Mstaafu Jakaya Kikwete anakerwa na nini?

Mstaafu Jakaya Kikwete anakerwa na nini?

Yaani umeaua kuwachonganisha kabisa hapa waziwazi?

Nisikilize kitu kimoja ndugu yangu. Mara zote tunapotokea kujidai kuwa sisi ni wajanja zaidi kuliko JK, yeye huwa anatukubali na kuamua kutulia halafu huko mbele ya safari tunakuja kukutana na kigingi ambacho huwa kinatukumbusha tena kuwa busara za JK ni za muhimu sana kwetu

JK ni Rais mstaafu, ameiongoza nchi hii kwa miaka 10 kamili, akastaafu, akaondoka madarakani huku akiiacha nchi ikiendelea kuwa salama, achilia mbali umaskini wetu. Tuna watu wawili tu kwa sasa wenye CV zenye sifa hiii, JK na Rais Mstaafu Mwinyi. Kwa hiyo ukimwondoa Rais mwinyi, JK anabaki kuwa mTanzania pekee mwenye CV ambayo waTanzania wote million 60 hatuna.

Tumsikilizeni JK kwa sababu kuna mambo ambayo Mungu huwa anapitishia kwake. Ni kwa sababu JK ana CV ambayo waTanzania wengine wote hatuna
Joka Kuu ndo mzizi wa matatizo yote nchini.
 
Mtoa mada ameandika maneno mengi ila kuna kitu hajaelewa.
Lengo la JK sio kumponda Suluhu ila lengo la JK ni kumfagilia Suluhu aendelee kwa sababu wanammudu.
Wanahofia akiingia mtu mpya mfumo unaweza ukabadilika yakaja kama ya Marehemu Magu.
Pole akili Yako fupi sana
 
Naona sahivi nyie,mnapeta tu

Mnatereza kama wingaaaa terezaaaa

Hongereni bana nchi iko vizuri

Uchumi na mambo mengine yako mukide

Ova
Furaha ya Watanzania wengi ni kwamba lile dubwasha liovu halipo duniani, usitegemee serikali kuja kukugawia pesa fanya kazi acha malalamiko kama mke wa pili
 
Mwacheni huyo mzee apumzike mtamuua kwa maneno ndugu watanzania... yupo pale kama mshauri... angekuwa mbaya tayari wasiojulikana wangekuwa washamuweka kitimoto na kumpa onyo kali na angekuwa kashatulia muda mrefu.. watu wengine mna uzushi sana! Sasa watoto wa JK wana nguvu gani na wao walete chokochoko kwenye serikali?!....Kwani ni wao tu ndo baba yao alikuwa Rais hapa nchini?! Mzee mwinyi hana watoto?! Mzee Mkapa marehemu?! Mzee Nyerere?! Mzee Magufuli?!

Kusoma hamjui hata picha kutazama jamani 😂

#SioKwaUbaya
 
Licha ya kusema kuwa siyo utamaduni kwa Rais anayemaliza muhula mmoja kupingwa na wagombea wengine ndani ya chama, alionya kuwa hilo linaweza kutokea "kama mambo yakiharibika sana."
Yani anamaanisha kwamba sasaivi mambo yanaharibika lakini hayaja haribika sana.
 
Mstaafu Jakaya Kikwete anawashwa na nini?

Na Mjumbe wa Mkutano Mkuu

MWAKA 2017, aliyekuwa Rais wakati huo, John Pombe Magufuli, alisema: "wastaafu wengine hawachoki kusema, wana washwa washwa."

Magufuli alitoa kauli hiyo kuwalenga baadhi ya wastaafu ambao aliwaona kuwa wanaleta chokochoko dhidi ya serikali yake.

Mmoja wa wastaafu ambao walidhibitiwa na Magufuli wasilete chokochoko ni Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ambaye aliufyata na kukaa kimya.

Ingawa baadhi ya watu walimlaumu Magufuli kwa aina ya uongozi wake, uamuzi wake wa kumdhibiti Kikwete asilete mtafaruku kwenye serikali yake sasa wengine tumeanza kuuelewa.

Nikiwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika hivi karibuni, mimi ni miongoni mwa watu wengi ambao walikerwa na kauli ya Kikwete kwenye mkutano huo.

Alipoombwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, atoe neno kwa wajumbe, licha ya kudai kuwa ameshtukizwa, hakuwa amejiandaa kutoa hotuba,, Kikwete aliongea karibu nusu saa na kutoa maneno ambayo ni dhahiri kuwa aliyapanga kuyasema.

Kwenye hotuba yake, Jakaya alimwambia Rais Samia kuwa "asisikilize porojo za watu."

Kauli hiyo siyo sawa na ni mbaya sana kwani ni kama vile Jakaya eti anamfundisha kazi Rais Samia na anamsema hadharani kuwa Rais ni mtu wa kusikiliza porojo.

Jakaya aliongeza kuwa Rais Samia "asibabaishwe na maneno ya watu kuwa kuna wanasiasa vijana na wazee" wanafanya kampeni za chini kwa chini kuchuana na Dkt Samia kuwa mgombea urais wa CCM 2025.

Kauli hii inaashiria kuwa Jakaya anamsema Rais Samia kuwa ni mtu wa kubabaishwa na maneno na hajiamini kwenye nafasi yake.

Kikwete alisema "Rais wewe usibabaishwe na maneno haya" huku akitaka umma uamini kuwa Rais Samia ni kiongozi dhaifu anayebabaishwa na maneno ya porojo.

Wakati Rais Samia mwenyewe amewahi kuonya mara kadhaa kuhusu uwepo wa makundi ndani ya CCM yanayojipanga na urais 2025, Jakaya alikebehi tuhuma hizo na kusema kuwa huo ni "uongo" na maneno ya "hovyo hovyo."

Hii maana yake ni kuwa Jakaya anamsema Rais Samia kuwa anaamini maneno ya uongo.

Pia Jakaya alionekana kukosoa uongozi wa Rais Samia kama Mwenyekiti wa CCM kwa kusema kuwa katika kipindi chake Jakaya akiwa Rais na Mwenyekiti wa CCM hakutoa nafasi kwa "upuuzi" wa watu kusema uongo ndani ya chama.

Licha ya kusema kuwa siyo utamaduni kwa Rais anayemaliza muhula mmoja kupingwa na wagombea wengine ndani ya chama, alionya kuwa hilo linaweza kutokea "kama mambo yakiharibika sana."

Maneno hayo ya Jakaya yaliwashtusha wajumbe wengi kwani inaonekana kaongea kwa makusudi kutokana na uzoefu wake mkubwa kwenye chama na serikali.

Taarifa za ndani kutoka kwenye chama zinasema kuwa Jakaya na watoto wake wamekuwa wanaleta chokochoko za chini kwa chini dhidi ya serikali ya Rais Samia.

Anadaiwa pia kuwa Jakaya alifanya mipango kupanga safu yake ya viongozi wa CCM kupitia uchaguzi wa juzi wa vipngozi wa chama.

Ndiyo maana Magufuli aliamua kumdhibiti Jakaya na alitulia kweli kweli. Baada ya Rais Samia ametoa uhuru kwa wastaafu, sasa Jakaya ameamua kutumia uhuru huo kujaribu kukivuruga chama.

Nikiwa kama Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM namshauri Jakaya atulie zake Msoga kama mstaafu afuge tausi wake aliopewa na Magufuli.

Amuache Rais Samia aongoze kwa amani, kama yeye Jakaya alivyoachwa na Mkapa atawale kwa amani.

Kwani Jakaya anawashwa washwa na nini hasa?
Wewe una chuki binafsi tu na JK.....hizo chuki hazikusaidii lolote tafuta tu maisha.
 
""Taarifa za ndani kutoka kwenye chama zinasema kuwa Jakaya na watoto wake wamekuwa wanaleta chokochoko za chini kwa chini dhidi ya serikali ya Rais Samia.

Anadaiwa pia kuwa Jakaya alifanya mipango kupanga safu yake ya viongozi wa CCM kupitia uchaguzi wa juzi wa vipngozi wa chama".


