Msishangae Diamond siku baba yake akifa akaandaa mazishi ya kifahari

Hiyo familia ni mfano mzuri wa kuigwa
 
Pamoja na yote ila uwezi kuweka bifu na mzazi hata kama kafanya nini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo chanzo ni mama diamond na hivi anakibenten hawez ruhusu diamond asamehe nadhani yuko radhi amwage radhi maana mapato yakula na kibenten itabid yagawiwe na mzee
 
Mkuu uneona eh, halaf shida inaanzia hapa, wajua kama mama uliemweka mwanao tumboni miezi tisa, hutapebda kuja ona mwanao anatumbukia kwenye makundi ya hovyo, angalia diamond anavyobadili wanawake kama nguo na mama yake yuko okay kabisa kalipokea bila tatizo unadhani atakua anamshauri vitu gani ukute pia pengine anatamani msaidia babaye lakini mama mtu hataki kusikia hizo ishu
 
Kuna mambo ni ya aibu kufanywa na mzazi tena haswa mama, kuolewa ni vizuri lakini aelewe ukishaolewa unakwenda kwa mumeo hung'ang'anii kwa mtoto as if hujaolewa alipaswa aondoke ampe mtoto nafas na yeye kutengeneza future na maisha yake hiyo ya kumbana matumizi anaingilia mambo yasiomhusu
Hapo chanzo ni mama diamond na hivi anakibenten hawez ruhusu diamond asamehe nadhani yuko radhi amwage radhi maana mapato yakula na kibenten itabid yagawiwe na mzee
 
Baba ni baba haijalishi ubaya wowote alokufanyia,mzazi atabaki kua mzazi wako tu pengine kama si baba ake kukytana na mama ake diamond unadhani angekua nani au wapi??
ni kweli baba ni baba,lkn kumbuka kuitwa baba haina maana ule uwezo tu wakumpa mwanamke mimba,la hasha.
ubaba unaanzia pale kiumbe kinapotungwa,mahusiano mazuri ya baba na mtt ni tangu mtt akiwa tumboni,baada ya hapo pia ujue mtt anakula nn anavaa nn na mahitaji mengine muhimu kwa makuzi yake!
kama ishu ni kumpa tu mama mimba mbona hata mnyama anauwezo huo...what matters ni Kutimiza majukumu kama baba
 
Mi nikifa watu wasilie hela za mchango wanunue bia watu walewe wakatike kiduku mpaka asubuhi.
 
Okay fine baba yake alimtelekeza akiwa bado hajaweza kujisumamia mwenyewe na mama ake akasimama kikike akakua akawa star akawa hivi, ni kweli pengine bila mama ake asingefija alipo leo hii!! Angalia anayoyafanya mama yake sasa hivi? Wajuaje kipindi hio alisababisha huu mpasuko? Ye diamond amsaidie tu atende tu wema bas nafsi itamsuta huyo baba kwa aliyoyafanya lakini mama mtu kasimama kidete hatak
 
Ni kweli inabidi ifike point wamuangalie yule baba kwa jicho la 3,alikosea na nina amini amejutia,palipobakia ni kumkumbuka hata kwa kidogo nadhani nafsi yake itamsuta na atapata fundisho pia,anatia huruma yule baba
 
Kwangu mimi na kwamtazamo tu yule baba ni mstaarabu na laiti diamond angefunguka angemtafuta na wakayamaliza hata kama ni kumsaidia amsaidie ishu niliyoina sana kwa baba ni fursa ya kutowaona hata wajukuu. Mjukuu ni zaid ya mtoto.mzaz anatokeaga kumpenda mjukuu kuliko hta mtoto mwenyewe. Mama diamond sio mstaraabu na ukweli uliopo anguko la d litatokana na mama. Mimi nilitarajia mama angekuwa kemeo kwa mwanae kuhusu kesi za wanawake lkn sitashangaa mama ndo akawa chanzo cha mahusiano ya d kuvunjika.
 
