Kwa hali inavyoendelea Kwa Sasa ni vyema CCM tukajitafakari. Ukweli ni kwamba hatuna watu wenye 'energy' ya kutosha, hatuna mtu ambae anaushawishi Kwa wananchi si tu Kwa muonekano ata Kwa kuongea. Nimetafakari upande wa Serikali mawaziri wetu wamekosa nguvu na ushawishi Kwa wananchi.
Kuirudisha CCM kwenye mstari, nashauri Dr Nchimbi tumpe kijiti Cha Katibu Mkuu CCM, Paul Makonda apewe Uenezi wa chama.
Kwenye Serikali, tunafahamu Doto Biteko kateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu kama mkakati wa kuvuna kura za Kanda ya ziwa 2024 na 2025. Hili wazo km ni la kweli basi halitafanikiwa sababu Biteko Hana ushawishi wowote katika Mikoa ya Kanda ya ziwa.
Ili kuleta mvuto mpya CCM Kanda ya Ziwa ni Bora Mzee Kalemani angeteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu kuliko huyo Biteko ambae hadi Sasa kishapoteana.
Kazi iendeleee!!