Mstaafu Jakaya Kikwete anakerwa na nini?

Mstaafu Jakaya Kikwete anawashwa na nini?

Na Mjumbe wa Mkutano Mkuu

MWAKA 2017, aliyekuwa Rais wakati huo, John Pombe Magufuli, alisema: "wastaafu wengine hawachoki kusema, wana washwa washwa."

Magufuli alitoa kauli hiyo kuwalenga baadhi ya wastaafu ambao aliwaona kuwa wanaleta chokochoko dhidi ya serikali yake.

Mmoja wa wastaafu ambao walidhibitiwa na Magufuli wasilete chokochoko ni Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ambaye aliufyata na kukaa kimya.

Ingawa baadhi ya watu walimlaumu Magufuli kwa aina ya uongozi wake, uamuzi wake wa kumdhibiti Kikwete asilete mtafaruku kwenye serikali yake sasa wengine tumeanza kuuelewa.

Nikiwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika hivi karibuni, mimi ni miongoni mwa watu wengi ambao walikerwa na kauli ya Kikwete kwenye mkutano huo.

Alipoombwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, atoe neno kwa wajumbe, licha ya kudai kuwa ameshtukizwa, hakuwa amejiandaa kutoa hotuba,, Kikwete aliongea karibu nusu saa na kutoa maneno ambayo ni dhahiri kuwa aliyapanga kuyasema.

Kwenye hotuba yake, Jakaya alimwambia Rais Samia kuwa "asisikilize porojo za watu."

Kauli hiyo siyo sawa na ni mbaya sana kwani ni kama vile Jakaya eti anamfundisha kazi Rais Samia na anamsema hadharani kuwa Rais ni mtu wa kusikiliza porojo.

Jakaya aliongeza kuwa Rais Samia "asibabaishwe na maneno ya watu kuwa kuna wanasiasa vijana na wazee" wanafanya kampeni za chini kwa chini kuchuana na Dkt Samia kuwa mgombea urais wa CCM 2025.

Kauli hii inaashiria kuwa Jakaya anamsema Rais Samia kuwa ni mtu wa kubabaishwa na maneno na hajiamini kwenye nafasi yake.

Kikwete alisema "Rais wewe usibabaishwe na maneno haya" huku akitaka umma uamini kuwa Rais Samia ni kiongozi dhaifu anayebabaishwa na maneno ya porojo.

Wakati Rais Samia mwenyewe amewahi kuonya mara kadhaa kuhusu uwepo wa makundi ndani ya CCM yanayojipanga na urais 2025, Jakaya alikebehi tuhuma hizo na kusema kuwa huo ni "uongo" na maneno ya "hovyo hovyo."

Hii maana yake ni kuwa Jakaya anamsema Rais Samia kuwa anaamini maneno ya uongo.

Pia Jakaya alionekana kukosoa uongozi wa Rais Samia kama Mwenyekiti wa CCM kwa kusema kuwa katika kipindi chake Jakaya akiwa Rais na Mwenyekiti wa CCM hakutoa nafasi kwa "upuuzi" wa watu kusema uongo ndani ya chama.

Licha ya kusema kuwa siyo utamaduni kwa Rais anayemaliza muhula mmoja kupingwa na wagombea wengine ndani ya chama, alionya kuwa hilo linaweza kutokea "kama mambo yakiharibika sana."

Maneno hayo ya Jakaya yaliwashtusha wajumbe wengi kwani inaonekana kaongea kwa makusudi kutokana na uzoefu wake mkubwa kwenye chama na serikali.

Taarifa za ndani kutoka kwenye chama zinasema kuwa Jakaya na watoto wake wamekuwa wanaleta chokochoko za chini kwa chini dhidi ya serikali ya Rais Samia.

Anadaiwa pia kuwa Jakaya alifanya mipango kupanga safu yake ya viongozi wa CCM kupitia uchaguzi wa juzi wa vipngozi wa chama.

Ndiyo maana Magufuli aliamua kumdhibiti Jakaya na alitulia kweli kweli. Baada ya Rais Samia ametoa uhuru kwa wastaafu, sasa Jakaya ameamua kutumia uhuru huo kujaribu kukivuruga chama.

