Msongo wa mawazo, ugumu wa maisha wasababisha Msanii Q Jay kuranduka mpaka kuokota makopo

Msongo wa mawazo, ugumu wa maisha wasababisha Msanii Q Jay kuranduka mpaka kuokota makopo

Daah... Aliacha muziki wa kidunia, akaokoka, akaanza kuimba injili halafu akagongewa mke kisha akapata depression halafu akaanza kuokota makopo.... Huyu angeendelea kuimba nyimbo za kidunia huenda angekuwa fresh tu kama mwenzake akina makamua na Josline....
 
Wanawake bana, halafu wametuundia vi- nyuzi kibao humu eti wanaume kwa michepuko.

Nyie mpaka mmefanya jamaa dishi kuyumba
 
hakuna kitu rahis kwa sasa kupata kama kudata in ngosha ze don voice
 
Daah! Mkali wa rnb Tz alikosea sana alipoamua kuachana na muziki na kuamua kuokoka. So sad
 
Mi nasema, Sintorudi, Kwasababu uliniona Sifai,
Hata uje, Kwa Magoti, Sikubali mi nasema sitaki.

Mimi sina makosa, ila ni weweee,
Kwani ulivyofanya, Wewe Wajuaaaa,

Ukanifanya nilie, niteseke,.................
Na tena ukanikana, bila ya huruma, mbele ya mama yangu hey,
Sio poaaaaa,
Nasemaaaa,
Sirudiiiiiiii tena,
Ulivyoniumizaaa, Yatoshaaaaa
Daah mkuu hatari sana
 
Msanii wa kizazi kipya aliyekuwa kundi la Wakali Kwanza, Q Jay kwa sasa amekuwa kama chokoraa kwani amekuwa anaokota makopo na kuongea vitu visivyoeleweka

Chanzo cha matatizo yote ni kutokana na ugumu wa maisha pia na msongo wa mawazo baada ya kuachana na familia yake.

Mkewe alichepuka, akabeba ujauzito wa mtu mwingine wakati akiwa naye, akamuaminisha kwamba mtoto alikuwa ni wake hadi anafikisha miaka sita ndio akajua kuwa mtoto sio wake.

Kwa sasa msanii huyu anaishi Bukoba, mkoani Kagera.

Daah mwenyezi Mungu amjaalie......ila kuna wakati jamaa aliokoka.
 
Picha si vizuri inabidi tumsitiri kijana mwenzetu
Wiki 2 zilizopita nilikuwa Club MINT bukoba, nilimuona QJay akiruka debe. Kwakweli nilimuhurumia, kimuonekano ni kama msela wa kitaa asiye na mbele wala nyuma, huwezi fikiri amewahi kuwa staa wa muziki. Halafu alikuwa anaruka pekeyake hakuna anayemjali, ukiwa huna hela noma sana maana sidhani hata kama kuna demu anamtaka[emoji23] [emoji23] . Nilikuwa na shemeji yenu tunapata kinywaji tukawa tunamchora tu, nikawa namwambia huyo jamaa aliwahi kuwa staa akawa anakataa[emoji23][emoji23][emoji23] nilipomkumbusha aliimba wimbo Fulani na Fulani ndo akamkumbuka, sema sio vizuri kumpiga picha maana ni kumchoresha zaidi. Halafu kuhusu hoja ya kuwehuka sina hakika, maana kama angekuwa amewehuka hata Club kusingekalika
 
Quality Joseph "Q Jay"


Huyu MTU nilikuwa namkubali sana, alikuwa chorus killer balaaa.. Kuna ngoma alishirikishwa na Joh Makini , nyingine D-Knob aliua Mbayaaa.



Yote kwa yote Kundi lao la wakali kwanza lililoundwa na Joslyn, Mackmua, na Qjay lilikua ni kundi ukisikia ngoma yao lazima utege sikio. Wimbo wao wa "SIFAI" Mpaka Leo ukipigwa lazima niache kila Kitu ninachofanya nitege sikio.



BTW kila limpatalo mtu ni funzo kwetu
Sifai ni wimbo wa QJay pekeyake. Labda unasema Natamani
 
Wiki 2 zilizopita nilikuwa Club MINT bukoba, nilimuona QJay akiruka debe. Kwakweli nilimuhurumia, kimuonekano ni kama msela wa kitaa asiye na mbele wala nyuma, huwezi fikiri anewahi kuwa staa wa muziki. Halafu alikuwa anaruka pekeyake hakuna anayemjali, ukiwa huna hela noma sana maana sidhani hata kama kuna demu anamtaka[emoji23] [emoji23] . Nilikuwa na shemeji yenu tunapata kinywaji tukawa tunamchora tu, nikawa namwambia huyo jamaa aliwahi kuwa staa akawa anakataa[emoji23][emoji23][emoji23], sema sio vizuri kumpiga picha maana ni kumchoresha zaidi. Halafu kuhusu hoja ya kuwehuka sina hakika, maana kama angekuwa amewehuka hata Club kusingekalika
Daaah!
 
Kuokota makopo sio uchizi siku izi, kuna watu wanaishi kwasababu ya hayo makopo.
 
Kupost hujafanya kosa mkuu achana na vistobe wanaodandia train kwa mbele kikubwa tushapata taarifa wenye uwezo wamsaidie tafadhali
 
Back
Top Bottom