Msishangae Makonda akiteuliwa na kurudishwa serikalini au kwenye chama

Msishangae Makonda akiteuliwa na kurudishwa serikalini au kwenye chama

Makonda alitakiwa awe mahakamani au jela na sio kwingine popote. Kwa kweli adui UJINGA bado yupo sana Tanzania. Yaani mtu aliyetajwa hadi na mabeberu kuwa anahusika kuua watu lakini bado anajitokeza mtu mjinga na kutaka eti awe kiongozi mkubwa wa chama tawala. Mwenyekiti wa CCM sio wa CHADEMA kwamba amteue mtu aliyewahi kuchafuka kiasi kile. CHADEMA peke yao ndo wanaweza kumwita mtu fisadi kwa miaka 10 halafu wakamteua kuwa mgombea wao wa urais.

Punguza unafiki , CHADEMA inaingiaje hapo?
 
Kama wamelenga kura za washamba wasukuma kwa kumteua Dotto Biteko wamechemka.Dotto hana ushawishi wowote na isitoshe wanasena ni mtutsi yule CCM wajipange

Mimi nashangaa wanaosema dotto ataleta kura za Kanda ya Ziwa. Nashangaa Sana. Kanda ya Ziwa sio malofa wa kubebwa Kama magunia. Nadhani ataleta kura za Geita pekee yake.
 
Kwa hali inavyoendelea Kwa Sasa ni vyema CCM tukajitafakari. Ukweli ni kwamba hatuna watu wenye 'energy' ya kutosha, hatuna mtu ambae anaushawishi Kwa wananchi si tu Kwa muonekano ata Kwa kuongea. Nimetafakari upande wa Serikali mawaziri wetu wamekosa nguvu na ushawishi Kwa wananchi.

Kuirudisha CCM kwenye mstari, nashauri Dr Nchimbi tumpe kijiti Cha Katibu Mkuu CCM, Paul Makonda apewe Uenezi wa chama.

Kwenye Serikali, tunafahamu Doto Biteko kateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu kama mkakati wa kuvuna kura za Kanda ya ziwa 2024 na 2025. Hili wazo kama ni la kweli basi halitafanikiwa sababu Biteko Hana ushawishi wowote katika Mikoa ya Kanda ya ziwa.

Ili kuleta mvuto mpya CCM Kanda ya Ziwa ni Bora Mzee Kalemani angeteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu kuliko huyo Biteko ambae hadi Sasa kishapoteana.

Kazi iendeleee!!
The Genge ….huyo Dotto hawatoshi? kiongozi wenu ni KALEMANI
 
Kanda ziwa, bila Luhaga Mpina wala wasijihangaishe.
Kwanini hakuongea chochote kwenye sakata la bandari? Yeyote yule tunayemfaham mwenye mawazo chanya kwenye nchi yetu lkn hakuongea chochote au hakupaza sauti na huku tulimwihutaji afanye hivyo lazima tuwe na wasiwasi na yeye.
 
Kwanini hakuongea chochote kwenye sakata la bandari? Yeyote yule tunayemfaham mwenye mawazo chanya kwenye nchi yetu lkn hakuongea chochote au hakupaza sauti na huku tulimwihutaji afanye hivyo lazima tuwe na wasiwasi na yeye.
Alishazungumza mbona kitambo sana kwenye space za maria sarungi....anyway Biteko yeye kasemaje kuhusu bandari?
 
Toka majuzi kumekuwa na milio kutoka pande mbalimbali kuwa Mh.Makonda anatakiwa kurudishwa kwenye system kwasababu kuna mambo mengi yanamhitaji yeye.

Wengine hili tuliliona toka mwaka 2022 kuwa kuna gap anahitajika Mh.Makonda ili turudi kwenye siasa tulizozizoea na ambazo zilikuwa zinakipa chama uhai miaka yote.

Tambueni akirudi huyo upinzani kazi wanayo 2025. Ile ngumu mliyoipata kipindi cha Kinana na Nape kinarudi tena.
Screenshot_20231020-090148_Instagram.jpg
 
Kwa nini Ben Mkapa wakati wa kampeni aliitwa Mr.Clean?Ndani ya siasa ukiweka mtu mwenye do (na huyu uliyemtaja ana madoa) ni kama umejiweka kwenye spotlight.
Kwa niniBenson Kigaila wa Chadema amepoa?TAFAKARI
 
Hivi watu wengine kama matumbo yanuma kwenda tu kuharisha hua mnaona ugumu gani? Kuliko kuharisha humu kwenye jamii forum asubuhi subuhi?

Huyo Makonda wa kwenye awamu ya vyeti feki wa nini sasa? Ana nini cha mno? Ana jipya gani?
Kwenye huu utawala wa democracy and rule of law Makonda wa nini? Si ataharibu tu?

Uelewe wakati wao hao akina Makonda kwenye chaguzi CCM walikuwa hawashindi bali walikuwa wanapora wewe unayemtaka huyo Makonda unamtaka aje aendeleze uporaaaaaaaaaaaaaji?

Kwa CCM hii ya mama Samia Hassani ushauri tu CCM inapata ushindi kwa nini waje akina Makonda waanze uporaji wao?
 
Toka majuzi kumekuwa na milio kutoka pande mbalimbali kuwa Mh.Makonda anatakiwa kurudishwa kwenye system kwasababu kuna mambo mengi yanamhitaji yeye.

Wengine hili tuliliona toka mwaka 2022 kuwa kuna gap anahitajika Mh.Makonda ili turudi kwenye siasa tulizozizoea na ambazo zilikuwa zinakipa chama uhai miaka yote.

Tambueni akirudi huyo upinzani kazi wanayo 2025. Ile ngumu mliyoipata kipindi cha Kinana na Nape kinarudi tena.View attachment 2787035
Amesafisha vyeti vyake tayari?
Je ametubu zile dhambi za uporaji kwa jina la baba?
 
Back
Top Bottom