Msongo wa mawazo, ugumu wa maisha wasababisha Msanii Q Jay kuranduka mpaka kuokota makopo

Msongo wa mawazo, ugumu wa maisha wasababisha Msanii Q Jay kuranduka mpaka kuokota makopo

hapana mkuu kuna watu wanapiga mzigo haswa kwa wahindi na wachina wanaondoka na ujira wa 4000 kwa siku na wanapiga kazi saa mbili asubuhi mpaka 12 jioni lakini hawajawa vichaa kwasababu ya malipo duni.
Jamaa alioa akaokoka akaachana na mziki wa dunia akawa anafanya kwenye kampuni flani ya kufunga majukwaa kuna kipindi alifanyiwa mahojiano na dullar kwenye planet bongo ya TV na alikuwa fresh tu miaka kama minne nyuma sasa sijui imekuaje
Inaumiza kaka jamaa alikuwa so talented yan ila Mungu ndo muweza atampigania
 
kuna maisha baada ya ustar kweli wajifunze kuwekeza....tupewe utaratibu tutachangia ila wajifunze
Wengi wa hawa mnao waita "mastar" hawana kipato cha maana ni mbwembwe tuu na kuuza sura kwenye tvii!!!!hawana lolote huishi maisha ya kuigiza
 
dah hao vijana wa wakali kwnza walikuwa na vipaji vya ukweli kabisa asee

lost talents..
 
Haya maisha jamani. Pole yake Mungu amsaidie apone tu kwa kweli..
 
Quality Joseph "Q Jay"


Huyu MTU nilikuwa namkubali sana, alikuwa chorus killer balaaa.. Kuna ngoma alishirikishwa na Joh Makini , nyingine D-Knob aliua Mbayaaa.



Yote kwa yote Kundi lao la wakali kwanza lililoundwa na Joslyn, Mackmua, na Qjay lilikua ni kundi ukisikia ngoma yao lazima utege sikio. Wimbo wao wa "SIFAI" Mpaka Leo ukipigwa lazima niache kila Kitu ninachofanya nitege sikio.



BTW kila limpatalo mtu ni funzo kwetu
 
Mi nasema, Sintorudi, Kwasababu uliniona Sifai,
Hata uje, Kwa Magoti, Sikubali mi nasema sitaki.

Mimi sina makosa, ila ni weweee,
Kwani ulivyofanya, Wewe Wajuaaaa,

Ukanifanya nilie, niteseke,.................
Na tena ukanikana, bila ya huruma, mbele ya mama yangu hey,
Sio poaaaaa,
Nasemaaaa,
Sirudiiiiiiii tena,
Ulivyoniumizaaa, Yatoshaaaaa
 
Duh uyu dogo alitokea kwenye msoto sana nakumbuka alikua anauza barafu kule Songea akapambana akatoboa na umaarufu juu leo tena karudia tena msoto basi ni balaa.
Tena afadhali ingekuwa ni msoto kuliko uchizi. Pole kwake.
 
Huyu alijiingiza pia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya..
 
Bila picha hata muweke namba sichangii ,uzuri wa kitenge lazima uvae lemba kichwani
 
Maombi Yangu ni msaada wangu tosha
Mungu akufadhili jinyenyekeze kwake atakuheshimisha
 
Back
Top Bottom