Msingi tu 3.5M? Au Kuna namna napigwa wakuu

Msingi tu 3.5M? Au Kuna namna napigwa wakuu

Nyumba ipo Dar ya vyumba vitatu kimoja self, jiko, Sebule, dining na public toilet hii ndo bajet ya msingi fundi wangu kanitumia ila nahisi Kuna namna ananipiga au wataalamu hii mnaionaje
Umepigwa mzee ,unajenga wapi ?

USSR
 
Nyumba ipo Dar ya vyumba vitatu kimoja self, jiko, Sebule, dining na public toilet hii ndo bajet ya msingi fundi wangu kanitumia ila nahisi Kuna namna ananipiga au wataalamu hii mnaionaje
Ukisimamia mwenyewe na vifaa unanunua mwenyewe bei unaweza kupunguza hapo

Mimi msingi nimetumia 2.8m na kila kitu nimekisimamia mwenyewe

Tofari za msingi nimetumia pcs 800 na nilinunua kwa 920 tshs kila tofari

Pesa imekuja kutembea sana kwenye kufunga mkanda maana msingi wangu ulikuwa na nguzo karibia 6 so nondo zimetembea karibia 15

Cement kwenye mkanda imetembea mifuko 9 maana nilitaka iwe kali na kokoto za kutosha
 
Nyumba ipo Dar ya vyumba vitatu kimoja self, jiko, Sebule, dining na public toilet hii ndo bajet ya msingi fundi wangu kanitumia ila nahisi Kuna namna ananipiga au wataalamu hii mnaionaje
Vitu vingine jitahidi kuangaika ukavipata kwa bei rahisi

Cement nilinunua nyati mfuko mmoja kwa 15000
Kokoto nilinunua gari moja kwa laki 2 zile nyeupe zimeingia kwenye mkanda,zimeingia kwenye shimo la choo na zimebakia kwenye kufunga linta zinapungiza gharama kuliko kununua viroba

Loli la mchanga linachezaga kwenye 250 mpaka 270

Kama una uwezo wa kuvuta bomba ili upate maji itakuwa good sana kuliko kununua kila siku ni gharama sana

Pipa la kukodi nilipo nilikodishwa kwa buku 2 nilizama kwa wapangaji wakanikodisha

Nodno niliambiwa za mm 12 huku nilipo bei nilipata kwa 19000

Mbao za kukodi huku nilipo ni 1500 na nilifanikiwa hapa hapa jamaa aliniuzia nyingine za kununua kwa 7500 kila moja
 
Hiyo bajeti haitoboi ndugu yangu,
Nondo 15!!!!
Kokoto - viroba..???
TAFAKARI UPYA
 
Back
Top Bottom