SankaraBoukaka
JF-Expert Member
- Jul 2, 2019
- 3,577
- 5,664
Kauli ya makamu mwenyekiti wa CHADEMA John Heche, kuhusu mfumo wa elimu wa Tanzania kuzalisha "mabingwa wa kukariri" badala ya wasomi halisi ni ukweli usiyo namashaka.
Vijana machawa walijikusanya na kutoa majibu kwa kauli hiyo, wakidai kuwa amekosea na kuidhalilisha Elimu ya Tanganyika.
Na chawa mmoja akauliza eti yeye (Heche) kasomea wapi? Sasa angejuaje ubovu wa Elimu bila naye pia kupitia hiyo Elimu?
Kwani chuo chetu kikuu kabisa si ndo mkufunzi mmoja mkubwa alikiita jalala? Sasa jalala linazalisha nini kama sis uchafu?
Ukichunguza kwa kina hoja ya Heche, tunaweza kujiuliza swali muhimu zaidi: Msomi unapataje muda wa kulumbana na mwanasiasa badala ya kutumia elimu yako kutatua matatizo ya jamii?
Kwanini nasema Heche yuko sahihi:
1. Tofauti Kati ya Msomi na Mwenye Cheti
Kauli ya John Heche ni ukweli mchungu ambao baadhi hawapendi kuusikia. Hili si suala la kushambulia au kutetea, bali ni fursa ya kutafakari.
Msomi wa kweli hana muda wa kulumbana na wanasiasa – ana muda wa kujenga hoja, kufanya tafiti, na kutoa suluhisho.
Badala ya kufanya Conference za kubadilisha ufahamu wa watumwa wenzenu, wanaojiita wasomi wanajipendekeza kwa mamlaka za NCHI.
Tukitaka taifa letu lipige hatua, basi lazima tubadilishe namna tunavyofikiri kuhusu elimu.
Tusiwe mabingwa wa kukariri, bali tuwe wabunifu, wachambuzi, na watatuzi wa matatizo. Huo ndio usomi wa kweli.
Hao wasomi wangekuwepo vitu muhimu kwenye nchi kama BANDARI na KIA vinavyozalisha visingezawadiwa kwa WAGENI.

- Msomi ni mtu anayefikiri kwa kina, anayejua kuchambua mambo na kutatua matatizo kwa kutumia maarifa.
- Mwenye cheti anaweza kuwa amemaliza chuo kikuu kwa mafanikio lakini hana uwezo wa kutumia elimu yake nje ya darasa.
- Mfumo wa elimu ukizalisha watu wanaotegemea kufaulu mitihani tu bila kuelewa dhana, basi tunakuwa na mabingwa wa kukariri, si wasomi.
- Elimu ya sasa inalenga zaidi kwenye "memory recall" badala ya "critical thinking".
- Wanafunzi wanapopinga kauli ya Heche kwa jazba badala ya hoja, wanathibitisha walichopingwa nacho.
- Msomi wa kweli humjibu mwanasiasa kwa hoja, utafiti, na ushahidi, si kwa maandamano au matusi mitandaoni.
- Wanafunzi wengi hujifunza ili wapate kazi serikalini au mashirika binafsi, si kwa kutatua matatizo ya jamii yao.
- Hili linaonyesha ukosefu wa dhamira ya kisomi – yaani kuona elimu kama chombo cha mabadiliko na si chombo cha kipato pekee.
- Tunahitaji mfumo wa elimu unaoendana na mahitaji ya sasa: ubunifu, ujasiriamali, sayansi ya kisasa, na ujuzi wa karne ya 21.
- Elimu yetu bado iko katika misingi ya kikoloni – kufundisha kutii badala ya kuhoji, kukariri badala ya kuelewa.
- Badala ya kupinga kwa maandiko, wanafunzi wa vyuo vikuu wangekuwa mstari wa mbele katika uvumbuzi, utafiti wa kisayansi, na miradi ya kijamii.
- Heche hakukosea – kinachotakiwa ni tafakari na hatua za kubadilika, si kulumbana na sauti ya tahadhari.