King Kong III
Platinum Member
- Oct 15, 2010
- 64,227
- 98,761
Nyumba ni msingi ,ukileta ubahili kwenye msingi umeua nyumba.Nyumba ipo Dar ya vyumba vitatu kimoja self, jiko, Sebule, dining na public toilet hii ndo bajet ya msingi fundi wangu kanitumia ila nahisi Kuna namna ananipiga au wataalamu hii mnaionaje
Yalinikuta na mimi mwisho wa mwaka jana tu.Hizi gharama za kindezi wakat najenga nilijikuta imefik 4M yaan pesa nje na maesabu
Kabisa, msingi imara sidhani kama unaweza kuapatikana kwa tofali za Tzs 1,000.hapo kwenye tofat atakua kachukua mepesi na iyo ni atari
Yaan iyo ni lazimaYalinikuta na mimi mwisho wa mwaka jana tu.
Tumeenda site na fundi baada ya kuandika kila kitu na ujira wake ikaja 3.2.
Ila mpaka kuja kumaliza msingi, ilikwenda mpaka karibia na 3.8m.
Beam aanze chini kabla ya kuanza kupanga tofari.mkuu beam inashikiliwa na nini kama sio mbao?
Dah, mkuu ukishachimba msingi, mwaga jamvi zikiambatana na nondo msingini chini kabisa mwanzoni. Zege hilo litashikiliwa na ukuta wa ardhi siyo mbao.mkuu beam inashikiliwa na nini kama sio mbao?
Hivi wale wanaoa za kupanga tofali kwenye msingi alafu wanakuja kumwaga beam juu ya tofali hii inakuwaje kiutalaamDah, mkuu ukishachimba msingi, mwaga jamvi zikiambatana na nondo msingini chini kabisa mwanzoni. Zege hilo litashikiliwa na ukuta wa ardhi siyo mbao.
Ni maamuzi yanayotokana na aina ya udongo.Hivi wale wanaoa za kupanga tofali kwenye msingi alafu wanakuja kumwaga beam juu ya tofali hii inakuwaje kiutalaam
Weka pesa hiyo kwenye mtaji pesa yote hiyo unaweka kwenye ujenzi na unalia!? Izungushe hiyo pesa ndani ya 3 years utakuwa na more than 30 million utanunua nyumba au kujenga sehemu nzuri zaidi. Sijui nani katuroga tunawazaga kujenga tu.Nyumba ipo Dar ya vyumba vitatu kimoja self, jiko, Sebule, dining na public toilet hii ndo bajet ya msingi fundi wangu kanitumia ila nahisi Kuna namna ananipiga au wataalamu hii mnaionaje
kwahiyo wewe huweki bean ya kutenganisha tofali za msingi na tofali za kuta za nyumba sio unasimamisha moja kwa mojaDah, mkuu ukishachimba msingi, mwaga jamvi zikiambatana na nondo msingini chini kabisa mwanzoni. Zege hilo litashikiliwa na ukuta wa ardhi siyo mbao.
Mkuu haukufunga mkanda?Leta Ubahili kwenye msingi utaziba nyufa mpaka uchoke kama mimi, mpaka nimeamua niachane nazo
View attachment 3288081
Mbona bei ya kawaida sanaaMbao za nini kwenye kujenga msingi, kwanini zege lisianze chini kabla ya kuanza tofari?
Gharama zingine hizi zinaepukika!
Halafu fundi huyo ushauri wake ni wa kipigaji, asikabidhiwe fedha kwenda kununua vifaa, fuata mwenyewe.
Pia zunguka maeneo wanayofyatua tofari waweza kupata tofari kwa bei nafuu, hiyo mbona ghali sana?
Halafu material zote isipokuwa mchanga na tofari, usikubali kwenda kuvinunua kwa mkupuo, nunua nusu nusu ili vifaa visibaki, hapo tathimini yako itaenda vizuri.
Hadi pale ujenzi utakapo kamilika utakuwa umeokoa gharama kubwa sana katika bajeti hiyo.
Ningelipata scatch map ya nyumba yako kwa vipimo kamili, ningelikupigia mahesabu sahihi ya mahitaji ya nondo, saruji na matofari.
Nakazia tena usimpe hela fundi kwenda kwenye manunuzi, nenda mwenyewe,hata mkeo usimtume.
Kabla ya kujiridhisha kuanza kununua, zunguka kwanza kwenye maduka mbalimbali ya vifaa vya ujenzi kuhakiki bei ya bidhaa zile zile ulizopanga kununua.
Lazima utakuta kuna maduka mengine yana bei taafifu, ndiyo ufungue pochi.
Ukifanya hivyo laki3, laki nne zitaokolewa hapo.
Mkuu ukiachana na gharama za ufundi, kuna vitu hapo akisimamia mwenyewe kindaki ndaki, vinapungua!Mbo
Mbona bei ya kawaida sanaa
Yaan ya ufundi kaandika 450000/???
Usipojenga utaishi poriniWeka pesa hiyo kwenye mtaji pesa yote hiyo unaweka kwenye ujenzi na unalia!? Izungushe hiyo pesa ndani ya 3 years utakuwa na more than 30 million utanunua nyumba au kujenga sehemu nzuri zaidi. Sijui nani katuroga tunawazaga kujenga tu.
Kwenye budget ya fundi, ongeza million ya kukulinda maana anytime iyo ela itaongezekaNyumba ipo Dar ya vyumba vitatu kimoja self, jiko, Sebule, dining na public toilet hii ndo bajet ya msingi fundi wangu kanitumia ila nahisi Kuna namna ananipiga au wataalamu hii mnaionaje
Labda kama Kuna slope ni sawa hizo tofali 1300Naona hakuna kipigo hapo ila wasiwasi wangu kwenye tofali za msingi, hivi zinakuwa na ratio SAWA na za ukuta......!