Joan lewis
JF-Expert Member
- Jan 3, 2019
- 993
- 1,463
Mimi nilimkubali JK tangu Mwendazake alipoingia madarakani. Hata wabunge mwaka ule nadhan 2016 waliposema tumekumiss alipoingia bungeni ni dhahiri kwamba tuliokuwa hatumwelewi kabla hatuna uzoefu wake. Toka mwendazake alipoingia mpk leo na kesho na milele sitathubutu kuacha kumwelewa.Yaani umeaua kuwachonganisha kabisa hapa waziwazi?
Nisikilize kitu kimoja ndugu yangu. Mara zote tunapotokea kujidai kuwa sisi ni wajanja zaidi kuliko JK, yeye huwa anatukubali na kuamua kutulia halafu huko mbele ya safari tunakuja kukutana na kigingi ambacho huwa kinatukumbusha tena kuwa busara za JK ni za muhimu sana kwetu
JK ni Rais mstaafu, ameiongoza nchi hii kwa miaka 10 kamili, akastaafu, akaondoka madarakani huku akiiacha nchi ikiendelea kuwa salama, achilia mbali umaskini wetu. Tuna watu wawili tu kwa sasa wenye CV zenye sifa hiii, JK na Rais Mstaafu Mwinyi. Kwa hiyo ukimwondoa Rais mwinyi, JK anabaki kuwa mTanzania pekee mwenye CV ambayo waTanzania wote million 60 hatuna.
Tumsikilizeni JK kwa sababu kuna mambo ambayo Mungu huwa anapitishia kwake. Ni kwa sababu JK ana CV ambayo waTanzania wengine wote hatuna
Nawashauri na wengine. Maana majuto ni mjukuu.