Nilivyoona tittle yako tu nikataka nije niliongee hili maana nina ushahidi nalo bahati nzuri umeliongelea,kiukweli nimesikitika sana huyu mzee sijui bado anataka nini katika nchi hii.

Kuna mama yetu alikuwa mwenyekiti mkoa X alikuwa swahiba sana na mama samia na nimeshawahi kumsikia wakifurahi na kucheka kwenye simu live na mheshimiwa prezidaa lakini jamaa kaforce mpaka jina halijarudi kapanga watu wake.

Halafu mama ni alikuwa ni kjpenzi cha watu ana roho nyeupe sana yule mama,wajumbe asilimia 70 ilibaki kidogo tuharibu kura kwa kuandika jina la yule mama kwenye uchaguzi sema busara zilitumika tu kututuliza,lakini hahathahata hivyo mwisho wa siku tumemchapa mtu wake tumempigia kura mtu tusiyemtaka hili kumkomoa
Una hasira sababu unayempenda kakosa cheo.
 
Una hasira sababu unayempenda kakosa cheo.
Mimi sitegemei cheo cha mtu mzee wa kazi siasa tunafanya temporary kwani ndio tumelelewa kwenye mazingira ya siasa tangu utotoni,tupo kwenye siasa kama hobby tu lakini sitegemei kupata chochote maana kazi ninayofanya inanilipa mara kumi zaidi ya huo ujumbe wa halmashauri kuu ya Mkoa..Baba yangu kawa mwenyekiti wa mkoa wa chama miaka kibao hakuna alichoambulia mama yangu pia Katibu wa UWT wilaya miaka na miaka unadhani nitakuwa na nafasi ya kutegemea cheo cha mtu nisiyemfahamu?!
 
Mimi sitegemei cheo cha mtu mzee wa kazi siasa tunafanya temporary kwani ndio tumelelewa kwenye mazingira ya siasa tangu utotoni,tupo kwenye siasa kama hobby tu lakini sitegemei kupata chochote maana kazi ninayofanya inanilipa mara kumi zaidi ya huo ujumbe wa halmashauri kuu ya Mkoa..Baba yangu kawa mwenyekiti wa mkoa wa chama miaka kibao hakuna alichoambulia mama yangu pia Katibu wa UWT wilaya miaka na miaka unadhani nitakuwa na nafasi ya kutegemea cheo cha mtu nisiyemfahamu?!
We ni muhaya?! 😃 huoni sasa kama unajianika wewe ni nani humu?! Kuna watu wataalam wa ku-connect dots shauri yako... sifa zitakuponza
 
We ni muhaya?! 😃 huoni sasa kama unajianika wewe ni nani humu?! Kuna watu wataalam wa ku-connect dots shauri yako... sifa zitakuponza
Mimi hata picha yangu mkitaka nawawekea..tangu 2015 mpaka leo nimekuwa nikikutana na wanajamii forums kibao nje ya forums so hakuna cha ajabu hakuna mtu ninayemuhofia humu maana watu kibao wananijua
 
Mimi hata picha yangu mkitaka nawawekea..tangu 2015 mpaka leo nimekuwa nikikutana na wanajamii forums kibao nje ya forums so hakuna cha ajabu hakuna mtu ninayemuhofia humu maana watu kibao wananijua
Good for you! 😊
 
Natamani mzee JK 2025 aingie ulingoni hata kwa kubadili katiba...
(3) "Mtu aliyewahi kuwa Rais wa Tanganyika au Zanzibar
hatapoteza sifa za kugombea na kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano kwa sababu aliwahi kushika nafasi ya madaraka ya Rais wa
Tanganyika au Rais wa Zanzibar.
(4) Endapo Makamu wa Rais atashika nafasi ya madaraka ya
Rais kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 76 kwa kipindi kisichozidi
miaka mitatu, ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais kwa vipindi
viwili, lakini kama atashika nafasi ya madaraka ya Rais kwa muda
wa miaka mitatu au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya madaraka
ya Rais kwa kipindi kimoja tu. "

Hiyo ni katiba mpya inavyosema.
So hakuna lisilowezekana chini ya jua hili.
 
Back
Top Bottom