Mbao za nini kwenye kujenga msingi, kwanini zege lisianze chini kabla ya kuanza tofari?
Gharama zingine hizi zinaepukika!
Halafu fundi huyo ushauri wake ni wa kipigaji, asikabidhiwe fedha kwenda kununua vifaa, fuata mwenyewe.
Pia zunguka maeneo wanayofyatua tofari waweza kupata tofari kwa bei nafuu, hiyo mbona ghali sana?
Halafu material zote isipokuwa mchanga na tofari, usikubali kwenda kuvinunua kwa mkupuo, nunua nusu nusu ili vifaa visibaki, hapo tathimini yako itaenda vizuri.
Hadi pale ujenzi utakapo kamilika utakuwa umeokoa gharama kubwa sana katika bajeti hiyo.
Ningelipata scatch map ya nyumba yako kwa vipimo kamili, ningelikupigia mahesabu sahihi ya mahitaji ya nondo, saruji na matofari.
Nakazia tena usimpe hela fundi kwenda kwenye manunuzi, nenda mwenyewe,hata mkeo usimtume.
Kabla ya kujiridhisha kuanza kununua, zunguka kwanza kwenye maduka mbalimbali ya vifaa vya ujenzi kuhakiki bei ya bidhaa zile zile ulizopanga kununua.
Lazima utakuta kuna maduka mengine yana bei taafifu, ndiyo ufungue pochi.
Ukifanya hivyo laki3, laki nne zitaokolewa hapo.