Nikiwa kama Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM namshauri Jakaya atulie zake Msoga kama mstaafu afuge tausi wake aliopewa na Magufuli.

Amuache Rais Samia aongoze kwa amani, kama yeye Jakaya alivyoachwa na Mkapa atawale kwa amani.

Kwani Jakaya anawashwa washwa na nini hasa?
Ndio siasa Mkuu na ulaji wa asali ulivyo.
 
Mstaafu Jakaya Kikwete anawashwa na nini?

Na Mjumbe wa Mkutano Mkuu

MWAKA 2017, aliyekuwa Rais wakati huo, John Pombe Magufuli, alisema: "wastaafu wengine hawachoki kusema, wana washwa washwa."
Sasa wewe ukianza kuweka tafsiri zako kwa kila linalosemwa inamaanisha nini?
 
Waswahilina hawajawahi kuwa na akili kubwa na ndo wamejazana huko fisiemu kwa sababu wamebobea kwenye ndumba, fitina na majungu, kwa hiyo hakuna la kushangaza hapa tuache muda uamaue ya mbeleni.....
Eh kijana kwa kweli uwe na adabu usitutukane wakati wewe unakuja mjini hata kutawadha tu ulikuwa hujui
 
Mtoa mada ameandika maneno mengi ila kuna kitu hajaelewa.
Lengo la JK sio kumponda Suluhu ila lengo la JK ni kumfagilia Suluhu aendelee kwa sababu wanammudu.
Wanahofia akiingia mtu mpya mfumo unaweza ukabadilika yakaja kama ya Marehemu Magu.
Kwani RA yuko wapi?
 
Naona sasa watu wameanza kumuelewa Ally Happi na ile kauli ya wastaafu wakae kimya. Nathubutu kusema yule mtoto ana maono ya mbali mno na anaijua ccm haswa hususani tabia za wazee wastaafu katika mambo yasiyo ya maana.

Ndio maana Magu pia aliamua kuwatuliza akafanya kazi zake, nadhani nae alikuwa anawajua watu kama hawa.

Kama Samia mwenyewe alikiri kuna watu wanajipanga kwa urais akawatoa kina lukuvi na kina Kabudi akawaweka kina January na sie raia wa nje tukamuambia ameruka maji amekanyaga oil chafu.

Jibu kamili la hii sinema nitalipata kama RC wa Bukoba akiondolewa au akiendelea kupeta. Kwamba mama yupo upande wa aliyosema JK kuwa hakuna na ni uzushi au hata yeye mama anaamini wapo na yupo na RC.
RC wa bukoba anahusikaje mkuu hapa sijaelewa
 
Magu alikuwa ni kichwa sana maana alishajua kwamba hii nchi bila ubabe haiwezi kutawalika wala kubadilika
 
Licha ya kusema kuwa siyo utamaduni kwa Rais anayemaliza muhula mmoja kupingwa na wagombea wengine ndani ya chama, alionya kuwa hilo linaweza kutokea "kama mambo yakiharibika sana."
Kaulii ya mambo kuharibika sana imekaa kimajungu na kichochezi. Kwanini aweke kichwani kwake mambo kuharibika sana?. Kwanini awe na mawazo hasi kichwani haswa anapomuongelea rais wa nchi?.

JK na kundi lake hawana nia safi na rais SSH na kibaya zaidi hakuna sauti nyingine yenye hekima inayokuwa juu yake ndani ya CCM kwa sasa.
 
Mstaafu Jakaya Kikwete anawashwa na nini?

Na Mjumbe wa Mkutano Mkuu

MWAKA 2017, aliyekuwa Rais wakati huo, John Pombe Magufuli, alisema: "wastaafu wengine hawachoki kusema, wana washwa washwa."

Magufuli alitoa kauli hiyo kuwalenga baadhi ya wastaafu ambao aliwaona kuwa wanaleta chokochoko dhidi ya serikali yake.

