Msiwe watu wa kupayuka ovyo, kama kuna ufisadi ulifanyika awamu ya tano wekeni ushahidi wazi. Tuambieni namna pesa zilivyokwapuliwa na zilipofichwa

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Mbona mnakuwa kama watoto wadogo?

Mmesahau namna sakata la Escrow lilivyowekwa wazi? Tuliambiwa pesa namna zilivyo kwapuliwa na hata zilikofichwa. Vivyohivyo hata sakata la Kagoda na Epa.

Mnadai kuna ufisadi mkubwa ulitokea awamu ya tano. Tuambieni namna pesa zilivyokwapuliwa , nani alikwapua na sasa amezificha wapi. Serikali izirudishe.
 
Rais aliamua Tanroad ndio waagize mtambo wa kiwanda cha kuzalisha sukari akawapa bil 50, na hawakuleta na hakuwafanya kitu.
Kwa hiyo uamuzi wake pamoja na kuwapa hizo billioni ndio ushahidi?
Kama Tanroad "hawakuleta" na 'kutokufanya' ndio iwe na maana awamu ya tano walikwapua na kuficha?

wewe huoni huo ni utovu wa nidhamu badala ya ukwapuaji na kuficha?
 
Mbona mnakuwa kama watoto wadogo?

Mmesahau namna sakata la Escrow lilivyowekwa wazi? Tuliambiwa pesa namna zilivyo kwapuliwa na hata zilikofichwa. Vivyohivyo hata sakata la Kagoda na Epa.

Mnadai kuna ufisadi mkubwa ulitokea awamu ya tano. Tuambieni namna pesa zilivyokwapuliwa , nani alikwapua na sasa amezificha wapi. Serikali izirudishe.
Lisilo na ubishi ni Tshs 1.5 Trilion.
Mwulize CAG.
 
Kwani ile trillion 1.5 ilikwapuliwa na awamu ile ilikuwaje?
Kipindi kile hakukuwa na mwenye uthubutu wa kuweka mambo wazi
Kila kitu kitakua wazi
 
Mbona mnakuwa kama watoto wadogo?

Mmesahau namna sakata la Escrow lilivyowekwa wazi? Tuliambiwa pesa namna zilivyo kwapuliwa na hata zilikofichwa. Vivyohivyo hata sakata la Kagoda na Epa.

Mnadai kuna ufisadi mkubwa ulitokea awamu ya tano. Tuambieni namna pesa zilivyokwapuliwa , nani alikwapua na sasa amezificha wapi. Serikali izirudishe.
Mbona unayepwayuka ni wewe? Ufisadi mkubwa uliofanywa na awamu ya 5, si umedhihirishwa na uchunguzi wa CAG?

Si usubiri hatua gani zitafuatwa? Mbona unakua kama mwehu asiyejua kuwa katika kila jambo kuna taratibu zake? Kwani hata hiyo EPA na Escrow kila kitu kilifanyika siku moja?

Au unafikiri, na wewe ukifoka kama alivyokuwa anafanya marehemu utafanikiwa kuwaziba midomo watu kama marehemu alivyokuwa anafanya ili kuficha uovu wake, na wewe utafanikiwa?

Marehemu, uovu wake wote, ndani ya miaka 10 utawekwa wazi kwa kila mmoja.
 
Kwani ile trillion 1.5 ilikwapuliwa na awamu ile ilikuwaje?
Kipindi kile hakukuwa na mwenye uthubutu wa kuweka mambo wazi
Kila kitu kitakua wazi
Kichaa akiwa ameshika panga mkononi ilikuwa ngumu kumsogelea.
 
Back
Top Bottom