Mtaniwia radhi kwa ukubwa wake kutokana na hii mada.. Natambua wengi wenu mtakereka na maudhui yake na baadhi mtaudhika Sana..! Lakini kupitia mada hii naomba msijichukulie Kama walengwa bali kama wanafunzi wanaohitajika kujifunza kitu kizuri
1. Kutambua dhima ya social media
Tambueni ya kwamba hapo sio mahali pa kujianika na kujifunua maisha yako binafsi kupitia maandishi ama mitazamo yako! Fanya vyote lakini linda sana privacy yako..! Mitandao haifuti kitu
2. Tafuta faraja, tafuta msaada, omba ushauri kwa watu sahihi, uliowasoma vya kutosha na unaoweza kuwaamini.. Kwamba kwa kulinda privacy lakini kwa kukulinda na kukusaidia kwa usahihi
3.Epukeni kuwaamini watu hasa wa jinsia yenu wenyewe ambao hamfahamiani zaidi ya kwenye hizi social media.. Mna tabia za kike za kumwamini mtu kwa haraka na kuanza kuwajadili wengine ama kujadili mambo ambayo hayana afya
4. Itendeeni haki slogan ya Great thinker..! Kuna mengi ya kujadili dunia inaenda kasi sana.. Epukeni majungu na kuwajadili watu muda wote kila mnapo interact.. Kumbukeni small minds discuss people
5. Heshimuni faragha za watu waliowapeni nafasi ya kuwasiliana nanyi.. Sio jambo la busara kuanza kutumiana screenshots za mawasiliano ya wengine.. Kikulacho ki nguoni mwako..! Screenshot moja ikishatumwa ndio imeshaanza safari ndefu ya kufika mbali
6. Moyo wa mtu ni kiza kinene.. Umdhaniaye ni rafiki kumbe ndiye adui yako no moja . akili kichwani mwako
7. Epukeni kukwazika na kuumizwa na vitu vya kipuuzi.. Umeingia mtandaoni mwenyewe utatoka mwenyewe.. Uliokuta na watakaokukuta sio malaika.. Hutapendwa na wote na hutachukiwa na wote..! Ukiumia kwakuwa fulani hakupendi utakuwa hujajitendea haki kabisa
8. Wabeba mafaili ya watu.. Hivi mnakuwa hamna kazi za kufanya au ni ukosefu wa akili hekima na maarifa.. Kujitapa kwamba una mafaili ya watu ni upuuzi mwingine wa kiwango cha lami
9. Epukeni kutengeneza maadui wapya.. Epukeni kuwachagulia watu marafiki ama mamdui.. Anayekupenda nenda naye kwa tahadhari.. Asiyekupenda chapa lapa.. Wewe sio pesa upendwe mpaka na vichaa
10. Bifu nyingi za JF zimesababishwa na wengi kutojitambua, akili finyu maono mafupi na ushamba wa kudhani watu wanaokutana nao social media ndio watu halisi na wa kuaminika sana..
Kuwa GT sio title ni matendo..!
Good night..!