Mstaafu Jakaya Kikwete anawashwa na nini?
Na Mjumbe wa Mkutano Mkuu
MWAKA 2017, aliyekuwa Rais wakati huo, John Pombe Magufuli, alisema: "wastaafu wengine hawachoki kusema, wana washwa washwa."
Magufuli alitoa kauli hiyo kuwalenga baadhi ya wastaafu ambao aliwaona kuwa wanaleta chokochoko dhidi ya serikali yake.
Mmoja wa wastaafu ambao walidhibitiwa na Magufuli wasilete chokochoko ni Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ambaye aliufyata na kukaa kimya.
Ingawa baadhi ya watu walimlaumu Magufuli kwa aina ya uongozi wake, uamuzi wake wa kumdhibiti Kikwete asilete mtafaruku kwenye serikali yake sasa wengine tumeanza kuuelewa.
Nikiwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika hivi karibuni, mimi ni miongoni mwa watu wengi ambao walikerwa na kauli ya Kikwete kwenye mkutano huo.
Alipoombwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, atoe neno kwa wajumbe, licha ya kudai kuwa ameshtukizwa, hakuwa amejiandaa kutoa hotuba,, Kikwete aliongea karibu nusu saa na kutoa maneno ambayo ni dhahiri kuwa aliyapanga kuyasema.
Kwenye hotuba yake, Jakaya alimwambia Rais Samia kuwa "asisikilize porojo za watu."
Kauli hiyo siyo sawa na ni mbaya sana kwani ni kama vile Jakaya eti anamfundisha kazi Rais Samia na anamsema hadharani kuwa Rais ni mtu wa kusikiliza porojo.
Jakaya aliongeza kuwa Rais Samia "asibabaishwe na maneno ya watu kuwa kuna wanasiasa vijana na wazee" wanafanya kampeni za chini kwa chini kuchuana na Dkt Samia kuwa mgombea urais wa CCM 2025.
Kauli hii inaashiria kuwa Jakaya anamsema Rais Samia kuwa ni mtu wa kubabaishwa na maneno na hajiamini kwenye nafasi yake.
Kikwete alisema "Rais wewe usibabaishwe na maneno haya" huku akitaka umma uamini kuwa Rais Samia ni kiongozi dhaifu anayebabaishwa na maneno ya porojo.
Wakati Rais Samia mwenyewe amewahi kuonya mara kadhaa kuhusu uwepo wa makundi ndani ya CCM yanayojipanga na urais 2025, Jakaya alikebehi tuhuma hizo na kusema kuwa huo ni "uongo" na maneno ya "hovyo hovyo."
Hii maana yake ni kuwa Jakaya anamsema Rais Samia kuwa anaamini maneno ya uongo.
Pia Jakaya alionekana kukosoa uongozi wa Rais Samia kama Mwenyekiti wa CCM kwa kusema kuwa katika kipindi chake Jakaya akiwa Rais na Mwenyekiti wa CCM hakutoa nafasi kwa "upuuzi" wa watu kusema uongo ndani ya chama.
Licha ya kusema kuwa siyo utamaduni kwa Rais anayemaliza muhula mmoja kupingwa na wagombea wengine ndani ya chama, alionya kuwa hilo linaweza kutokea "kama mambo yakiharibika sana."
Maneno hayo ya Jakaya yaliwashtusha wajumbe wengi kwani inaonekana kaongea kwa makusudi kutokana na uzoefu wake mkubwa kwenye chama na serikali.
Taarifa za ndani kutoka kwenye chama zinasema kuwa Jakaya na watoto wake wamekuwa wanaleta chokochoko za chini kwa chini dhidi ya serikali ya Rais Samia.
Anadaiwa pia kuwa Jakaya alifanya mipango kupanga safu yake ya viongozi wa CCM kupitia uchaguzi wa juzi wa vipngozi wa chama.
Ndiyo maana Magufuli aliamua kumdhibiti Jakaya na alitulia kweli kweli. Baada ya Rais Samia ametoa uhuru kwa wastaafu, sasa Jakaya ameamua kutumia uhuru huo kujaribu kukivuruga chama.
Nikiwa kama Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM namshauri Jakaya atulie zake Msoga kama mstaafu afuge tausi wake aliopewa na Magufuli.
Amuache Rais Samia aongoze kwa amani, kama yeye Jakaya alivyoachwa na Mkapa atawale kwa amani.
Kwani Jakaya anawashwa washwa na nini hasa?