Mmoja wa wastaafu ambao walidhibitiwa na Magufuli wasilete chokochoko ni Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ambaye aliufyata na kukaa kimya.

Ingawa baadhi ya watu walimlaumu Magufuli kwa aina ya uongozi wake, uamuzi wake wa kumdhibiti Kikwete asilete mtafaruku kwenye serikali yake sasa wengine tumeanza kuuelewa.

Nikiwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika hivi karibuni, mimi ni miongoni mwa watu wengi ambao walikerwa na kauli ya Kikwete kwenye mkutano huo.

Alipoombwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, atoe neno kwa wajumbe, licha ya kudai kuwa ameshtukizwa, hakuwa amejiandaa kutoa hotuba,, Kikwete aliongea karibu nusu saa na kutoa maneno ambayo ni dhahiri kuwa aliyapanga kuyasema.

Kwenye hotuba yake, Jakaya alimwambia Rais Samia kuwa "asisikilize porojo za watu."

Kauli hiyo siyo sawa na ni mbaya sana kwani ni kama vile Jakaya eti anamfundisha kazi Rais Samia na anamsema hadharani kuwa Rais ni mtu wa kusikiliza porojo.

Jakaya aliongeza kuwa Rais Samia "asibabaishwe na maneno ya watu kuwa kuna wanasiasa vijana na wazee" wanafanya kampeni za chini kwa chini kuchuana na Dkt Samia kuwa mgombea urais wa CCM 2025.

Kauli hii inaashiria kuwa Jakaya anamsema Rais Samia kuwa ni mtu wa kubabaishwa na maneno na hajiamini kwenye nafasi yake.

Kikwete alisema "Rais wewe usibabaishwe na maneno haya" huku akitaka umma uamini kuwa Rais Samia ni kiongozi dhaifu anayebabaishwa na maneno ya porojo.

Wakati Rais Samia mwenyewe amewahi kuonya mara kadhaa kuhusu uwepo wa makundi ndani ya CCM yanayojipanga na urais 2025, Jakaya alikebehi tuhuma hizo na kusema kuwa huo ni "uongo" na maneno ya "hovyo hovyo."

Hii maana yake ni kuwa Jakaya anamsema Rais Samia kuwa anaamini maneno ya uongo.

Pia Jakaya alionekana kukosoa uongozi wa Rais Samia kama Mwenyekiti wa CCM kwa kusema kuwa katika kipindi chake Jakaya akiwa Rais na Mwenyekiti wa CCM hakutoa nafasi kwa "upuuzi" wa watu kusema uongo ndani ya chama.

Licha ya kusema kuwa siyo utamaduni kwa Rais anayemaliza muhula mmoja kupingwa na wagombea wengine ndani ya chama, alionya kuwa hilo linaweza kutokea "kama mambo yakiharibika sana."

Maneno hayo ya Jakaya yaliwashtusha wajumbe wengi kwani inaonekana kaongea kwa makusudi kutokana na uzoefu wake mkubwa kwenye chama na serikali.

Taarifa za ndani kutoka kwenye chama zinasema kuwa Jakaya na watoto wake wamekuwa wanaleta chokochoko za chini kwa chini dhidi ya serikali ya Rais Samia.

Anadaiwa pia kuwa Jakaya alifanya mipango kupanga safu yake ya viongozi wa CCM kupitia uchaguzi wa juzi wa vipngozi wa chama.

Ndiyo maana Magufuli aliamua kumdhibiti Jakaya na alitulia kweli kweli. Baada ya Rais Samia ametoa uhuru kwa wastaafu, sasa Jakaya ameamua kutumia uhuru huo kujaribu kukivuruga chama.

Nikiwa kama Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM namshauri Jakaya atulie zake Msoga kama mstaafu afuge tausi wake aliopewa na Magufuli.

Amuache Rais Samia aongoze kwa amani, kama yeye Jakaya alivyoachwa na Mkapa atawale kwa amani.

Kwani Jakaya anawashwa washwa na nini hasa?
Pascal tusaidie kujibu swali hili na mie niongeze swali je vijana wake ndio wale wa kimchongo?
 
Back
Top Bottom