Msomi Unapataje Muda wa Kulumbana na Wanasiasa? Heche Yuko Sahihi. Tunazalisha Mabingwa wa Kukariri

SankaraBoukaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2019
Posts
3,577
Reaction score
5,664
Kauli ya makamu mwenyekiti wa CHADEMA John Heche, kuhusu mfumo wa elimu wa Tanzania kuzalisha "mabingwa wa kukariri" badala ya wasomi halisi ni ukweli usiyo namashaka.

Vijana machawa walijikusanya na kutoa majibu kwa kauli hiyo, wakidai kuwa amekosea na kuidhalilisha Elimu ya Tanganyika.
Na chawa mmoja akauliza eti yeye (Heche) kasomea wapi? Sasa angejuaje ubovu wa Elimu bila naye pia kupitia hiyo Elimu?
Kwani chuo chetu kikuu kabisa si ndo mkufunzi mmoja mkubwa alikiita jalala? Sasa jalala linazalisha nini kama sis uchafu?
Ukichunguza kwa kina hoja ya Heche, tunaweza kujiuliza swali muhimu zaidi: Msomi unapataje muda wa kulumbana na mwanasiasa badala ya kutumia elimu yako kutatua matatizo ya jamii?
Kwanini nasema Heche yuko sahihi:
1. Tofauti Kati ya Msomi na Mwenye Cheti
  • Msomi ni mtu anayefikiri kwa kina, anayejua kuchambua mambo na kutatua matatizo kwa kutumia maarifa.
  • Mwenye cheti anaweza kuwa amemaliza chuo kikuu kwa mafanikio lakini hana uwezo wa kutumia elimu yake nje ya darasa.
  • Mfumo wa elimu ukizalisha watu wanaotegemea kufaulu mitihani tu bila kuelewa dhana, basi tunakuwa na mabingwa wa kukariri, si wasomi.
2. Kukosa Mwamko wa Kufikiri kwa Kina
  • Elimu ya sasa inalenga zaidi kwenye "memory recall" badala ya "critical thinking".
  • Wanafunzi wanapopinga kauli ya Heche kwa jazba badala ya hoja, wanathibitisha walichopingwa nacho.
  • Msomi wa kweli humjibu mwanasiasa kwa hoja, utafiti, na ushahidi, si kwa maandamano au matusi mitandaoni.
3. Kujifunza kwa Ajili ya Ajira Siyo Suluhisho
  • Wanafunzi wengi hujifunza ili wapate kazi serikalini au mashirika binafsi, si kwa kutatua matatizo ya jamii yao.
  • Hili linaonyesha ukosefu wa dhamira ya kisomi – yaani kuona elimu kama chombo cha mabadiliko na si chombo cha kipato pekee.
4. Mahitaji ya Mageuzi ya Elimu
  • Tunahitaji mfumo wa elimu unaoendana na mahitaji ya sasa: ubunifu, ujasiriamali, sayansi ya kisasa, na ujuzi wa karne ya 21.
  • Elimu yetu bado iko katika misingi ya kikoloni – kufundisha kutii badala ya kuhoji, kukariri badala ya kuelewa.
5. Kujibu Kwa Vitendo, Siyo Kwa Maneno
  • Badala ya kupinga kwa maandiko, wanafunzi wa vyuo vikuu wangekuwa mstari wa mbele katika uvumbuzi, utafiti wa kisayansi, na miradi ya kijamii.
  • Heche hakukosea – kinachotakiwa ni tafakari na hatua za kubadilika, si kulumbana na sauti ya tahadhari.
Hitimisho:
Kauli ya John Heche ni ukweli mchungu ambao baadhi hawapendi kuusikia. Hili si suala la kushambulia au kutetea, bali ni fursa ya kutafakari.

Msomi wa kweli hana muda wa kulumbana na wanasiasa – ana muda wa kujenga hoja, kufanya tafiti, na kutoa suluhisho.
Badala ya kufanya Conference za kubadilisha ufahamu wa watumwa wenzenu, wanaojiita wasomi wanajipendekeza kwa mamlaka za NCHI.

Tukitaka taifa letu lipige hatua, basi lazima tubadilishe namna tunavyofikiri kuhusu elimu.
Tusiwe mabingwa wa kukariri, bali tuwe wabunifu, wachambuzi, na watatuzi wa matatizo. Huo ndio usomi wa kweli.
Hao wasomi wangekuwepo vitu muhimu kwenye nchi kama BANDARI na KIA vinavyozalisha visingezawadiwa kwa WAGENI.
 
Mkuu, mimi nana wazo la tofauti kwenye hili...! Mimi naona mfumo wetu wa elimu hauna shida kabisa...ila shida ipo kwa watu husika(wanaotaka kusoma) ikiwa na pamoja motivation wanazopewa katika kuliendea suala zima la elimu. Watu wakibadili mindset katika lengo la elimu na namna ya kueindea..hata bila kubidili chohote kingine tutaanza kuona matokeo chanya saana kwenye jamii zetu na taifa kwa ujumla.
 
Umeshafanya kauchunguzi kwenye hizo nchi zinaitwa zimeendelea ukaona kabla ya umri wa miaka 7 mpaka 8 watoto wanapata elimu ipi?
 

Bado tunahitaji kubadili mfumo wa elimu, tumesoma na tunafahamu, wapo waliobahatika kupitia mazingira wezeshi wana utofauti sana kwa uwezo wa fikra.

1: Ni wachache na wenye uwezo binafsi si wa zao halisi la mfumo wa elimu yetu unapeleka wahusika kwenye maeneo yetu ya kimaisha tukiwa na uelewa/knwoledge zaidi ya vyeti na maksi.

Hii ni sababu kubwa watu wanazunguka na vyeti kutafuta kazi waliyosomea badala ya kuhuisha elimu yao kwenye mazingira waliyopo na kuishi(master mazingira).

Walimu pia wanahusika kwenye kuandaliwa vyema.

2: Tuangalie mifumo ya ufundishaji.
Walimu wanaelekeza wakitengeneza mazingira gani kwa wanafunzi? Kuelewa au kukariri materials?
Hii ataielewa mtu aliyesoma teaching methodologies and coaching.

3: Mitihani yetu inatungwa kulenga nini?
Uelewa wa wanafunzi au kumbukumbu/kukariri?

4: Ni yapi mahusiano ya kielimu na kijamii kati ya mwalimu na mwanafunzi?
Mwalimu anaweka jitihada za kiasi gani kumwelewesha mwanafunzi? Anazo skills? Anahusika na perfomance ya mwanafunzi, darasa au shule? Matokeo yanamgusa/yanamhusu?
Au ndo inabidi hili darasa mpungue, mmekuja wengi mno?

5: Walimu wako tayari kwa majadiriano na wanafunzi bunifu au walio na challenge zaidi ya anachokielewa mwalimu?

6: Yako wapi mazingira bora ya kujifunza, mwalimu 1 wanafunzi 80-100?? Vitendea kazi vya mwalimu? Kwa wanafunzi, kama hawana mashimo ya vyoo ya kutosha? Madawati? Vyumba vyenye nafasi na usalama vs utulivu?

7: Wazazi tuko tayari kusaidia watoto wetu wanaokuwa na mawazo fikirishi?
Tumewawezesha wanafunzi kuhoji juu ya masomo na maisha au kukubali kilichopo tu?

8: Hili ndo limezaa viongozi wasio fikirishi na hawapendi mawazo fikirishi vs mbadala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…