Ni kweli inabidi ifike point wamuangalie yule baba kwa jicho la 3,alikosea na nina amini amejutia,palipobakia ni kumkumbuka hata kwa kidogo nadhani nafsi yake itamsuta na atapata fundisho pia,anatia huruma yule baba
Kwa mtizamo na kwa ninavyowajua wabawake wa kiha na yule mama nasikia anatokea eneo na zito kuna koo flani ya kiha inaitwa bhachabha ambapo mwanamke siku zote huwa anataka kumcontrol mwanauwme. Mama diamond atakuwa chanzo cha mengi. Ila baba avumilie tu d atakuja tambua tu ampe muda
 
Kuna jamaa yangu kaamua kuachana na mwanamke wake, kaamua kuachana na mtoto, hatoi huduma wala chochote kaamua kuanza maisha mapya kaoa mke mwingine na ana mimba

Hayo yote ni baada ya kuchoshwa na mbilinge, fedheha, dharau na mambo kedekede ya mke wake ambayo tumeyasuhudia

Na si kwamba hampendi mtoto lakini amepima kati ya kuendelea kuwa karibu na familia yake akaja kuishia pabaya ama kujitenga kipi afadhali

Kesho na keshokutwa mtoto bila kujua sababu ni nini na baada ya kulishwa sumu na mama yake atakuja kumchukia baba yake

Mimi binafsi sijawahi kuhukumu kwa haraka mababa wenye kadhia kama ya baba yake na diamond ni mpaka ujue sababu
Hakuna kichaa atatelekeza tu watoto bila sababu ya msingi labda awe karogwa

Kwa akili ya mama diamond huwa nafikiri huenda yeye ndio alikuwa sababu

Kuna wengi hasa vijana ambao bado ndoa kwao ni msamiati hawaelewi haya mambo

Mheshimiwa Makonda alizua sekeseke la kusaka baba waliotelekeza watoto wao, nafikiri kwa asilimia kubwa tulijionea aina ya wanawake waliojitokeza

Mwanamke anaongea mpaka mic inalowa mate
 
Kwa maana mzee akidedi asishoboke kwenye mazishi yake.

,,kama ambavyo amshobokei akiwa hai,,.
Ushauri wangu..
Chibu amsamehe mzee..
Hata yy anakosea..
Hata mungu tunamkosea lkn tukimuomba anatusamehe...
Mondi msamehe mzee ameshatubu,,mungu atahukumu kwa haki,,


Sent using Jamii Forums mobile app
 
familia zetu za kitz zina siri nyingi sana kwa kweli
 
Sijawahi kusikia "mazishi ya kifahari" kwa Waislam.

Halafu nakushauri kuwa wachana na mambo ya kufatilia ya watu, huyajuwi. Wewe fata yako na familia yako. Ya Diamond na familia yake yatakusaidia nini?

Unajuwaje nani atatangulia?
Wachana = acha
Kufatilia = kufuatilia
Huyajuwi = huyajui
Unajuwaje = unajuaje

"Huko shule ulienda kusomea ujinga?"
 
huyo jamaa anakosea kumtelekeza mtoto. Shahawa si zake yaan lait ningekuwa mimi afe paka afe nyanj mtoto nabeba.eti niachane na mwanamke kwa ukorofi wake niache mtoto haha shahawa zangu hazilali nje ya nyumba hata kama inakunguni zitalala tu na hapa ndo tunapokesaea wanaume tulio wengi sisi tunaona solution ni kumtelekeza na mtoto. Kama umeshindwana na mama unategemea huyo mtoto atakuwaje si ndo mwanzo wa kuwa kina anti john na mama akashangilia tu ilimradi kinaingia mdomoni tuu
 
Mkuu, mimi nilizaa na mwanamke nje ya ndoa ( kabla ya ndoa) na nikawa namuhudumia sasa kuna kipindi niliyumba kiuchumi akawa ananikasirikia ikafikia kipindi anatafuta sababu ya kugombana na mimi ili nimwambie tuachane, na nikimwambia hivyo tu atasema na nikae nikijua kwao sina mtoto

Nikamuuliza mtoto akikua akikuuliza Baba yake alipo utamjibu nini, akajibu nitamwambia "Kafa"

Na sasa hivi nimeoa ndo najua kwa nini baadhi ya wazazi wanaamua kukimbia nyumbani

Huyu ninaishi nae hapa nikimwambia ntakutimua urudi kwenu ananijibu "humu utaondoka wewe utaniachia nyumba mimi na mwanangu"

Wakati mwingine wake zetu ndo vichomi na tutakapoamua kuachana nao wanawapa sumu watoto ili sisi Kinababa tuonekane hatufai
 
Umeona eh, hapo ilika amsaidie tu sis wenyewe tuna mabaya tukianza kuhukumiana kwa hivi dunia haitakua sehem salama ya kuishi
Ni kweli inabidi ifike point wamuangalie yule baba kwa jicho la 3,alikosea na nina amini amejutia,palipobakia ni kumkumbuka hata kwa kidogo nadhani nafsi yake itamsuta na atapata fundisho pia,anatia huruma yule baba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…