanaonewa.

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Mpuuzi kweli wewe!!! Huna hoja sasa unaleta viroja sikujui hunijui acha kuandika uongo kutaka kulazimisha unanijua. Upuuzi wako beba peleka lumumba humu tutakuchapa za uso.
Tulia sindano ikuingie!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…