Mstaafu wa Jeshi atuhumiwa kuua kwa risasi kisa mgogoro wa mipaka

Ukubwa wa eneo sasa linalogombewa
Utakuta vihatua 3,4 tu
Na siku zote ugomvi wa ardhi huwa mmbaya sana,kama watu hamuelewani iko siku ardhi hiyo hiyo
Itammeza mtu

Ova
Ni upuuzi kugombea futi 3 za mpaka na kuwekeana uhasama hata kufikia hatua ya kuuwana. Futi 3 ambazo hata kuchimba kaburi hazitoshi. Mimi jirani akisema huku kwangu, nikatumia njia yote kumwelewesha kuwa sio kwake, akang'ang'ana na kuhamaki na njia zote kusuluhisha zimegoma. Namwachia.
 
Afu kaeneo kanakotumika kukuzika nikadogo sana. Mnauana kwa ajili ya ardhi?
Unaenda jela na kuacha familia yako kwa ajili ya ardhi?
Na ana sevente wan years ndio hivyo Tena ataozea jela. Kaua halafu kakimbia kwenda kujificha. Murder case siyo ya kuchezea hata kwenye nchi judiciary system ni dhaifu Bado tu murder case ni serious.
 
Mipaka ni hatari. Vijijini ndiyo hatari kabisa. Maana mipaka ya vijijini huwa hainyooki. Hapa kimeingia mdani, hapa kimetoka nje. Na watu wa vijijini uelewa ni sifuri kabisa.
 
Kupakana na askari yeyote wa jeshi la Tanzania ni changamoto kubwa sana. Wale wanao pakana nao nikiwemo mimi tulio wengi itakuwa tunajuta sana. Japo si wite, ila walio wengi wao wanajifanya wababe sana.
 
Akisha hukumiwa kifungo cha maisha familia hiyo hiyo itaiuza ardhi(ya mstaafu) na kwenda kuishi mbali.
Ila kuna majirani wanakera jamani!
Very true. Sasa yeye ataozea jela, na watoto/ndugu hawataitaka hiyo ardhi tena iliyosababisha mauaji. Kuna watu wajinga sana dunia hii. Sasa sijui kapata faida ganihuyo aliyoua. Alidhani kwenda kujificha kungemsaidia?
 
Umeandika utafikiri umekurupushwa, tulia andika uzi wako kwa mpangilio hata mtu akisoma anaelewa.
 
Alipo niacha hoi,kwamba kaua harafu kakimbia kwenda kujificha!!yeye alifikiri ameua kuku!!Hawa watu ni wepesi sana,Richa ya kujitapa na magwanda yao
 
Nipo msibani hapa wazo. Kesho tutazika. NADHANI HUZUNI NA SONONEKO LA FAMILIA HII NI KUBWA KULIKO TUNAVYODHANI.
Hilo eneo jamaa alienda kuangalia ni la rafiki yake yupo nje ya nchi, alimuomba akaangalie. Huyo babu wa miaka 71 kwa wenge akadhani huyu ni mmiliki nikiua huyu namiliki ardhi yote hii...POMBE NA BANGI VINAATHIRI SANA WANAJESHI.
 
Nimetoka hapo muda sio mrefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…